Semarang
Member
- Jun 30, 2016
- 35
- 47
Salam wana JF,
Najua hapa jamiiforums ni sehemu ambayo viongozi mbali mbali na wadau mbali mbali hupita kupata taarifa na malalamiko kutoka kwa wananchi.
Mabaharia wa kitanzania tunaofanya kazi nje ya nchi tunasikitika kukosa msaada wa serikali yetu sikivu.
Mabaharia wa kitanzania waliokua wanaofanya kazi kwenye meli yenye flag state ya Panama wameshushwa melini kwa sababu mkataba ulioko baina ya Tanzania na Panama umekwisha na Tanzania haikuupa kipaumbele tena kuurudisha,hivyo mabaharia wengi wa kitanzania wamekosa kazi kwa kushushwa melini,serikali iuangalie tena ili mabaharia wapate kazi tena.
Mabaharia wengi wa kitanzania tumerudishwa Tanzania kwa sababu vyeti vyetu vimepitwa na wakati kwa maana bado tunatumia vyeti vya STCW 1978 wakati duniani huko vyeti vinavotambulika ni vya Manilla amendment 2010.
IMO ambayo ipo chini ya UN ilitangaza mwisho wa kutumia vyeti vya STCW 1978 ni 2012 lakini serikali ya Tanzania haikutilia manani suala hio kwa kua ubaharia hauthaminiwi nchi hii.
IMO imeeka deadline mpaka January 2017 vyeti vya STCW 1978 vitakua havitambuliki kabisa.DMI chuo cha ubaharia ikaanzisha course hii mpya ya manilla amendment iitwayo refresher kama wiki 4 zilizopita ili mabaharia wapate vyeti hivyo vipya.usumbufu mkubwa uliojitokeza ni kuwa vyeti havitapatikana mpaka mwakani ambapo mwenye mamlaka ya kutoa vyeti hivyo ni Sumatra.
Vyeti vya ubaharia Tanzania hutolewa na Sumatra ambapo huko kuna usumbufu mkubwa sana.Iweje vyeti vitoke mwakani wakati ndivyo vilivyoturejesha nyumbani!!! Tutaishi vipi mabaharia bila kazi maana hatuwezi kupata kazi bila ya vyeti vipya!
Je ni haki kukaa miezi 6 juu bila ya kazi ambapo tuna familia zinatutegemea!!
Kwa wenye mamlaka naomba muliangalia jambo hili kwa jicho la huruma ili tuweze kuvipata vyeti vyetu maramoja na si mwakani kama wanavodai Sumatra..
Wasalaam..