Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
DED BAGAMOYO ALILIA BANDARI
Na: Edgar Nazar, Bagamoyo
MKURUGENZI mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda ametoa kilio kwa Naibu waziri wa uchukuzi kuwa bandari ya Bagamoyo inaliliwa sana na wana Bagamoyo kwa ajili ya usafiri kwenda Zanzibar na ikijengwa itafungua milango ya uchumi kwa wakazi wake.
Kilio hicho amekitoa Juni 25, 2024 wakati wa kilele cha siku ya mabaharia Duniani ambapo kitaifa ilifanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Nianjema wilayani Bagamoyo.
Amesema kuwa wakazi wa Bagamoyo mara kwa mara wanatamani waone boti na meli za usafiri zije na ziwe zinaelea katika maeneo ya fukwe za Bagamoyo tayari kubeba mizigo na abiria kutoka mjini hapa kuelekea Zanzibar, Tanga na Pemba.
"Wakazi wa Bagamoyo kwa niaba yangu nawawasilishia kilio chao cha uhitaji mkubwa wa bandari ili boti za usafiri ukiwepo utawezesha kuinua uchumi" amesema Mkurugenzi Serenda.
Amesema kuwa anaimani kubwa na serikali ya daktari Samia Suluhu Hasani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga fedha za ujenzi wa bandari hiyo ili kuinua uchumi wa buluu.
Naibu waziri wa Uchukuzi Bw. David Mwakiposa Kihenzile nae alitoa wito kwa mabaharia nchini kujiendeleza kielimu ili waweze kuwa na soko la kazi ndani na nje ya Tanzania.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa kilele cha sherehe za mabaharia nchini iliyofanyika mjini Bagamoyo.
"Nitoe wito kwa mabaharia nchini niwatake msome na mjiendeleze kielimu kimataifa ili kazi hii ya ubaharia muweze kuifanya nchi yoyote ambayo inajihusisha na usafiri wa maji kwani soko lipo wazi" amesema Naibu waziri huyo wa uchukuzi.
Amesema kuwa siku hii ya mabaharia Duniani huwa inafanyika kwa ajili ya kupokea changamoto zao na kuzifanyia kazi pamoja na kujua serikali imefanya nini katika nyanja hii ya usafirishaji kwenye maji.
Amesema kuwa serikali ya awamu hii ya sita ni sikivu na itaendelea kuwahudumia wananchi wake kuhakikisha sekta ya usafiri wa maji inakuwa kwa kuongeza tija kwenye sekta hii.