Kilimoo cha miti ya mbao Kibondo

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
156
Mkuu, mambo vipi?
Naomba ushauri wako. Kuna eneo naweza kupata Kibondo (Kigoma), nahitaji nipande miti ya mbao.

Nimeambiwa miti hii inastawi Kibondo.
1)Acrocarpus
(2)Casuarina spp
(3)Cedrela odorata
(4)Pinus
(5)Cypres
(6)Acacia mangium

Naomba kujua kwa ujumla ni miti ya aina gani katika hiyo ina-return kubwa (yaani ina faida kubwa na ndani ya muda mfupi)?

Pia nahitaji kujua mchanganuo wa kila aina ya mti hapo juu katika vitu hivi:
(a)Inachukua miaka mingapi (minimum & maximum) kufikia kuvunwa?

(b)Inapandwaje (umbali kati ya mche na mche na umbali kati ya mstari na mstari?

(c)Mti mmoja ukikomaa baada ya hiyo miaka una uwezo wa kutoa mbao ngapi (minimum & maximum)?

(d)Mti mmoja una uwezo wa kutoa mbao za sh. ngapi kwa bei ya sasa (minimum & maximum)?

(e)Mti mmoja ukishakomaa unauzwa kwa bei gani (minimum & maximum) ili mnunuzi apasue mwenyewe?
 
Mkuu nimekuja, asante kwa kuniita.

Naomba niwape rotation age ya miti iliyotajwa hapo juu sawa na watalaamu wanavyosema.
1. Cedrella odorata - 26 - waswahili wanavuna 13/16 yrs
2. Cyprus - 28 - wanavuna kuanzia 16yrs
3. pines - 26 - tunavuna kuanzia 11/16 yrs
4. casuarina - 26 - soko la mbao utata
5. acrocarpus - 23 , waswahili tunavuna kuanzia 13/14yrs

Kwa ufupi, ili upate ubao bora kwa miti hiyo, ni lazima ufikishe rotation age ya kila mti, hiyo miaka tunayovuna sisi Waswahili, ni kwa sababu ya njaa na maandalizi duni ya project zetu.

Tuje kwa mwenye uzi, wewe ulitaka uvune baada ya muda gani ili tukutafutie croned spp za Mlingoti na pinus patella?
 
Mkuu, Malila, asante sana!
Sihitaji kuvuna mimi, nataka wanangu waje wavune mkubwa wao kabisa akiwa na miaka 25 (miaka miwili/ mitatu baada ya kuhitimu shahada ya kwanza) i.e miti (hususan Pines na/ Cyprus) ikiwa na umri wa miaka 15-18.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom