Kilimo, soko na faida za Uyoga

Habari, mimi ni mjasiriamali nipo Bukoba najishughulisha na kilimo cha uyoga ila nina changamoto moja inayonisumbua, kuna fangasi wanashambulia mifuko ya uyoga ikiwa katika chumba cha giza. Naomba msaada kwa yeyote anayejua zaidi kuhusu ili.
 
Wapendwa naomba mwenye kujua zinapopatikana mbegu za uyoga anijuze tafadhali nina shida nazo.mi nipo moshi.tnx
 
Wapendwa naomba mwenye kujua zinapopatikana mbegu za uyoga anijuze tafadhali nina shida nazo.mi nipo moshi.tnx

hizo mbegu za uyoga nimeteseka nazo xx mwezi wa 5 tena wataalam wenyewe wanatoka sua morogoro kila ukienda mbegu zimeharibika sasa nimeamua kuachana kabisa na kilimo hicho kwan nimekula hasara hela imeenda mbegu hakuna udogo umeharibika maandaliz yote ni bureee..then tunasema tuna chuo cha kilimo shameful saaana......!
 
hizo mbegu za uyoga nimeteseka nazo xx mwezi wa 5 tena wataalam wenyewe wanatoka sua morogoro kila ukienda mbegu zimeharibika sasa nimeamua kuachana kabisa na kilimo hicho kwan nimekula hasara hela imeenda mbegu hakuna udogo umeharibika maandaliz yote ni bureee..then tunasema tuna chuo cha kilimo shameful saaana......!
Pole sana mkuu sua wako makini naamini taarifa walizokupa ni sahihi na sio longolongo jaribu tengeru kama alivyoshauri mdao hapo juu kilimo chema.
 
Uyoga ni Mushroom

Google kwa kupata jinsi ya kulima na faida zake (how to farm mushroom na advantages of farming mushroom) nadhani hapo kwenye faida ni kwamba inachukua eneo dogo sana...

Kuhusu soko lake kwa Tanzania na sehemu ya kupata mbegu hapo nadhani wengine watajazia..
 
Habari wanaJF. Nimepata mafunzo ya kilimo cha uyoga aina ya oyster (mamama) na ninajipanga kujaribu. Naomba kujua soko lake likoje kwa hapa Dar. Mambo yakienda vizuri nategemea kuanza kuvuna mwishoni mwa November. Asanteni.
 
Nimeanza rasmi kilimo cha kuotesha uyoga. Nimegundua kuwa shughuli hizi hazijazoeleka sana na jamii ya watanzania . Natoa wito kwa wakulima wenzangu ambao wangependa kupata maendeleo kupitia kilimo hiki basi tuungane na kuionesha serikali kuwa kilimo cha uyoga kina faida keme kem kuanzia kuwa rafiki wa mazingira, lishe , tiba na uchumi. imeona kuna changamoto kibao ambazo tukiziongea kwa pamoja zitakwisha na hatimaye kuboresha kilimo hiki kwa faida ya jamii. Wenzetu hata wa nchi jirani kama Kenya na Zimbabwe wamepiga hatua kubwa katika kuendeleza kilimo hicho
 
hongeraa mkuu kwa kuanza rasmi mm nilichemka huko changamoto kibao wataalam wenyewe majanga tu niliandaa mbolea kwa ajili ya kupanda uyoga maajabu mbegu nilifuatilia miezi sita mtaalam anatoka chuo cha kilimo SUA yani nilistaajabu sana hela yangu imeenda mbegu sijapata kila siku mbegu zinaharibika unaambiwa subir tena ...Tanzanian we are not serious kabisa niliamua kuacha kabisa ...
 
Uko wapi mkuu,
Mimi nilimuona dadaa mmojaa katika kipindi cha AMKA TBC anaitwa Upendo anaishi changanyikeni Dar, anasema amefanikiwa sana na alikuwa anahamasisha watu waanzishe kilimo hiki,
 
Back
Top Bottom