Kilimo, soko na faida za Uyoga

Habari zenu wanajamvi?
Kwanza kabisa ninaomba kama kuna mwenye elimu juu ya kilimo cha uyoga,
;kuanzia upatikanaji wa mbegu,
:namna ya kupanda
.muda wa kulima mpaka ukomae(uwe tayari kuvunwa)
:na pia masoko yake ndani na nje ya Tanzania,
Asanteni kwa mchango wenu.
 
Nenda Dodoma maeneo ya Ntyuka (Hospital ya meno) iliyopo hapo wanatoa mafunzo,mbegu pia wanauza uyoga
 
Habari zenu wapendwa
Kwa niaba ya rafik yangu anataka kuaanza kusambaz uyoga sehmu mbalimbali hqkin hajui wapi anaweza pata uyog nd nikwabei gani kwa kilo...
Tusaidiane tuepukane na umaskini
 
Tembelea hii link mie nimeisoma na ni nzuri itakupa mwangaza wa kutosha, japokuwa nami,bado niko na,swali kwa mwanza mbegu za uyoga naweza zinunua wapi???

mossesanney.blogspot.com/2013/05/fahamu-faida-za-uyoga-mwilini-na-jinsi.html?m=1 Enyoy your reading, education and learning
 
Hornet, Majibu kuhusu suala lako linalohusu kilimo cha Uyoga, Mimi ni Mjasiliamali na Mtaalamu wa kilimo cha Uyoga na Uyoga wenyewe,kwangu mimi kilimo cha Uyoga ndio kazi yangu na ndio Maisha yangu.
1.nianze na suala la upandaji wake, ok kilimo cha Uyoga ni kilimo tofauti na vilimo vyingine, ni kilimo kinacholimwa ndani, ni kilimo chenye tecknolojia ya kipekee, kinachotumia mabaki ya shambani, kiwandani pamoja na taka tunazozalisha kila siku.
2.Uyoga huchukua kati ya siku 30-35 toka kupandwa kwake, na huvunwa kila baada ya siku moja kwa muda wa miezi mitatu, inategemea na ubora wa mbegu pamoja na utaalamu wa mboji uliotumika.
3.Kuhusu masoko, bado soko la uyoga halijawa rasmi lakini ni bidhaa yenye soko lisilojulikana, soko kubwa la nje kwa sasa ni kenya ndio kulipo na uhitaji mkubwa wa uyoga.

4.kuhusu mbegu za Uyoga, mbegu za uyoga huzalishwa kitaalamu kwenye maabara maalumu kwa kutumia uyoga halisi (tissue culture), hapa utapata mbegu bora za Uyoga zilizotambuliwa kitaalamu

Kwa maelezo zaidi ya mafunzo ya kilimo cha Uyoga kibiashara tutembelee,(mafunzo ya darasani, mafunzo kwa vitendo, na shamba mfano) Mwanagati Mushroom Growers,0767 307 800.

Karibuni Mjionee na mpate mafunzo kivitendo
 
Wakuu,kifikra nimechoka na ajira nataka kujiajiri na kuajiri pia.Wakuu,Nimepata taarifa juu ya soko la Uyoga huko barani Asia na ulaya kuwa ni kubwa lakini pia linalipa sana!!! Wataalamu na wajuzi hebu tupeni elimu jinsi gani naweza fanya hiki kilimo na gharama zake pia hata aina za uyoga.Ni mimi ndugu yenu nafsi yangu
 
Uko wapi?

Juzi nimeona flyer ya mafunzo mbalimbali mojawapo ilikuwa kilimo cha uyoga. Hao walimu wako 8/8 grounds A-town. Wanasema wao ni wastaafu ambao wameamua kujiajiri.... Kama uko jirani ungeweza kuongea na mtaalamu wao.
 
KWA mujibu wa tafiti mbalimbali kuna aina nyingi za uyoga duniani ambazo zina matumizi tofauti yakiwemo ya chakula na dawa.

Chama cha Wazalishaji Uyoga cha Dar es Salaam, (DMGA) kinasema kwamba uyoga umegawanyika katika makundi makuu matatu; kundi la kwanza likiwa la uyoga-taka (saprophyetes). Kinafafanua kwamba uyoga huu hupata virutubisho vyake kutoka kwenye miti mikavu na masalia ya mazao ya kilimo.

Aina nyingine kwa mujibu wa DMGA ni uyoga tegemezi (parasites) ambao hupata virutubisho vyake kutokana na mimea na wanyama hai na huweza kusababisha uharibifu mkubwa wa mimea na wanyama hao. Uyoga ufaano (symbionts) ni aina nyingine ambayo DMGA wanasema hupata virutubisho vyake kutokana na mimea na wanyama wanaoishi karibu nao bila kuleta madhara.

Huu pia ni uyoga unaoishi kwa kutegemeana. DMGA wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Judith Muro wanasema uyoga ni mmea mkavu ambao hauwezi kujitengenezea chakula, lakini hutoa vimeng'enyo vinavyosaidia kuyeyusha mabaki ya mimea au wanyama ili kujipatia chakula.

Uyoga huweza kuota wenyewe porini au kuoteshwa kitaalamu na matumizi ya uyoga kwa binadamu ni pamoja na lishe na tiba. Uyoga una vitamini lishe B, C na D, madini ya fosfarasi, chumvi, potasiam na chokaa na pia una protini kwa wingi kiasi cha wastani wa asilimia 10 hadi 49.

Mbali na wingi wa vitamini lishe, pia uyoga ni tiba inayosaidia kuimarika kwa kinga za mwili na kudhibiti magonjwa kutokana na kuwa na viinilishe vingi.

"Zipo aina mbalimbali za dawa kwa mtindo wa vidoge, maji na sindano zinazotengenezwa kutokana na uyoga," anasema Muro. "Dawa hizo zinaweza kutibu au kuzuia magonjwa ya kifua kikuu, kusukari, moyo, shinikizo la damu, figo, saratani mbalimbali, vidonda vya tumbo na lehemu," anasema.

Kutokana na umuhimu wa uyoga kuwa lishe na tiba kwa binadamu Juni 28, mwaka huu Chama cha Wazalishaji Uyoga cha Dar es Salaam kilifanya maonesho ya uyoga kwa vikundi vya wakulima wa zao hilo katika Shule ya Sekondari Mongola, iliyopo Kata ya Mzumbe, wilayani Mvomero, Morogoro.

Vikundi vya wakulima wa uyoga kutoka Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro na Kijiji cha Vigenge, Kata ya Mzumbe, vilishiriki kwa kuonesha bidhaa zitokanazo na uyoga na mapishi. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa DMGA, Judith Muro, vikundi vya akinamama vimekuwa na hamasa kubwa zaidi hasa baada ya kutambua kuwa uyoga unaweza kuwa chanzo cha mapato kwa familia na hivyo kuwa njia mojawapo ya kupunguza umasikini.

"Uyoga ni rafiki wa mazingira kwa kuwa unatumia makapi ya viwandani na mashambani ambayo yangeweza kuwa kero kwa jamii. "Baada ya kuvuna uyoga mabaki yake hutumika kurutubisha ardhi na kuua minyoo ya ardhini inayoshambulia mazao kama nyanya na migomba," anaelezea Muro.

Anasema uyoga unaweza kuwa ajira kwa vijana pia wazee na unafaa pia kuwa kilimo cha wenye kipato kidogo mijini kwa kuwa hauhitaji eneo kubwa la kuzalishia. Anasema kwa kutambua umuhimu wa uyoga, Mwenyekiti huyo anaiomba Serikali hasa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika iliingize zao la uyoga kwenye mfumo wa kuendeleza mazao muhimu na lipatiwe rasilimali watu na fedha katika kuliendeleza.

"Bado uzalishaji wa mbegu bora za uyoga nchini hautoshelezi na uzalishaji wake haujaingizwa kwenye mfumo wa kudhibiti mbegu ili wakulima wapate mbegu bora. Ombi letu kwa serikali ni zao hili kuingizwa kwenye mfumo wa kuendeleza mazao nchini," anabainisha. Kwa upande wake, mkulima wa uyoga wa Kijiji cha Vigenge, Kata ya Mzumbe, Janeth Mbwambo, anasema tangu ameanza kushiriki kilimo cha uyoga, kimempatia mafanikio makubwa ya kiuchumi.

Mbwambo ambaye ni Ofisa Ugani katika Kijiji hicho anasema ameotesha uyoga katika banda lenye urefu wa mita nne kwa mita tano. "Uyoga unaniingizia fedha kuanzia Sh milioni nne hadi nane kwa kipindi cha miezi mitatu ya uzalishaji. Fedha hizi zinanisaidia kuboresha maisha na familia yangu," anasema Ofisa Ugani huyo.

Naye mkulima mwingine wa uyoga, Maria Shindika, anasema licha ya kuwepo kwa soko la zao hilo, bado wakulima wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mbegu, hali inayowafanya waoteshe kwenye maeneo madogo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Anthony Mtaka, ambaye alikuwa mgeni rasmi siku ya maonesho ya uyoga, anakitaka chama hicho kuweka mfumo utakaowaunganisha wakulima wa zao hilo wa mikoa yote nchini ili kuongeza uzalishaji utakaotosheleza soko la ndani na nje.

Mkuu wa Wilaya anasema, hatua hiyo itakuwa ni kuendeleza juhudi zilizokuwa zimeanzishwa na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Anasema Mzee Kawawa, baada ya kustaafu alikijita katika kilimo cha uyoga hapa nchini na kuwa mhamasishaji mkuu wa zao hilo.

Hata hivyo anasema huko nyuma uyoga ulikuwa unaliwa na wale waliokuwa na utamaduni wa kuufahamu hususan ule wa msituni na wale waliokuwa wakitembelea hoteli kubwa hususan wapenzi wa supu ya uyoga.

"Kupitia siku hii ya maonesho ya uyoga, jamii inaweza kupata fursa ya kujifunza na kufahamu faida na matumizi ya uyoga katika mwili wa binadamu," anasema Mkuu huyo wa Wilaya ya Mvomero. Anaongeza: "Historia ya kilimo cha uyoga inaonesha kuwa ina zaidi kidogo ya miaka 10 hivyo hapa ninaona kuna baadhi yetu tunahitaji kuweka nguvu zaidi katika kuendeleza zao hili.

Anasema kwamba tangu Mzee Kawawa afariki dunia kasi ya kuhamasisha kilimo cha uyoga nchini imeshuka na kwamba kutokana na umuhimu wake jamii inapaswa kufufua juhudi zilizoanzishwa na Mzee Kawawa. "Mzee Kawawa alikuwa ni kiungo muhimu katika uendelezaji wa zao la uyoga. Chama hiki kwa sasa kifanye kazi aliyoanzisha huyu mzee wetu kabla ya kifo chake kama njia ya kumuenzi pia," anasisitiza Mtaka.

Mtaka pia anakishauri chama hicho kuelekeza nguvu zake katika kufundisha zaidi juu ya ujasiriamali wakulima wote na si wa uyoga pekee pamoja na kusimamia uzalishaji bora wa zao hilo. Anasema chama hicho kinapaswa kuwa na mtandao ikiwa ni pamoja na kuchukua jukumu la kuwatafutia wakulima masoko ya uhakika, hususan katika hoteli kubwa na maduka makubwa maarufu kama supermarkets.

Chanzo: Habari Leo

 
Wadau na wajasiriamali popote, naomba yeyote mwenye kufahamu wapi naweza kupata mbegu za uyoga aina yoyote tujulishane.... Km mjasiriamali kwani ni mtaji tosha kwa maish haya ya mtanzania
 
Jamani, Nimejipanga Kuzalisha Kilo 20 Za Uyoga Aina Ya Oyster (mamama)Kila Siku, Sasa Naomba Kwa Yeyote Ambaye Atakuwa Tayari Nikawa Nafanya Naye Biashara Hii ( Yaani Mteja Wa Jumla) Naomba Tuwasiliane
 
Back
Top Bottom