Kilimo na Usimamizi

Jesusfreak08

JF-Expert Member
Jul 20, 2019
823
1,797
Mtazamo kuhusu kilimo imepelekea watu kufanya kilimo kama kazi ya ziada au shughuli ya zaida katika kupata faida ili kuendesha maisha au naweza kusema hawachukilii serious ulimaji wao,

Ni kweli sawa umebanwa na kazi au shughuli za hapa na pale lakini kamwe usije kufanya kilimo cha simu kwasababu watu wengi sana sio waaminifu kwenye pesa lakini ukiachana na hilo ni ngumu sana mtu kuchukulia uzito kama ambavyo wewe ungechukulia.

Mfano kwenye umwagiliaji ,uwekaji mbolea, upuliziaji dawa unakuta mambo haya yanafanyika lakini sio kwa ufanisi ambao unatakiwa kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri inapelekea upotevu wa muda ,pesa na nguvu na baadae kupelekea mavuno machache.

Jambo la kufanya hakikisha unapata msimamizi mwaminifu ,makini ,muadilifu na mchapakazi hata kwa kumlipa ni heri ulipe gharama ndogo kuliko kutokulipa na kupata hasara kubwa baadae epuka sana ndugu jamaa katika usimamizi au kama unaweza hakikisha unapitia walau mara tatu kwa wiki moja ili ujihakikishie na usiishie kupiga simu tu.

Usimamizi ni muhimu katika uzalishaji wa mazao.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom