njowepo, ni mafinga vijiji gani hivyo mkuu. na ni miti gani ya kuvuna ndani ya miaka 3 (inanitia wasiwasi) au unavuna milingoti?[/QUOTE]
Hapo pekundu,ungeuliza kama jamaa anavuna boriti/poles/fito za mlingoti. Hata mimi nina shaka juu ya umri huo, ila kwa fito za kujengea sehemu za starehe kama baa inawezekana kuvuna baada ya miaka 4, mara nyingi nimekutana na malori yakiwa yamepakia fito toka Iringa kuja Dar kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya starehe.
Ukienda Uchindile au Kilosa ya Mufindi unaweza kupata ardhi ya bure, ila ni namna gani uende huko, ni mziki mzito huo. Au ukienda Kimara Kilolo, kuna ardhi hadi basi,ila uendaji huko ni hatari. Ukienda Magome Kilolo, kuna misitu ya bure ya kununua ila kuna mteremko mmoja hivi ni hatari, ukiumaliza inabidi upumzike kidogo gari lipoe.
Ila msiogope, huo ndio utafutaji wa halali na haki kabisa.