Kilimo kwanza sio sawa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Serikali ya Tanzani ya JK ilipoamua kilimo kuwa kipaumbele chake haikuwa sahihi. Mwana-zuoni Abraham Maslow aliyaweka mahitaji ya viumbe hai katika makundi matano. Kundi la kwanza na la chini ni mahitaji ya msingi/lazima kabisa (physiological needs) kwa viumbe hai vyote tukiwemo wanadamu. Alisema (Maslow) kuwa bila kupata mahitaji haya ya msingi binadamu hawezi kutamani wala kutafuta wala kufanikisha mahitaji mapya (secondary needs). Kwenye kundi hili la mahitaji muhimu pia wanasayansi walimuunga mkono kwa kufanya tafiti mbalimbali kuhusu mahitaji ya mwili. Wanasayasi waligundua kuwa kwa kwa umuhimu wake binadamu anahitaji hewa (oxygen) kama hitaji la kwanza la mwili. Kama ubongo ukikosa oxygen kwa dk 4 tu binadamu ataudhulika vibaya sana (brain death). Maji ndio yanayofuata kwa umuhimu baada ya hewa, yakifuatiwa na chakula (kilimo kwanza), love na safety (free from pain, shelter, clothing, etc).

Kwakuwa hewa tunaipata bure basi tungehamishia nguvu zetu kwanza kwenye hitaji la pili ambalo ni maji. Serikali ingetangazi sera ya "maji kwanza" kabla ya kilimo kwanza. Watanzania hawana maji hawawezi kufikiria maendeleo yao. wanatumia muda mwingi kuwaza na kupata maji ya kunjwa, kupikia, kuoga, kufua, kuosha, na kunywesha mifugo yao.

Tanzani tunayo mito na maziwa makubwa. Sera zetu zingelenga kuhakikisha tunazuia mito kutiririsha maji baharini kabla kila mwananchi hajapata maji. Tukaushe maziwa yote nchini ili kila mwananchi apate maji. Mbona huku Marekani wenzetu wanatumia maji kumwagilia majani ya mji mzima? hakuna vumbi kwanini sisi tunashindwa kuwapa watu wetu maji ya kunjwa tu? hata hicho kilimo kwanza hakitawezekana kama hatuta maji.

Wazo langu, JK aache kuwekeza zaidi kwenye kilimo na barabara ambazo baada ya miaka 5 tu zitakuwa na mashimo kila mahali na kelele ndipo zitakaposikika zaidi nchi nzima watu wakilalamikia mahandaki barabarani. watasema bora ya barabara za mavumbi kuliko mahandaki haya. Wazungu wanasema "no pain no gain" tuwaandae wananchi kisaikologia kukabili ubovu wa barabara kwa sasa ili tuwape maji kwanza, kisha chakula, barabara, kisha, matibabu, nyumba, nguo, love, esteem na mwisho self actualization (Maslow's)
 
Ndugu yangu naomba msamaha nimetafuta kitufe cha like kimekosa ila nikiingia kwenye computer ntakupatia. Ubarikiwe sana ila haya mawazo yangeingia magazetini ingefikisha ujumbe.
 
serikali ya tanzani ya jk ilipoamua kilimo kuwa kipaumbele chake haikuwa sahihi. Mwana-zuoni abraham maslow aliyaweka mahitaji ya viumbe hai katika makundi matano. Kundi la kwanza na la chini ni mahitaji ya msingi/lazima kabisa (physiological needs) kwa viumbe hai vyote tukiwemo wanadamu. Alisema (maslow) kuwa bila kupata mahitaji haya ya msingi binadamu hawezi kutamani wala kutafuta wala kufanikisha mahitaji mapya (secondary needs). Kwenye kundi hili la mahitaji muhimu pia wanasayansi walimuunga mkono kwa kufanya tafiti mbalimbali kuhusu mahitaji ya mwili. Wanasayasi waligundua kuwa kwa kwa umuhimu wake binadamu anahitaji hewa (oxygen) kama hitaji la kwanza la mwili. Kama ubongo ukikosa oxygen kwa dk 4 tu binadamu ataudhulika vibaya sana (brain death). Maji ndio yanayofuata kwa umuhimu baada ya hewa, yakifuatiwa na chakula (kilimo kwanza), love na safety (free from pain, shelter, clothing, etc).

Kwakuwa hewa tunaipata bure basi tungehamishia nguvu zetu kwanza kwenye hitaji la pili ambalo ni maji. Serikali ingetangazi sera ya "maji kwanza" kabla ya kilimo kwanza. Watanzania hawana maji hawawezi kufikiria maendeleo yao. Wanatumia muda mwingi kuwaza na kupata maji ya kunjwa, kupikia, kuoga, kufua, kuosha, na kunywesha mifugo yao.

Tanzani tunayo mito na maziwa makubwa. Sera zetu zingelenga kuhakikisha tunazuia mito kutiririsha maji baharini kabla kila mwananchi hajapata maji. Tukaushe maziwa yote nchini ili kila mwananchi apate maji. Mbona huku marekani wenzetu wanatumia maji kumwagilia majani ya mji mzima? Hakuna vumbi kwanini sisi tunashindwa kuwapa watu wetu maji ya kunjwa tu? Hata hicho kilimo kwanza hakitawezekana kama hatuta maji.

Wazo langu, jk aache kuwekeza zaidi kwenye kilimo na barabara ambazo baada ya miaka 5 tu zitakuwa na mashimo kila mahali na kelele ndipo zitakaposikika zaidi nchi nzima watu wakilalamikia mahandaki barabarani. Watasema bora ya barabara za mavumbi kuliko mahandaki haya. Wazungu wanasema "no pain no gain" tuwaandae wananchi kisaikologia kukabili ubovu wa barabara kwa sasa ili tuwape maji kwanza, kisha chakula, barabara, kisha, matibabu, nyumba, nguo, love, esteem na mwisho self actualization (maslow's)

thumb up!!!
 
lakini je watanzania tunafahamu walau tunahitaji nini ktk maisha haya au tunaishi kwa bahati?
 
Back
Top Bottom