KILIMO KWANZA, sera au kauli mbiu?

Mwanahisa

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
1,382
510
....... Tanzania is forecast to grow at a rate slightly 6.9%pa over 2012-2017. Agriculture is an important contributor to GDP, according for 26% and goverment is very supportive of this sector development. A number of initiative are underway to inhance its perfomance. Hawakutaja chochote kuhusu kilimo kwanza, hawa ni IMF report, source; Website www.imf.com

Kutoka chanzo hiki, Watengenezaji maarufu wa pembejeo za kilimo toka Marekani John Deer, kutokana na msukumo wa soko kwa uhitaji mkubwa wa zana za kilimo waliamua kuweka viwanda vyao katika nchi za India, China, na Mexico ambako trekta moja linazalishwa kwa gharama ya dola $12,000.

Mozambique, wakulima wa kiwango cha chini huwezeshwa kununua trekta kwa kuwekeza kiasi cha $5000 (deposit) tu katika BAnk ya Standard, na mkopo huo husimamiwa na USAID.
Ninachojiuliza haya maigizo ya Bank ya wakulima, sijui Matreka ya SUMA-JKT ya mil 25. Tunamfanyia nani? Mbona wenzetu wanaangalia kilimo kwa mtizamo wa kipekee sana, sisi serekali yetu hata aibu hakuna? Inanipa mashaka makubwa kuamini kama viongozi na serikali wanamaanisha wanachokisema juu ya Kilimo Kwanza.
 
hapo kwenye underline..naskia trekta moja liliwahi kugongana na starlet..liliumia vibaya mpaka injini kudondoka...te he hee!!

mkuu, kwa ufahamu wangu hii nchi huwa inakuwa na kauli mbiu, sidhani kama katika miaka 50 kama taifa huru tumewahi kuwa na sera yoyote ya maana na endelevu....

sisi ni kauli mbiu tu: tanzania bila umaskini yawezekana, tanzania bila ukimwi yawezekana, tanzania bila malaria yawezekana...hizo ni za karibuni kabisa.

za zamani ni pamoja na: siasa ni kilimo, kilimo cha kufa na kupona, mvua za kwanza ni za kupandia.....
 
Mkuu Al Zagawi, usinikumbushe juu ya hizo trekta hapo jeshini, huko ni sawa na kufanyia biashara uhai wa Mtanzania.
Sera ni kitu ambacho kingetakiwa kiimbwe sawa na wimbo wa taifa, Umewahi sikia matokeo ya Mapinduzi ya kijani Uchina? mbona hatuna chakujifunza?
 
For God's sake Tanzania hatujawa tayari katika kilimo kwanza.!Pye pyepye tuna nyingi mno, sera ya kilimo kwanza haizingatii kumwendeleza mwananchi wa kawaida bali mwenye uwezo, pia suala la kuhamasisha vijana washiriki kwenye kilimo kwanza ndo basi tena yaani serikali haina mpangop nao hata kuweka mikakati ya kuwawezesha ili washiriki kisasa zaidi kwenye kilimom kwanza . Hatutaenda popote kwa kutumia jembe la mkono na kutegemea kilimo cha mvua.Muulize Mh. Waziri mwenye dhamana, Ni Kiasi gani cha ardhi ifaayo kwa kilimo kwanza iko mijini na kwanini wazee wengi hawatoki vijijini kukimbilia mijini na badala yake vijana ndo wanatoka vijijini wanakimbilia mijini.Eti! tutakaribisha wawekezaji ,sawa, lakini kwa nchi hii ,viongozi hawa, na maamuzi haya, tutegemee kuongeza migogoro ya ardhi ama baina ya wananchi na wawekezaji au wananchi kwa wananchi.
 
kilimo ni uti wa mgongo wa taifa, kilimo cha kufa na kupona, siasa ni kilimo, kilimo kwanza, n.k. tunarudi nyuma hatusongi mbele
 
kilimo ni uti wa mgongo wa taifa, kilimo cha kufa na kupona, siasa ni kilimo, kilimo kwanza, n.k. Tunarudi nyuma hatusongi mbele

mbona mnajadili mambo yaliyoko mahakamani??werema atakuja sasa hivi
 
Back
Top Bottom