Kilimo Kwanza: Kauli mbiu inayoonekana kushindwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo Kwanza: Kauli mbiu inayoonekana kushindwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ulimakafu, Jan 13, 2012.

 1. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Mwaka 2009 kuna hiki kitu kinaitwa Kilimo Kwanza kiliibuliwa baada ya kubuniwa na kuhubiriwa sana na wanasiasa kuwa kitakuwa mkombozi wa watanzania kwenye chakula na kipato,lakini mpaka sasa naona kama imeshindwa,kama ile ya kujivua gamba.Baada ya takribani miaka miwili ushee hali ya chakula ni mbaya na kilichopo bei yake haikamatiki.Jamani Tz inachosha sana.
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Nchi yetu ni ya kaulimbiu tu.Utekelezaji..........
   
 3. w

  wikolo JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tatizo la viongozi wetu ni kuweka siasa zaidi hata katika mambo yanayohitaji utendaji. Najaribu kufikiria kauli mbiu za siku za hivi karibuni lakini nashindwa kupata hasa ile iliyofanikiwa ni ipi. Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya; Maisha Bora kwa Kila Mtanzania; Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele nk. Hizi zote na nyinginezo, sijaona ambayo imetekelezeka. Sitaki hata kusikia hilo la maisha bora kwa kila mtanzania manake linatia hata hasira ukiangalia hali za watanzania zilivyo kwa sasa.

  Hiyo ya miaka hamsini ya uhuru ndo ilikuwa kiboko. Sijui wenzetu wanaokaa na kutunga kauli mbiu kama hizo wanakuwa na lengo la kumfurahisha nani hasa. Kwangu mimi kauli mbiu hiyo inaonyesha ni jinsi gani ambavyo tumeshindwa kujitambua kama taifa. Hatujui matatizo yetu ya msingi ni yapi na ni wapi hasa tunakotaka kuelekea kama taifa. Tumethubutu katika lipi? Tumeweza lipi? na tunasonga mbele kuelekea wapi?

  Wewe subiri tu ndugu yangu utaona jinsi hiyo ya kilimo kwanza itakavyobadilishwa baada ya matokeo yake kutoonekana, nadhani unakumbuka jinsi tulivyobadilisha ile ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya! Haya yote yanapatikana Tanzania tu!
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Yaani inakaera mpaka basi.Good analysis.
   
Loading...