Kilimo kikubwa, utumwa mpya (1)? Eti utumwa!!

Ngurudoto

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
208
26
KILIMO KIKUBWA, UTUMWA MPYA (1)... YAMEKUWA HAYA! UTUMWA???
Na Joseph Mihangwa
0713-526 972
jmihangwa@yahoo.com
Mwanahalisi Issue # 130, April 1-7


KATIKA hali isiyotarajiwa, na pengine bila utafiti na uchambuzi makini, Tanzania sasa imetangaza kuingia katika kile kinachoitwa "Mapinduzi ya Kijani" ya nchi zilizoendelea.
Mapinduzi ya Kijani maana yake ni Kilimo cha Mashamba makubwa na endelevu, chenye kutumia zana za kisasa kama vile matrekta, mashine za kuvuna (combined harvester) na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo.
Kile ambacho kinapendekezwa na wataalamu wa kilimo ni kwamba, mkulima wa Tanzania mwenye kutumia jembe la mkono na plau hatakiwi; anapaswa kutupwa mara moja kwenye jumba la makumbusho asionekane tena, na "Mapinduzi ya Kilimo" yatawale na kuongeza uzalishaji.
Ndio kusema kwamba, programu za kumwendeleza mkulima mmoja mmoja, ili naye aweze kuwa mkulima endelevu, zilizoasisiwa enzi za uhuru, sasa basi!
Lakini swali muhimu ni hili: Ni wapi duniani mapinduzi ya kilimo yameleta neema (badala ya shari) ili yaweze kuigwa?
Siku zote Mapinduzi ya kijani yameambatana na matumizi ya mbegu zilizorekebishwa-genetically modified seeds" (GM), maarufu kama "Miracle Seeds", mbegu zenye maajabu kwa uzalishaji zaidi.
Mbegu hizi zilibuniwa na wanamikakati wa Marekani kama sehemu ya mikakati wa kudhibiti kuenea kwa ukomunist, kwa kufungua soko kamili la teknolojia ya kilimo kwa nchi masikini.
Mmoja wa wanamkakati hao, John King, aliwahi kuandika, "Mapambano kati ya Mashariki (ukomunisti) na Magharibi (Ubepari) barani Asia, kwa sehemu kubwa, ni mashindano katika uzalishaji, na mpunga ni ishara ya mashindano hayo."
Kuanzia miaka ya 1960, juhudi za nguvu ziliendelezwa kueneza mapinduzi ya kijani na "Kurekebisha Kilimo" kwa ujumla kwa nchi masikini bila kujali matokeo yake.
Hii haikuwa ajabu kwamba, baada ya kuratibu uzalishaji katika kilimo kwa njia ya zana kubwa na mashamba makubwa huko Marekani Kaskazini, katika miaka ya 1960, makampuni ya kimataifa (Agri-business Multinationals), yakaanza kutafuta masoko mahali pengine.
Kwa mfano, kati ya mwaka 1968 na 1975, Kampuni ya Zana ya Kilimo International Harvester, iliongeza mauzo nje ya Amerika Kaskazini, kutoka chini ya asilimia 20 hadi asilimia 33 ya mauzo yote; John Deer kutoka asilimia 16 hadi 23 na Massey-Ferguson kutoka asilimia 40 hadi 70.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ndilo limepewa kazi ya kuratibu ukuaji wa shughuli za makampuni haya. Baadhi ya makundi yake kikazi ni pamoja na majina makongwe kama Caterpillar, Tractors, John Deer, Fiat, FMC, Massey Ferguson na Mitsui.
Kwa kuwa Kilimo kikubwa cha zana kubwa hutumia mafuta, vivyo hivyo makampuni makubwa ya mafuta yanaingia humo. Haya ni pamoja na British Petroleum (BP) na Shell.
Ushirikiano kati ya FAO na makampuni ya kuhodhi unakwenda hadi kwenye (dawa) viua wadudu. Kundi la viua wadudu huhamasisha matumizi ya dawa hata pale palipo na njia mbadala ya dawa.
Mbegu za Miujiza (GM), au kwa njia la kuzifagilia "High Responsive Variety (HRV), hazikubali kupandwa hivihivi na mkulima akavuna mazao mengi. Ingekuwa hivyo, makampuni haya yasingehusishwa.
Ili mbegu za HRV zitoe mazao mengi, zinahitaji umwagiliaji maji wa viwango vikubwa na maalum, matumizi ya mbolea, viua wadudu na viua magugu.
Ili uzalishaji uwe wa faida, sharti kiwe kilimo kikubwa kwa maana ya ukubwa wa mashamba na teknolojia-matrekta, haro, mashine za palizi, upukuaji na zana za kuna mashamba makubwa.
Kwa ufupi, mapinduzi ya kijani yanataka matumizi ya teknolojia na pembejeo za Kilimo, ambapo vyote, ambapo vyote hivyo vinahitaji mafuta, na kwa sababu hii mkulima mdogo hawezi kutarajia hata siku moja kuwa "mwana-Mapinduzi ya Kijani."
Badala yake atakuwa manamba katika mashamba makubwa ya wenye uwezo. Huu ni utumwa mpya chini ya sera za Benki ya Dunia na nchi zenye viwanda. Mahali popote mapinduzi ya kijani yalipojaribiwa, yamesababisha bei ya chakula kupanda.
Kupanda kwa bei ya mafuta kutaongeza bei ya nafaka. Kwa sababu pembejeo lazima ziagiwe kutoka nje, sekta ya kilimo ndiyo pekee inayolipia, na maana hiyo kilimo cha mazao kama kahawa, pamba, chai, mkonge, korosho au tumbaku, lazima kipanuliwe kukidhi haja hiyo.
Ili kutimiza hili, sehemu ya ardhi ya kilimo cha chakula lazima itumike, na hivyo mkulima kulazimika kugawa muda wake kati ya kilimo cha mazao ya biashara ambayo serikali inayataka (na kwa yeye kupata fedha kulipia kodi), na kilimo cha chakula kwa ajili ya familia yake.
Kodi kubwa (na michango mbalimbali) na kuanguka kwa bei ya mazao ya biashara. Lakini kwa kuwa ardhi ya kilimo kikubwa italimwa kwa mfululizo bila kupumzishwa, itapoteza rutuba haraka.
Na ili kuiokoa ardhi, mkulima ataanza katumia mbolea za viwanda. Na kadri bei ya mbolea itakavyozidi kupaa, ataacha kuitumia. Hapo ataanza kugundua kwamba ardhi yake haiwezi kuota mimea tena na jangwa litaanza kunyemelea.
Mbali na madhara ya ki-ekolojia katika kufuata sera za kilimo za FAO na Benki ya Dunia, kuna hili ambalo wengi hatulioni: Kwa karne nyingi za majaribio, wakulima wadogo wameweza kuzalisha mbegu madhubuti za asilia, zenye kuvumilia matatizo ya ki-ekolojia.
Mbegu hizi zitatoweka haraka pale mapinduzi ya kijani yanaposhinikizwa. Lakini FAO na Benki ya Dunia wanajua jinsi zinavyoibwa na kuhifadhiwa huko Ulaya.
Haitashangaza kuona siku moja tukiuziwa mbegu hizohizo zikiwa zimebadilishwa kidogo tu na kufungwa kwenye pakti, zikiuzwa kwa fedha za kigeni.
Kwa kukimbilia mapinduzi ya kijani, serikali inajivua wajibu wajibu wa kumwendeleza mkulima mdogo na kufungua milango kwa maselta; hivyo kumfanya abaki kibarua kwenye ardhi ambayo anaihesabu kuwa ni urithi kutoka kwa mababu zake. Huo ni utumwa mpya.
 
JF: Hii makala or Tuite Waraka wa Wiki katika M/Halisi imenipush to seek mawazo mbadala sababu it stroke me na hisia hasi hasi sana (cynical) kama sio kupindukia..sikuona Tija.

A good reader ukisoma opening/closing agrument za andishi lolote unaweza pengine kutabari body ikoje, kwenye hii article, hayo yalishindikana: nikabidi nisome body yote kutafuta na kuelewa Utumwa Mpya umekuja vipi ktk Kilimo chetu kinachokua kwa 4% na jitihada za kuendelezwa zimetangazwa na kuonekana mwaka huu.

..Natubu Likanichukua muda zaidi ya matarajio yangu jamani... so here.

Opening statement, I quote, "KATIKA hali isiyotarajiwa, na pengine bila utafiti na uchambuzi makini, Tanzania sasa imetangaza kuingia katika kile kinachoitwa "Mapinduzi ya Kijani" ya nchi zilizoendelea."

Closing statement, I again quote, "Kwa kukimbilia mapinduzi ya kijani, serikali inajivua wajibu wa kumwendeleza mkulima mdogo na kufungua milango kwa maselta; hivyo kumfanya abaki kibarua kwenye ardhi ambayo anaihesabu kuwa ni urithi kutoka kwa mababu zake. Huo ni utumwa mpya."

Hybrid Open/Close iko hivi:KATIKA hali isiyotarajiwa, na pengine bila utafiti na uchambuzi makini, Tanzania sasa imetangaza kuingia katika kile kinachoitwa "Mapinduzi ya Kijani" ya nchi zilizoendelea.Kwa kukimbilia mapinduzi ya kijani, serikali inajivua wajibu wa kumwendeleza mkulima mdogo na kufungua milango kwa maselta; hivyo kumfanya abaki kibarua kwenye ardhi ambayo anaihesabu kuwa ni urithi kutoka kwa mababu zake. Huo ni utumwa mpya."

Mhariri kaanza utangulizi kama mtafiti aliyebobea (mbwembwe kidogo/kiingereza kidogo) and he grab my attention lakini Kachanganya mambo pamoja kiingereza mara (GM) or Miracle Seeds akiziita ni mbegu zenye maajabu..neno ki-ekolojia, mara bei za mafuta, mbolea, brand za matrekta ambayo kwa maoni yangu hazihusiani--With or without jitihada zozote (Green or Non-Green Revolution), factors za mbolea, mafuta, teknolojia zipo na kubadilika sio kosa la mkulima na sio sababu ya kuogopa maendeleo.

Miracle Seeds :maneno Miracle and Magical are distinctive (KUNA TOFAUTI WA MAANA)..Magical ndio huleta maajabu, sio miracle, mfano: Mgonjwa mwenye saratani akipona ndio people refer as a miracle ya baraka au kubarikiwa hivi, na sio magical maajabu au miujiza. Anyway Thats minor lakini yeye alielezea mbegu zenye miujiza fulani kuongeza mazao ..Sayansi sio miujiza wala ushirikina hapo..kachangaya kwa kuleta siasa za vita baridi Asia za akina John King...Utumwa mpya wapi???sikuona kabisa.
..
Lingine ktk andishi I noted ni kurudia rudia (repetition) matumizi ya maneno ukubwa, kubwa au makubwa ni zaidi 16 times, hapo nilikuwa najaribu kupata linkage ya Mhariri to the New Slavery na Green Revolution kuleta Utumwa.Yes, Tanzania ni kubwa.

Furthermore, Its also appeared mhariri wa Makala hii never really supported argument zake na facts independent, kutufanya tuamini or to conclude maendeleo ya Kilimo or huu uoga wake mkubwa (yeye) wa "Mapinduzi ya Kijani" yataleta utumwa na Maselta..sikumpata kabisa..

Hisia Hasi (Kupotosha): kusema Green Revolution italeta SHARI...Quote: Lakini swali muhimu ni hili: Ni wapi duniani mapinduzi ya kilimo yameleta neema (badala ya shari) ili yaweze kuigwa?

GREEN REVOLUTION YA INDIA OR MEXICO zilizotokea miaka ya 1950 0r 1960's hazikumwaga damu wala kuwa na shari like the RED REVOLUTION YA Kisiasa iliyotokea Urusi..Tusiwachanganye wakulima wetu, hata hao..eeh.

Green Revolution ni efforts za kujitosheleza kwa Chakula na kuuza akiba kupata kipato aidha ndani au nje ya nchi.. sasa utumwa unakuja wapi???..

Like India kuna mtu anaitwa Paul R. Ehrlich, author wa kitabu, "The Population Bomb" alitabiri njaa kubwa na kuwa India isingeweza kujitosheleza ki-chakula na kuwa ongezeko lao la watu wangekufa kwa njaa pamoja na mikakati ya Green Revolution (Green ya mimea sio vinginevyo)..hii ilikuwa mwaka 1968 kufikia mwaka 1974, India, mpaka hivi leo ni self-suffient kichakula

..sijui kama watatokea akina Paul R. Ehrlich (Tanzania), hizi haziwezi kuwa juhudi mbaya...Ardhi naamini ipo kubwa kufanya maendeleo.

Tanzania ni nchi yenye ardhi nzuri, kubwa, yenye rutuba na sisi wa-Tanzania by population are the 6th in Africa and kwa ukubwa Ardhi ni Nchi ya thelathini na moja duniani (31st in the World in terms of Area), km zetu za mraba karibu milioni moja, ni 954 Thousand na ushee (sq km) to be exact; kujitosheleza kimsosi ni swala nyeti na lakupongezwa hatuna budi kuchukua hatua kuna wilaya zaidi ya ishirini bado zinabebwa kwa chakula..hizi juhudi ni Njema.


Nchi zenye ukubwa wa namna hii, ardhi na rasilimali watu (40Million) ni sahihi kuendeleza food supply, element ya utumwa sikuelewa kweli zimekuja kivipi hapa, ardhi ipo, Teknologia ikiletwa ni swala zuri na wadogo wajifunze, wajiunge--tuache jembe la mkono

Wanasema: Mwenye njaa hana akili..

..Au Shamba kubwa litameza shamba dogo, ardhi isiyotumika ipo kubwa, Mapinduzi ya namna hii yanaweza kuendeleza hata miundombinu kwenda katika maeneo ambayo hayafikiki (interior areas)

Tusichanganye mambo, Mapinduzi haya sio mauwaji au Utumwa--najua wakulima hawajasoma, sasa tunaweza kubeza maendeleo lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni..

Nalazimika to conclude kama Mhariri wetu alivyoanza: "KATIKA hali isiyotarajiwa, na pengine bila utafiti na uchambuzi makini,Inawezekana Mhariri haelewi vizuri kile kinachoitwa "Mapinduzi ya Kijani" ya nchi zilizoendelea.
 
Kuna ukweli kidogo ulochanganyikana na uongo.
Makala nzima siikubali, ni woga ule ule wa kuogopa mabadiliko ya kiteknolojia.
Teknolojia yeyote inaweza kutumika kumwendeleza au kumwangamiza mwanadamu.
Hatuwezi kuegemea upande mmoja kiasi hicho.
Kuna mazuri mengi kuhusu Genetic Engineered Seeds ambayo hayakutajwa.
 
Kuna ukweli kidogo ulochanganyikana na uongo.
Makala nzima siikubali, ni woga ule ule wa kuogopa mabadiliko ya kiteknolojia.
Teknolojia yeyote inaweza kutumika kumwendeleza au kumwangamiza mwanadamu.Hatuwezi kuegemea upande mmoja kiasi hicho.
Kuna mazuri mengi kuhusu Genetic Engineered Seeds ambayo hayakutajwa.

Nakubaliana na wewe kwenye hiyo sentence marked. Lakini pia pamoja na kuwa mwandishi anaonyesha kwamba pengine kuna mambo yanahitaji evidence zaidi kuliko hisia bado mimi naona kaleta hoja ya maana sana kujadiliwa kwani kama alivyo hata mimi na hisia kama zake. Ukiangalia kwa mfano kilimo cha biofuel hakuna specific policy on it na bado watu wanapewa lease ya muda mrefu bila kujali huyu rural peasant nafasi yake i wapi. Kuhusu mashamba madogo kufa utafiti recent findings europe (Calus M Phd, 2009) inaonyesha si kweli. Mashamba makubwa yapo for centuries but still madogo yameendelea kuwepo hadi leo.

Chakuzingatia ni je hayo mapinduzi ni internerly driven or as usual from our masters wazungu? Na kama ndo wao hao what is the motive behind this. Taarifa = WTO ina wabana hao wakubwa kuondoa subsidy to their farmers na the recent findings zina sema japo kuwa inaonekana kama vile ni WTO lakini kikubwa ni kuwa as EU inapanuka hiyo subsidy ni mzigo kwa jumuia kwani ukiangalia 40% ya budget ya huo umoja inakwenda kwenye agric through direct payment kwa wakulima, politically okay but economically ni kikwazo. Kwa vile wenzetu akili yao iko mbele kila wakati wameazimia kuondoa hiyo na kuachana na mambo ya kilimo na kufanya something called rural development and nature development kwaajili ya environmental issues; na hivyo kuhamishia hiyo subsidy kutoka kwenye blue box kwenda green box. Hizo boxes soma WTO issues utaona maana yake. Sasa sisi tusipofanya analysis nzuri na kuangalia how we would take this as an opportunity ya maendeleo wao kama kawaida kwakuwa na negotiation skills nzuri tutajikuta tumeingia kwenye partnership ya kiutumwa zaidi kuliko development partners. And that is my thinking kwamba ndo alichotaka kukisema mwandishi ila labda hayuko well informed ila ameangalia impact zaidi kuliko the causes za huo utumwa. Swali ni je kama umejenga nyumba na kunashida ya nyumba hilo eneo na watu wengi wanatafuta nyumba utaamua kuuza au kupangisha? Definately utafanya financial analysis if private and economic analysis if communal property e.g country kuona what pays most and how will it be done to realise your objectives. In my opinion my country has not done that and so please let us use this as an opportunity to eradicate our poverty kwani those people need us more than we do as one member once said. tatizo letu kama kawaida wapo individuals wanaojua hilo na wameamua ku invest its good as private entities kwani ni entrepreneurs. BUT for the sake of the majority un informed (Rural peasants) the country is needed to protect them maana ndo kazi yake through appropriate policies kwakuangalia substitutional effects za mechanization and also ardhi yao isije wakaitoa kwa hiari yao kwa hao called investors for 90 years without knowing renting could equally pay them tena in sustainable manor with regards to problems of time preferences of a poor man needing todays food without thinking what would tomorrow look like.
 
nilivyomuelewa mimi utumwa mpya anaona utakuja kwa makulima wetu kuwa wategemezi kwa hao watakao kuja kuendesha kilimo kikubwa. mtu akiweza kulima sana na kupata mazao mengi sana anaweza kuinfluence bei ya bidhaa sokoni. hii inaweza kupelekea wakulima wadogowadogo wetu kuacha kulima au kwa ajili ya biashara na kuanza kulima kwa ajili ya kula. sasa hapo watapata wapi hela ya kununulia say sabuni, sukari, na nguo?

watakuja kuanza kwenda kwenye mashamba hayo makubwa. lakin wataenda na kupokelewa wangapi kufanya kazi mle? leo hii wakulima wetu wanalima kwa ajili ya chakula na pia kwa ajili ya kuuza ili waweze kununua vitu vingine.

wakulima wakubwa wataweza kabisa kuathiri hali inavyoenda kwa sasa kwa kumfanya mkulima asiweze kuuza mazao yake kwani kutakuwa na bidhaa kama alizozalisha zikipatikana kwa bei ya chini zaid na pengine 'bora zaidi'

chukulia mfano wa shinyanga. watu wa kule wanalima kwa ajili ya kula na kuuza. wateja wakubwa wanatoka dar na nk. hao wateja wakikosekana mkulima wa shinyanga atauzia wapi mahindi, mtama na mchele wake?

mapinduz haya ni bora tuyaendeshe sisi wenyewe. wakulima wetu wapewe mafunzo na zana. lasivyo utakuwa utumwa kweli

after all maendeleo tunayotaka sisi ni maendeleo ya watu wetu ambao wapo tayari hapa. tuache uvivu. tunayajua mazingira yetu na watu wetu na kama nia tunayo tukune vichwa jins gani tunaweza kufanya kuboresha maisha ya wakulima wetu kwa kutumia teknolojia
 
Back
Top Bottom