Wilaya gani hii?Kwa Morogoro nenda Dutumi kule wanalima sana mpunga
Na heka moja inatoa wastani wa gunia ngapi?Eneo ni laki 4 kwa huku, mpunga unacheza kwa 90,000 huku mawindi kule rujewa naskia ni 105,000 kwa gunia....eneo mimi nipo kata ya mawindi kijiji cha isunura
Na vipi upatikanaji wa mashambaNenda Kijiji cha Kongwa, Kata ya Mvuha, Tarafa ya Mvuha, Morogoro Vijijini kuna mbuga nzuri sana ya mpunga. Pia kuna scheme ya umwagiliaji. Mwaka jana serikali imeingiza billion 4 kwaajili ya ukarabati wa scheme wakandarasi wapo site wanaendelea na ukarabati. Kilimo ni cha uhakika na gharama za uendeshaji ni nafuu sana ukilinganisha na maeneo mengine. Ekari moja unatumia mifuko 2 tu ya mbolea (mmoja wa kupandia na mwingine wa kukuzia). Eneo la scheme ya umwagiliaji ekari moja wanakodi kati ya laki moja hadi laki na nusu pia kuna gharama ya maji elfu kumi na gharama ya uendeshaji na matunzo ya miundombinu elfu hamsini. Ekari moja unavuna kati ya gunia 25 hadi 30.
Eneo la mbugani wanakodi kati ya elfu sitini hadi elfu themanini kwa ekari. Huko hutumii mbolea kabisa na wastani wa mavuno kwa ekari ni gunia kumi na tano hadi ishirini.
Kiukweli siwezi kukupa exact figures mana mm nilikua nafanya kilimo cha simu kile....sahivi nmekuja rasmi naingia front mwenyewe ambapo mapato ni wastani wa gunia 30 mbaka 35 kwa hesabu za fasta mkuu...na msimu huu wenyeji wanasema hali ni mbaya mvua haikua ya kutoshaa sanaNa heka moja inatoa wastani wa gunia ngapi?
Mashamba yapo, Karibu sana.Na vipi upatikanaji wa mashamba
Dumila MorogoroNa mwenye kujua sehemu mashamba ya nyanya yanapatikana Morogoro atujuze
Mpunga wanaanza kuvuna kwa wingi muda gani?Eneo ni laki 4 kwa huku, mpunga unacheza kwa 90,000 huku mawindi kule rujewa naskia ni 105,000 kwa gunia....eneo mimi nipo kata ya mawindi kijiji cha isunura
wengine washaanza sahivi inategemea tu uliwahi au laaa….wengine kuanzia mwezi huu mwishoni au wa sita kabisaaaaMpunga wanaanza kuvuna kwa wingi muda gani?
Maeneo mengi ya Mkoa wa Morogoro yanalima zao la mpunga. Isipokuwa hizi Wilaya tatu (Kilombero, Mvomero na Kilosa) ndiyo zinalima hili zao kwa kiwango kikubwa. Nje ya hapo kuna Malinyi pia wanalima kwa kiwango cha kuridhisha.Maeneo Gani morogoro naweza kupata mbuga Kwa ajili ya kilimo Cha mpunga na gharama yake please
Naomba Kwa anayefahamu anisaidie
Bei ikoje kwa sasa kwa gunia moja?Njoo wilaya ya mbarali hapa, kata ya mawindi...vijiji vya huku vyote ni kilimo tu...na sasa ndio watu wanavuna mpunga wao....karibu sana(maarufu zaidi kama bonde la usangu)
Habari mkuu je endapo kama nina mashine ya,combine harvester je naweza piga hela huko?Ukimpata mwenyeji wako mzuri anakuelekeza pazuri, kuna mashamba hata iwe hali gani unatapa....mfano hapo nilipopiga picha ni shamba la uhakika sana na wenyeji wanajua hivo linagombewa sana na hapa wanavuna lakini watu washalipia tyari kwa msimu ujao.....kwahyo huku ni nzuri upate mwenyeji akupe ramani za maeneo na mpunga unakubali sana mana hawa wakazi wa huku shughuli yao kubwa ni kilimo cha mpunga ndio mana unaona hata combiner zipo za kutosha tu mana maeneo ya kuvunwa pia yapo