mafimboo
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 2,415
- 976
Hebu eleza kidogo kuhusu automatic irrigation.
Naam.mifumo hii ya umwagiliaji inalenga kutatua matatizo makuu katika kilimo
1:manpower ya kumwagilia shamba.kwanimifumo hii hutumia solar power (40awtts-100watts ) kuendesha microntroller ndogo inayofanya kazi ya kufunga na kufungua bomba kutoka kwenye tank ya kuhifadhia maji au kuwasha water pump ili kuruhusu maji kwenda kwenye shamba pale inapobaini kuwa mimea inahitaji maji na kufunga pale inapojiridhisha kuwa udongo una maji ya kutosha hii ni economic zaidi kwa mazao yanaota kwa mashina mfano Nyanya ,matikiti na hata yanayoota kwa sensa
2;maeneo yenye upungufu wa maji(area with inadequate irrigation water sources).
mifumo hii ni mizuri pale panapokuwa hakuna maji ya kutosha kwa ajili ya umwagiliaji.kwani ni wazi kwamba unapomwagilia ndoo ya maji kwenye shina la mnyanya sio maji yote yatatumiwa na mnyanya .bali kitaalamu utakuta nusu lita ndio inayotumika tu mengine hupotea kama mvuke(evaporation ,aeration) na hivyo maji kupotea bure.mifumo hii hutumia sensor zinazo chimbiwa karibu na mmea ili kuweza kutambua matumizi sahihi (economic) ya maji ili kuepusha maji kupotea bure.
Faida kubwa ya mfumo hii .hujiendesha yenyewe katika kipindi chote cha mimea iwapo shambani bila kuhitaji usaidizi hivyo kuondoa tatizo la manpower.mitambo hutoa alarm na kujizima maji yanapo kwisha kwenye tanki ya maji .unapaswa kuhakikisha maji hayaishi kwenye chanzo.