Kilimo cha maembe ya kisasa

Na the best Kilimo ni Permanent Crops....yanazaa kila mwaka utakunata tu na soko zuri kipindi fulani...TULIME embe ndugu zangu
 
Hivi hakuna njia ya kitaalam yakufanya maembe yaive katka msimu tofaut na huu wa kawaida ili mtu apge pesa kivyake vyake
Zipo unafanya induction ya enzyme kwa kupulizia hivyo miti inaanza kuzaa na unafanya intensive irrigation,fertilization ili mambo yawe mazuri
 
Ili ufanikiwe katika jambo lolote unatakiwa ulifanye tofauti
 
Sasa si bora aliseme tumbaku kwa heka 10 anakuwa amezidi
 
Tango wengine wanaita tanga ni moja ya embe zinazohitajika zaidi viwandani
embe tango ni zile embe za tabora(wengine huziita boribo za tabora), embe tanga ni hizi embe zinatoka tanga(kule tanga wanaziita viringi(kwa umbo lake la mviringo))
 
Mkuu Bara Bara ya 5, unaendeleaje...umefanikiwa kuanza?

Nakushauri pia ujiunge na chama cha wakulima wa embe AMAGRO-Association of Mango Growers.

Kule utapata network ya kujuana na wakulima wenzio kama mimi na pia kupata utaalamu wa kilimo cha maembe kutoka kwa wakulima wazoefu.

Karibu sana kundini-mtafute katibu wa chama Mzee Mkopi @ 0715-312 036(nami nilipata habari zake humu JF zamani kidogo).

Kila la kheri-ni safari yenye matumaini ingawa kuna changamoto nyingi ndani yake!
 
Asante sana Mkuu...Nimeshapanda miche 450 kwa spacing ya 10x10m. Mzee Mkopi nimeongea nae na kanipa madini mazuri sana na AMAGRO nitajiunga very soon. Niko mbioni kuongeza miche mingine 300 ya Keit ili msimu huu niwe nayo 750.Nashukuru niliyopanda Nov.24 imeshakamata na nataraji nitoe nylon na kuondoa matawi chini yake
 
Unajua nashangaa watu wanacha kupanda mikaribea wakati Haina gharama yoyote ya uendeshaji
 
Juzi tu nimeng'oa Miche ya nyanya nusu heka😄 nimenunua 🐓 hata week hajafikisha ameanza kutaga
 
Nimetoka shamba wiki hii,..nashukuru miche yangu 500 inaendelea vizuri ingawa kama 50 hivi imekufa. Nimeiwekea mbolea ya samadi na kuipalilia.
Wasi wasi wangu ni kama itavuka kiangazi hiki maana nimepanda kwenye ardhi ya kidongo ingawa imeshika na
inatoa majani mapya. Kama tafanikiwa kuivusha na kiangazi hiki,basi mwezi wa 11 mwaka 2025 taongeza mingine 500 ili niwe na 1000.
 
Mkuu ingia gharama ya kumwagilia, mwaka huu mvua chache hata njombe ya mvua. Tafuta makopo ya maji kila mche makopo 4. Jaza maji toboa tundu yadondoke walau wiki moja. Tumia boda kubeba maji.
Huo mradi ushaenda kilichobaki ni kuboresha.
Tafuta mbolea ya HAKIKA ita bust haraka inauzwa 45elf kwa mfuko . Ina composite 25% hivyo ni kama samadi ilioboreshwa.
Uja piga picha miche? Tunafuatlia kwa karibu, waliokukatisha tamaa wataaibika soon.
Watoto wako hawata andamana kudai serikeli iwa ajili, umeisha waandalia ajira ya kudumu.Hayo mambo watanzania tunatakiwa kuyafanya,big up.
 
Hii mvua na mimi kuna miti imeteketea.
Hili wazo la makopo nalibeba. Maana nimetoka site leo tumeliongelea na hapa jukwaani napo nimelikuta
 
Asante sana Mkuu...hayo makopo yana ujazo upi??lita 1 au 0.5.??Vp na hiyo mbolea kwa Dar nitaipata wapi?
 
Nafikiri zoezi hili tulianza mwezi wa 8 maana kwa mujibu wa TMA mvua zitakata Mei.
 
Mkuu mbali na Keit, ni aina zipi wanashauri?
 
Reactions: Lax
Ushauri mzuri, kwenye kienyeji ni kweli ila tunataka tuwahi kurejesha capital. Kuhusu kupunguzia nakubaliana na wewe.
Mnaangalia kurejesha capital ilhali mnatuua.Pesa bhana.
 
Wamezaliwa na kukuta msitu wa miembe,kenta nzima kwa elfu 30.
Hahahahahahaha.
Kuna comment zingine zinakatisha tamaa sana japo huenda ikawa ndio ukweli wenyewe,unaweza ukapanda basi na kurudi nyumbani kwenda kulala.
 
Dah ama kweli kila kazi ina changamoto yake,ukiwakuta motivational speakers wanasimulia unaweza ukadhani ni jambo jepesi tu kumbe hadi uhondo wa ngoma uingie ucheze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…