kilimanjaro stars vs harambee stars

PingPong

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
926
159
Wadau wa michezo muda si mrefu kipute cha mchezo wa kirafiki kati ya kilimanjaro stars na harambee stars kitaanza. Kocha wa kilimanjaro ameonyesha wasiwasi wake kwenye maandalizi haya ya kombe la tusker challenge cup kwa kuwakosa mabeki wake wa kati ambao wanakipiga kwenye timu ya zanzibar na wakati huohuo kocha wa harambee amejigamba kuwa atawafunga watani wake kwa sababu anawajua vilivyo. Wadau wenye updates za mchezo huu wa kirafiki tunaomba mtujuze.
 

PingPong

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
926
159
duh, nimepewa taarifa kuwa game limeahirishwa, litachezwa jumanne badala ya jumatatu, samahani sana kwa wote mliopata usumbufu. Btw muda ukifika updates plz.
 

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,469
722
Kilimanjaro Stars wanaandika bao la kwanza lililowekwa kimiani na guess who? Gaudence Mwaikimba baada ya kazi nzuri ya Mrisho Ngasaa dakika ni ya 18 sasa...
 

PingPong

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
926
159
Kilimanjaro Stars wanaandika bao la kwanza lililowekwa kimiani na guess who? Gaudence Mwaikimba dakika ni ya 18 sasa...
naona kijana ameanza na nguvu kasi, ngoja tuone kama ataendelea kuwika au ndio kaja na nguvu za soda
 

PingPong

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
926
159
kwa kweli inabidi wajitahidi ili walau Poulsen nae aanze kuhesabu vichwa alivyonyoa
 

Kilakshari

JF-Expert Member
Dec 13, 2008
350
20
Inafurahisha kama Kilimanjaro Stars inatia moyo. Ina kila sababu kulichukua kombe la challenge hasa kwasababu inacheza kwenye uwanja wake wa nyumbani ikiwa na msaada wa mashabiki wake. Poulsen alikuwa na wasiwasi na beki hasa beki wa kati, nyie mnaoona gemu mnaweza kutuambia beki kati ikoje?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom