Kilimanjaro: Polisi wapata ajali

Hapo miaka hiyo walikufa watalii wa Kijapan wakiwa na gari ya kitalii enzi hizo 'volkswagen combi" ndio kuna hiyo alama kama kumbukumbu. Kama sikosei walikuwa wajapan takribani 6 hivi.
Unaweza kumbuka ni mwaka Gani Mkuu
 
Ivi Na polisi hawatibiwi hadi wawe na PF3

Nauliza tu
 
Dah Jamani naonaga sana Hilo kaburi hapo nilikuwa sijui la nani haswa,.
Dah Japanese
Kama kumbu kumbu zangu zipo vizuri maana uzee ushaingia sasa ilikuwa ni miaka ya 80 ilikuwa stori kubwa sana by then. Wakati huo gari maarufu za kubebea watalii zilikuwa "volkswagen comb, volkswagen transpoter na Landrover mandolin 109".
 
Haimanishi kwamba nawaamini polisi. hao ni watu wahalifu waliovishwa sare na bendera kwenye mikanda yao
polisi ni VIBAKA
Ukweli mchungu.Kiufupi ni wahalifu wenye Vibali vya kubeba bunduki na kukamata watu
 
Kama kumbu kumbu zangu zipo vizuri maana uzee ushaingia sasa ilikuwa ni miaka ya 80 ilikuwa stori kubwa sana by then. Wakati huo gari maarufu za kubebea watalii zilikuwa "volkswagen comb, volkswagen transpoter na Landrover mandolin 109".
Dah Zaidi ya Miaka 40 Sasa ,itakuwa walikuwa wanatoka KIA au walikuwa wanaenda KIA
 
Pole mkuu, hizo ni mbinu wanatumia kukamata waharifu kwa sababu baadhi ya waajiriwa hushirikiana na majambazi kuiba Mali za mabosi wao.

Lakini pia inategemeana na lugha uliyoitumia siku hiyo, baada ya kupigwa Kofi Kuna namna ulivo react hiyo ilimfanya askari atambue kama umehusika au hukuhusika( ni siri yake) hizo ni saikolojia tu ambazo zinatumika kwenye baadhi ya vyombo vya usalama.
Lakini pia ungeshukuru jitahada zao walizofanya mpaka kuwakamata hao wezi kwani huwezi jua walipitia mazingira gani Hadi kufanikisha jambo Hilo.
 
Raia wangapi wanaenda vituoni kuomba msaada na wanapuuzwa kwa kuwa hawana chochote? Au tu kwa kuwa wanayemlalamikia ana uwezo na nafasi na hivyo huishia kupuuzwa? Hivi kwa polisi hawa mtu asiye na chochote wataka kunambia wanaweza kumsaidia?
 
Kuna siku nimeshuhudia raia kafukuzwa kama mbwa na matusi pale kaunta kupeleka malalamiko ya kudhulumiwa 10,000 askari anamwambia kabisa " yaani wewe usumbue watu kwa hela hiyo,toka hapa pumbavu,tulifikiri kuna hela ya maana,usumbue watu kwa hela hiyo,potea haraka sana kabla hatujakuwela lockup"
Sasa huyo ndio mwananchi wa kawaisa,unasemaje hapo?
 
Story nyingi ila bila idadi ya majeruhi na wafu bado haijanoga siyo ajali bali ni mazoezi ya kijeshi labda
 
Polisi sikuizi ndo magaidi!!🎃 wafe tu
 
Kweli Polisi hawakumtendea Haki. Lakini huyo polisi aliyemfukuza hapo kaunta inawezekana sio mkuu wa Kituo
 
Raia wangapi wanaenda vituoni kuomba msaada na wanapuuzwa kwa kuwa hawana chochote? Au tu kwa kuwa wanayemlalamikia ana uwezo na nafasi na hivyo huishia kupuuzwa? Hivi kwa polisi hawa mtu asiye na chochote wataka kunambia wanaweza kumsaidia?
Kama Polisi mhusika atazingatia Taratibu, Maadili na Weledi katika majukumu yake tena akiwa na hofu ya Mungu atamsaidia.
Lakini kama Polisi mhusika atatanguliza mbele maslahi binafsi kweli itakuwa ni vigumu kumsaidia mtu asiye na chochote bali atampuuza.
Lakini pia Tuone kwamba wapo wanaoenda kituoni wakitegemea Polisi ndo watakaomaliza changamoto iliyopo na wanasahau kwamba kwa kwenda Polisi ni hatua ya kwanza ili kuanzisha Mchakato wa kupata suluhisho kwani Polisi wakiona Hoja iliyoletwa ina mashiko huwa wanaipeleka Mahakamani kama Shauri au Kesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…