KILIMANJARO: Kijana afariki kwa kujinyonga Kata ya Machame, anakuwa kijana wanne kujinyonga katika kata hiyo ndani ya Miezi 18

KILIMANJARO: Kijana afariki kwa kujinyonga Kata ya Machame, anakuwa kijana wanne kujinyonga katika kata hiyo ndani ya Miezi 18

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
654
Reaction score
1,598
Kijana Mmoja mwenye umri wa miaka 35 ajulikanae kwa jina la Allen Malya anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia shuka lake, tukio hilo la kusikitisha limetokea katika Kitongoji cha Sereni Kijiji cha Usari, Kata ya Machame Narumu, Kilimanjaro.

Kaka Mkubwa wa marehemu ajulikanae kama Samora amesema alishtushwa na kitendo cha mdogo wake kutokuamka mapema kitu ambacho sio kawaida yake, hadi inafika saa nne asubuhi mlango wake ulikuwa haujafunguliwa ndipo alipoamua kwenda kucheki dirishani na kukuta marehemu akiwa ananing'inia na shuka shingoni, akaita majirani na baadaye polisi walifika na kuchukua miwili wake.

Hata hivyo, mwenyekiti wa kijiji hicho, Wilfred Maiko amesema kuwa hili ni tukio la mtu wa nne kujinyonga ndani ya Kijiji chake ndani ya mwaka mmoja na nusu na katika matukio yote hayo manne waliojinyonga wote ni vijana wa kiume.
 
Mleta uzi unawakilisha wajinga wengi sana tulio nao nchini wasioijua nchi yao vizuri. Tangu lini Machame ikawa Arusha?
 
Machame si ipo moshi jaman au kuna machame nyingne arusha. Anyway pole yake
 
Moshi Kilimanjaro sio Arusha, apumuzike kwa amani.
 
Mleta uzi unawakilisha wajinga wengi sana tulio nao nchini wasioijua nchi yao vizuri. Tangu lini Machame ikawa Arusha?
Soma kwanza uzi uelewe vizuri, huenda wewe ndio unawakilisha lile kundi la watanzania wavivu kusoma.
 
Mleta uzi unawakilisha wajinga wengi sana tulio nao nchini wasioijua nchi yao vizuri. Tangu lini Machame ikawa Arusha?
Mbona kuna majina mengi tu yanajirudia sehemu mbalimbali?

Mfano kilombero ipo maeneo mikoa tofautitofauti, kuna ostabei, kuna rombo, kuna msasani arusha na Dar
 
Nitolee upumbavu wako hapa.
Upumbavu unao wewe mvivu wa kusoma habari kwa umakini. Hivi wewe ndio ulisema una uwezo mkubwa sana ukilingqnisha na wanajf wengi na unataka uleft kabisa?
 
Upumbavu unao wewe mvivu wa kusoma habari kwa umakini. Hivi wewe ndio ulisema una uwezo mkubwa sana ukilingqnisha na wanajf wengi na unataka uleft kabisa?
Kama sijasoma uzi ningeonaje kijiji cha Useri kilichopo Arusha badala ya Kilimanjaro? Kwa wewe uliumbwa utetee ujinga?
 
Kama sijasoma uzi ningeonaje kijiji cha Useri kilichopo Arusha badala ya Kilimanjaro? Kwa wewe uliumbwa utetee ujinga?
Ni wapi pameandikwa kijiji cha Useri? Mkuu unawakilisha kundi la wavivu wa kusoma na kuelewa habari kabla ya kutoa maoni yako. Na watu kama wewe tupo wengi sana Tanzania, no wonder nchi masikini.
 
Ni wapi pameandikwa kijiji cha Useri? Mkuu unawakilisha kundi la wavivu wa kusoma na kuelewa habari kabla ya kutoa maoni yako. Na watu kama wewe tupo wengi sana Tanzania, no wonder nchi masikini.
Jomba naona wewe umeamua kuwa mpuuzi kwa sababu unazozijua mwenyewe. Maoni ya watu wengine walioshangaa Machame kuwa Arusha hujaona? Mtu kama wewe ni laana kwa taifa.
 
Hili tatizo lilikuwa Iringa sasa linahamia Machame
 
Back
Top Bottom