Kilichotokea jana Tanzania kimetokea leo huku Puerto Rico muda si mrefu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
Kuna Mwasiasa mmoja huku nchini Puerto Rico ambako kiukweli ndiyo makazi yangu ya muda mrefu kuliko hata huko nyumbani nchini Rwanda anaitwa Ndutu Ssuli nadhani wale wafuatiliaji wakubwa wa Siasa za huku nchini Puerto Rico mtakuwa mnajua nae hivi punde tu yamemkumba yale ambayo yamemkuta jana Mwanasiasa maarufu huko Kwenu nchini Tanzania Bwana Tundu Lissu.

Huyu Mpuerto Rico Ndutu Ssuli ni ' machachari ' sana hadi amefikia hatua ya kuitikisa Serikali nzima ya Puerto Rico na mara nyingi sana amekuwa akiingia ' matatani ' na Polisi wa huku lakini huwa anashinda Kesi zake na kuachiwa japo Yeye siyo Mwanasheria bali ni ' Mwanasiasa ' mkubwa tu huku.

Kuna makampuni kadhaa ya Rasilimali kubwa na nyingi zilizopo huku Puerto Rico kama za Madini pamoja na Utalii huyu Ndutu Ssuli hupendelea sana kuzizungumzia na kusema kuwa Sisi wakaazi wa Puerto Rico hatuna haja ya kuwa masikini hivi tulivyo kwani ni matajiri isipokuwa tu Serikali yetu huku ndiyo inatudidimiza huku mara kwa mara akimlenga hasimu wake Mkuu Rais wa Puerto Rico kuwa ni mnyonyaji, mbabe fulani na kuna siku pia aliwahi kusema ni katili pia.

Katika hali isiyo ya kawaida kabisa mwezi mmoja tu uliopita kuna Meli moja kati ya Tatu ambazo Serikali ya huku nchini Puerto Rico ilikuwa imeshanunuliwa na inakuja lakini kukatokea taarifa ya kwamba hiyo Meli imezuiliwa nchini Singapore mpaka Serikali ya Puerto Rico itakapomaliza kulipa deni lake la Mafuta ghafi iliyoyaagiza mwaka jana.

Ndipo hapo akaibuka tena huyu Mwanasiasa Ndutu Ssuli na kutupasha Sisi Wana Puerto Rico kuhusiana na hii taarifa ' nyeti ' ya kukamatwa kwa Meli yetu hali ambayo iliishtua sana Serikali nzima ya Puerto Rico na ikaanza kuhaha kama vile kuficha hii taarifa ila ikashindwa na baadae nayo pia ikakiri kutokea kwa hilo jambo.

Wakati akiwa anazungumza mara kwa mara huyu Mwanasiasa Ndutu Ssuli kila mara amekuwa akisisitiza kwamba Yeye wala haogopi chochote kile na tena akiuwawa basi Kwake atafurahi kwakuwa atakuwa ameacha alama nyuma ya Ujasiri na hadi akaenda mbele na kusema kuwa hizo taarifa zote ' Nyeti ' amekuwa akizipata kutoka huku huku ndani ya Serikali ya Puerto Rico.

Sasa mara baada ya hili tukio lake la ' kushambuliwa ' na hivi sasa anatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya hapa Puerto Rico japo kuna fununu kuwa huenda akasafirishwa sasa hivi kuwahishwa kwenda Burma kwa matibabu zaidi ila bado taratibu za kumletea Boti iendayo Kasi zinafanyika ili awahishwe.

Kuna hizi ' sintofahamu ' kadhaa zimetokea huku ambazo nikiwa kama mwana Puerto Rico niliyetukuka nimeona siyo vibaya ' nikishea ' nanyi Watanzania mliopo huko ili tuweze kujua ukweli labda wa huyu Mwanasiasa ' machachari ' huku Puerto Rico Bwana Ndutu Ssuli nani atakuwa nyuma ya tukio zima la hili ' Shambulio ' lake la hatari lililotokea hivi punde tu.

Kuna wanaosema kwamba.....

  • Serikali ya Puerto Rico imehusika na huo ' Umafia ' dhidi yake
  • Maadui zake Kisiasa ndani ya Chama chake maarufu cha MADECHA wamehusika
  • Wale waliokuwa wakimpa taarifa ' Nyeti ' na kawaumbua hadharani wamehusika
  • Wale Marafiki zake wenye Makampuni huko Ulaya wameamua ' kumuondoa ' kwa kuhisi labda Kawasaliti
  • Maadui tu Wakubwa wa Serikali ya Puerto Rico wameamua kulifanya hili ' makusudically ' kabisa ili kuweza ' kuitikisa ' Serikali na nchi nzima ya Puerto Rico isitawalike
Je Wewe Mkuu unadhani hapo lipi linaweza kuwa la Kweli katika hili tukio baya la huyu Mwanasiasa wetu wa Chama cha MADECHA Bwana Ndutu Ssuli huku nchini Kwetu Puerto Rico? Nitashukuru sana kwa michango yenu kwani naamini kabisa kuwa humu JF ni Kisima tosha cha maarifa hivyo angalau nami nitaweza kupata kidogo picha juu ya sakata zima.

Akhsanteni.

Nawasilisha.
 
jamaa katumia kiswahili aisee, nilishangaa puerto rico na burma wapi na wapi kisha mtu apelekwe kwa boat inayoenda speed, na hilo jina limekaa ka kikwetu, sasa baadae nimemuelewa
 
Hapo raisi wa puerto rico anahusika,

Kama sikosei ameshapelekwa Burma maana nimeona boti moja imepita kwa kasi sana na mimi nipo huku pia tufahamiane mkuu
 
Back
Top Bottom