Kilichotekea Geita Gold FC ni ushamba tu

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Mpaka ligi inaanza bado watu wanasikika hawapo kambini.

Ilianzia kwa kocha Minziro, wenzao wanawatambulisha wachezaji kwa maana ya kujiandaa kwa ligi, ikasemekana yupo Dar na hajasaini mkataba wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Jana tu ikasikika mchezaji G. Mpole hayupo kambini na akasikika anasubiri mkataba mpya au kujiunga na timu nyengine. Wakati akihojiwa alikuwa kwake Mbeya.

Hapa ndio natatizwa kwani timu hii inatuwakilisha kimataifa yaani mashindano ya CAF.

Sasa ni aidha kocha Minziro na mchezaji G. Mpole wamelewa sifa na kuanza kudai pesa nyingi ya kulipwa na klabu au uongozi kimpira hawako makini.

Ndio maana nawafananisha na USHAMBA tu walichokifanya.
 
Vitu usivyovijua ni bora unyamaze, hiyo ni nyumba ya jirani ina siri nyingi tulia mkuu.
Unataka mtu aingie kambini bila mkataba?
Kama ni suala la mkataba basi ni tatizo la pande zote mbili kwa maana walipaswa wakamilishane kabla ya msimu wa ligi kuanza.

Nakukumbusha hawa wanatuwakilisha katika mashindano ya kimataifa yaani CAF. Mbona sijazungumzia timu nyengine ambazo hazipo kwenye mashindano hayo?

Ruvu Shooting wao walikuwa Unguja wakijiandaa na ligi na hawapo katika uwakilishi wa nchi CAF.
 
Hiz timu zinazomilikiwa na halmashauri mara nyingi zinakiwango chao Cha matumizi

Nachokiona kwa geita gold fc wao wanawaza mbali lakn pesa ndio kikwazo

Wangefuata model za timu Kama polisi mbeya city au dodoma jiji wasingekuwa na shida katika uendeshaji

Wakumbuke pesa ya timu haitoki mfukon kwa mtu Kama mtibwa Simba na yanga wao wanaweza kuamua tu kumleta yeyote kwa wakat wowote tofaut na geita had madiwan wakae chini wakubaliane matumiz ya timu

Viongoz wanoiendesha geita gold n watu wa 10% Sana

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mpaka ligi inaanza bado watu wanasikika hawapo kambini.

Ilianzia kwa kocha Minziro, wenzao wanawatambulisha wachezaji kwa maana ya kujiandaa kwa ligi, ikasemekana yupo Dar na hajasaini mkataba wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Jana tu ikasikika mchezaji G. Mpole hayupo kambini na akasikika anasubiri mkataba mpya au kujiunga na timu nyengine. Wakati akihojiwa alikuwa kwake Mbeya.

Hapa ndio natatizwa kwani timu hii inatuwakilisha kimataifa yaani mashindano ya CAF.

Sasa ni aidha kocha Minziro na mchezaji G. Mpole wamelewa sifa na kuanza kudai pesa nyingi ya kulipwa na klabu au uongozi kimpira hawako makini.

Ndio maana nawafananisha na USHAMBA tu walichokifanya.
kudai kuongezea malipo kama mikataba imeisha ni haki yao na wala siyo kulewa sifa.

Cha kushangaza inakuwaje wapo disorganize wakati soon mechi za kimataifa zinaanza? Na pia hata haisikiki usajili wa maana au kambi.
 
Yule mkurugenzi wa halmashauli ya geita bibie Zahra Michuzi anapenda show off sana, nilinusa kitu ukiona kiongozi camera nyingi ujue jambo hakuna.

Pamoja na kutegemea halmashauli ila kama wangekuwa na viongozi wazuri wangeoganize wananchi na wafanyabiashara wa geita wakaweka kitu kwenye kapu la kuendeshwa timu! Ila viongozi wengi kwenye halmashauli ni mchwa hawawezi kuaminika.
 
Yule ni another version ya Barbara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom