GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,292
- 6,769
Siku hiyo nikiwa na mawazo ambayo yalikuwa yanasumbua kichwa changu niliamua
Kwenda baa moja ambayo ilikuwa ina vikundi vya maonesho mbalimbali.
Nikaagiza soda, mtaani nimezoea soda ni 500 tu, pigo la kwanza nikalipata
kwa kuuziwa soda Tsh 1,000.
Nikawaza, nikaona Labda hii nyingine nalipia onesho la watu wanaocheza na nyoka.
Hicho kikundi kilileta Burudani ya kufana, wanawabwaga sakafuni nyoka kama
Wanane hivi, kisha wanawazuia wasifike kule waliko wateja. Hao nyoka walikuwa
warefu balaa, yaani kule kuwatazama tu mwili unasisimka.
Ilipofika majira ya saa 4 kasorobo wakawabwaga wale Nyoka sakafuni kama kawaida,
Duh! Ghafla umeme ukakatika, wakati huo nyoka wako sakafuni na wanakuja
Upande ambao wateja wanakaa.
Usifanye Mchezo namna tulivyoruka na kukanyagana siku hiyo, Watu waliweza
kupaa mita kumi mpaka kumi na tano kwenda juu kwa kuguswa na Gidamu/kamba
ya kiatu chake au mkanda wake mwenyewe.
Mwanga hafifu wa mbalamwezi uliniwezesha kuona jinsi watu wenye Vitambi
Vya nguvu walivyokuwa wanaruka kwa usahihi kabisa zile meza za plastiki za Baa.
Aaah! Wakuu hilo tafrani siwezi kulisahau, Umeme ulirudi baada ya Dakika kumi
Lakini sidhani kama hata wahudumu walikuwepo pale Baa wakati umeme unarudi.
Kilichonichekesha zaidi ni jinsi watu waliokuwa nje ya Baa walivyotoka nduki kuwazidi
wale waliotoka ndani huku wakiwa hawajui wenzao wanakimbia nini.
Yaani sijui kilichoendelea, maana ndani ya dakika hizo kumi tayari nilikuwa Kituo
Cha daladala tayari kurejea nyumbani, SINA HAMU.