Pengine kauli ya Mheshimiwa raisi inahitaji ufafanuzi. Amepiga marufuku safari za kwenda nje ya nchi kwa watumishi wa uma ili kubana matumizi. Kwa lugha hiyo amezuia government sponsorship kwa safari za nje kwa watumishi wa umma isipokuwa kwa kibali chake.
Katazo hilo linasemaje pale mtumishi wa umma anakwenda nje ya nchi kwa gharama zake na mwajiri wake hana tatizo na hilo? Au pale mtumish wa umma kapata mfadhiri binafsi nje ya serikali. Katika hili hizi katazo hilli linamashiko gani?
Ninaanza kuapta wasiwasi kwamba mheshimiwa raisi hakueleweka kama kakataza matumizi ya fedha za serikali kwa safari za nje ya nchi kwa watumishi wa umma isipokuwa kwa kibali chake, ama kakataza watumishi wa uma kwenda nje ya nchi hata kama safari zao hazigharimiwi na serikali?
Ninachelea inawezekana baada ya mheshimiwa raisi ku dissaprove maombi yao, walipata mfadhilli mwingine zaidi ya serikali. Jambo la kuweka bayana. Je hata kama mtumishi wa uma atapata ufadhili binafsi, atalazimika kuomba ruhusa kwa magufuli ni asafiri hata kama hatumii fedha za serikali? Kwa hiyo sas likizo na uratibu wote wa matumizi ya raslimali watu kwa sector ya umma nzima yatafanywa na raisi?
Ni hilo tu.