UKiwa na akili timamu huwezi kutumia lugha ya matusi katika mtandao eti kumtukana mtu kwa sababu yeye kakutukana. Kuwambia wenzio nyumbu na kutegemea mrejesho wa heshima ni jambo la ajabu sana na nadra kutokea na hasa kwa maadili ya sasa ya kitanzania.
Ni vizuri ukawa wa kwanza kuwaheshi wenzi ili nao waweze kukuheshimu. Kutukanana humu ndani sidhani kama ni jambo la busara.
Sie tunatafuta Rais na atatoka either CCm au CHADEMA kupitia muungano wao wa UKAWA na hapa huwezi kubisha au kulazimisha hisia zako ziwe za kila mtu.
Tumieani jukwaa hili kuelimishana kistaarabu maana tunaosoma maoni yenu tuko wengi sana na tunataka kuona hoja zenye hekima na busara na si matusi.