Umeongea mengi mazuri yenye kujenga lakini hii diplomasia ifanywe kwa mambo mengine sio kuvusha mifugo kienyeji bila taratibu za kudhibiti magonjwa na pia janga la uharibifu wa mazingira kutokana na ufugaji holela ni kubwa sana hapa kwetu.
Tayari hapa nyumbani tuna migogoro mikubwa na nchi inakuwa jangwa kwa kasi maeneo ya wafugaji, athari zake ni kubwa mno sio za kuzichukulia kirahisi na kutaka kuwafurahisha jirani. Ile njaa na ukame wa Kenya utakuja kwa kasi zaidi.
Diplomasia ifanyike kwenye mambo ya ukanda huru wa kibiashara na ajira n.k. sio mambo ya afya na mazingira.