kimboka one
JF-Expert Member
- Jan 23, 2010
- 734
- 85
Wanajamvi nimeona kupitia jamvi hili niwasaidie wana CCM walau kutambua chanzo cha anguko lao. Hii ni baada ya utafiti ambao ninaendelea kufanya lakini nimeona ni vema niwalete sehemu hii ya kwanza walau kama wapo wenye ROHO wafunguke na kuona.
CCM baada ya kifo cha mwalimu Nyerere aliyekuwa akiwabana sana, ilianza kupoteza mwelekeo wa kuongoza na kuwa chama cha watu kujipatia ulaji,tabia ambayo sasa imekua na imeanza kuwatokea puani.
Nitatoa mifano michache tu ya kinachosababisha anguko la CCM.
Kwanza katika uchaguzi wa arumeru ambao kijana machachari Joshua Nassari (mb) aliibuka mshindi.
Sababu zilizo sababisha CCM kuanguka ni hizi hapa:
wanakamwacha mtu ambaye aliwahi kugombea jimbo hilo hilo mara mbili katika kura za maoni za CCM na kuibuka mshindi wa pili,lakini zaidi ni kiongozi wa chama siku nyingi na sasa na katibu wa itikadi na uenezi wilaya ya nyamagana,ukienda mbali zaidi utagundua pia wananchi walimtaka huyo lakini kwasababu tu ya tabia mbaya sana ya CCM kukumbatia mambo haya mawili walimpiga chini,kwa sababu hana sifa wanazotaka wao.
jambo la kwanza,ndani ya CCM kama Baba yako hajawai kuwa Mkuu wa wilaya,Mkuu wa Mkoa,Mbunge,waziri,katibu wa wizara,katibu wa chama na nafasi nyingine kubwa ndani ya serikali na chama HAUWEZI KUPATA NAFASI YA KUONGOZA. hili jambo litaitafuna sana CCM na kwa kuwa hawana roho hawajali wala hawatakaa wajifunze kuwa wananchi wameshachoka na huo ujinga wa kurisishana madaraka,hawawezi kuona wenzao wa CHADEMA wao wanaangalia ni mtu gani Wananchi wanamtaka?.hapo arumeru kuna wanachama wengi wa CDM wenye pesa lakini wamewaacha wamechukua kijana kutoka familia duni mtoto wa mchungaji na mama ntilie bila kujali kama baba yake alikuwa nani? Ndani ya CDM.
hili kwa CCM haliwezi kutokea maana ukitangaza nia tu swali la kwanza huwa ni mtoto wa nani?,je Ana pesa?. Hiki ndicho kilicho wauwa pale arumeru.
Jambo la pili CCM ukiwa na uwezo wa kufikiri ulio sahihi na kuweza kutazama mambo kiualisia(yaani kusema nyeupe ni nyeupe na si nyeupe kusema ni nyeusi na nyeusi kusema ni nyeupe),hauwezi kupata nafasi ya kuongoza hata siku moja ndani ya CCM.
CCM wanataka YES MAN tu ambaye kila anachosema kiongozi wake anasema ndio kiongozi,ukipinga kidogo tena kwa nia ya kujenga wanakuita CDM.
sio kweli kwamba ndani ya CCM wote ni wajinga na wezi kama wengi wanavyodhani hasha,wapo vijana wengi tu mimi ninawafahamu vizuri tena wenye dhati ya kweli na uwezo ila wazazi wao ni kama wa Nassari hawajawai kuwa viongozi tena hawana pesa.mbaya zaidi vijana hao wanauwezo wa kusema ukweli mbele ya viongozi wao jambo linalowafanya waonekane wapinzani eti kwa kusema ukweli,wakati mwingine Nape akiguswa husema kijana ukiwa mnafiki ujanani uzeeni utakuwa mchawi lakini ndiyo huyo huyo anakuwa wa kwanza kusema yule ni chadema.lakini ukiwa kama LUSINDE aka kibabaji wanakupenda kweli kweli.ni kweli sasa imefika mahali ata CCM wanaamini kila mwenye uwezo wa kusema ukweli na kujenga hoja nzito ni Mwanachadema.hili nalo limechangia kuiangusha CCM.
Kwa leo ninaishia hapa katika sehemu hii ya kwanza,nitawaletea sehemu ya pili ponde tu. Mimi humu jamvini najua watu wanajiuliza ni chama gani? Hawapati majibu maana ninabadilika badilika.ukweli ni kwamba mimi si shabiki wa vyama ninasimama katika uhalisia kama mtu wa CDM akikosa nitasema amekosa wa CCM kadhalika na chama kingine chochote bila kujali uhusiano wangu nayeye na ifike mahali watanzania tuweze kuona hivyo.karibu nawe uweke mawazo yako.

- Makundi ndani ya chama,kila kundi likitaka kuonyesha nguvu yake katika chama.