Kilicho iangusha CCM arumeru hiki hapa (aibu tupu!!!!!) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilicho iangusha CCM arumeru hiki hapa (aibu tupu!!!!!)

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by kimboka one, Apr 4, 2012.

 1. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Wanajamvi nimeona kupitia jamvi hili niwasaidie wana CCM walau kutambua chanzo cha anguko lao. Hii ni baada ya utafiti ambao ninaendelea kufanya lakini nimeona ni vema niwalete sehemu hii ya kwanza walau kama wapo wenye ROHO wafunguke na kuona.


  CCM baada ya kifo cha mwalimu Nyerere aliyekuwa akiwabana sana, ilianza kupoteza mwelekeo wa kuongoza na kuwa chama cha watu kujipatia ulaji,tabia ambayo sasa imekua na imeanza kuwatokea puani.

  Nitatoa mifano michache tu ya kinachosababisha anguko la CCM.

  Kwanza katika uchaguzi wa arumeru ambao kijana machachari Joshua Nassari (mb) aliibuka mshindi.

  Sababu zilizo sababisha CCM kuanguka ni hizi hapa:


  1. Makundi ndani ya chama,kila kundi likitaka kuonyesha nguvu yake katika chama.
  Pia kufanya chaguo lisilo la wananchi wakati wa kura za maoni,hapa nieleze kidogo,hivi hawa watu sijui kama wana ROHO ama akili zao hazifanyi kazi vizuri,yaani mtu anatoaka zake huko hajawai kufikiria ata kuwa mwenyekiti wa kijiji mnakuja kumpa apeperushe bendera ya chama ati tu baba yake alikuwa kiongozi au eti tuna mpa pole kwa kufiwa na baba yake,pole kwa kumpa ubunge?,Mama Nyerere alivyofiwa na na mume wake mlimpa nini?,je familia ya Sokoine?,hizi ni hoja za kitoto kabisa na niaibu kwa mtu kutamka.

  wanakamwacha mtu ambaye aliwahi kugombea jimbo hilo hilo mara mbili katika kura za maoni za CCM na kuibuka mshindi wa pili,lakini zaidi ni kiongozi wa chama siku nyingi na sasa na katibu wa itikadi na uenezi wilaya ya nyamagana,ukienda mbali zaidi utagundua pia wananchi walimtaka huyo lakini kwasababu tu ya tabia mbaya sana ya CCM kukumbatia mambo haya mawili walimpiga chini,kwa sababu hana sifa wanazotaka wao.

  jambo la kwanza,ndani ya CCM kama Baba yako hajawai kuwa Mkuu wa wilaya,Mkuu wa Mkoa,Mbunge,waziri,katibu wa wizara,katibu wa chama na nafasi nyingine kubwa ndani ya serikali na chama HAUWEZI KUPATA NAFASI YA KUONGOZA. hili jambo litaitafuna sana CCM na kwa kuwa hawana roho hawajali wala hawatakaa wajifunze kuwa wananchi wameshachoka na huo ujinga wa kurisishana madaraka,hawawezi kuona wenzao wa CHADEMA wao wanaangalia ni mtu gani Wananchi wanamtaka?.hapo arumeru kuna wanachama wengi wa CDM wenye pesa lakini wamewaacha wamechukua kijana kutoka familia duni mtoto wa mchungaji na mama ntilie bila kujali kama baba yake alikuwa nani? Ndani ya CDM.
  hili kwa CCM haliwezi kutokea maana ukitangaza nia tu swali la kwanza huwa ni mtoto wa nani?,je Ana pesa?. Hiki ndicho kilicho wauwa pale arumeru.

  Jambo la pili CCM ukiwa na uwezo wa kufikiri ulio sahihi na kuweza kutazama mambo kiualisia(yaani kusema nyeupe ni nyeupe na si nyeupe kusema ni nyeusi na nyeusi kusema ni nyeupe),hauwezi kupata nafasi ya kuongoza hata siku moja ndani ya CCM.

  CCM wanataka YES MAN tu ambaye kila anachosema kiongozi wake anasema ndio kiongozi,ukipinga kidogo tena kwa nia ya kujenga wanakuita CDM.

  sio kweli kwamba ndani ya CCM wote ni wajinga na wezi kama wengi wanavyodhani hasha,wapo vijana wengi tu mimi ninawafahamu vizuri tena wenye dhati ya kweli na uwezo ila wazazi wao ni kama wa Nassari hawajawai kuwa viongozi tena hawana pesa.mbaya zaidi vijana hao wanauwezo wa kusema ukweli mbele ya viongozi wao jambo linalowafanya waonekane wapinzani eti kwa kusema ukweli,wakati mwingine Nape akiguswa husema kijana ukiwa mnafiki ujanani uzeeni utakuwa mchawi lakini ndiyo huyo huyo anakuwa wa kwanza kusema yule ni chadema.lakini ukiwa kama LUSINDE aka kibabaji wanakupenda kweli kweli.ni kweli sasa imefika mahali ata CCM wanaamini kila mwenye uwezo wa kusema ukweli na kujenga hoja nzito ni Mwanachadema.hili nalo limechangia kuiangusha CCM.

  Kwa leo ninaishia hapa katika sehemu hii ya kwanza,nitawaletea sehemu ya pili ponde tu. Mimi humu jamvini najua watu wanajiuliza ni chama gani? Hawapati majibu maana ninabadilika badilika.ukweli ni kwamba mimi si shabiki wa vyama ninasimama katika uhalisia kama mtu wa CDM akikosa nitasema amekosa wa CCM kadhalika na chama kingine chochote bila kujali uhusiano wangu nayeye na ifike mahali watanzania tuweze kuona hivyo.karibu nawe uweke mawazo yako.
   
 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  hakuna cha makundi wala nini bali wananchi wamechoka na ahadi hewa + uwongo.
   
 3. daywell

  daywell Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana jipya!
   
 4. Walikughu

  Walikughu Senior Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umechambua vizuri sana, Chama cha mapinduzi kwa sasa kinaelekea kupoteza mwelekeo na kila mtu lwake, ukiangalia nguvu za dola zinatumika sana ili kutisha wananchi lakini kwa sasa wananchi wengi wanafahamu kuwa wanaonewa na wanauwezo wa kufanya mabadiliko kwa kupitia kura na si vinginevyo. CCM hilo bado hawamini pamoja na hayo ni lazima tushukuru chama cha Chadema kuweza kufanya Elimu kwa umma kupitia "operation" sangara na hii walianzia ile mikoa ambayo kulikuwa ni ngome ya CCM. Na jambo la msingi ni kupata viongozi ambao wako tayari kuwatumikia wananchi kwa moyo wote, ndani ya chama cha mapinduzi wapo lakini hawapewi nafasi kwa sababu hawana pesa za kuhonga ila nawashauri watafute maeneo mengine ambayo wanaweza kupeleka fikra zao na Tanzania ikaenda mbele katika maendeleo.

  Hongera kijana Nassari
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu hapo natofautiana kidogo na wewe, jamaa alipigwa chini sababu ya rushwa, kinachoiua ccm ni matuzi ya pesa, nakumbuka waliwaludishia mchague upya mlifanyeje zaidi ya kujichukulia pesa na kumpitisha sioi!
   
 6. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hawawezi kudanganya watu siku zote,njia ya muongo ni fupi.
   
 7. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  :A S shade:Kimboka One nimekusoma. Ila natamka wazi kwamba hoja ulizozitoa si za kiutafiti. Utafiti ni mtiririko wa Kisayansi wenye kutambua tatizo kulijengea maswali/mabunio kisha kulitafutia majawabu uwandani. Hoja ulizozitoa zote hata Babu yangu pale Morotonga anazijua vivyo hivyo ulivyozitoa. Kwa hiyo nitofautiane na wewe kusema kwamba uliyoyasema yaweza kuwa ya kweli lakini yana upungufu mkubwa ikiwa tutayaita majawabu ya kiutafiti (research findings). Sana sana hiyo itakuwa ni matumizi ya common sense tu!!!:smile-big:
   
 8. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mh.inawezekana yote uliyosema nikwel,lakni kikubwwa kilcho iangusha ccm ni MASHAMBA meru kuna mgogoro mkubwa wa aridhi.mashamba yao yaliuzwa kwanguvu nawalio jarbu kupnga walipgwa zamoto.kama unabisha nenda kijji cha singisi watakujuza zaidi.
   
 9. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mkuu. Bado unashikilia research steps alizokufundisha mwalimu wako.research ni mtiririko maalum wa kukusanya taarifa na kuzitafsiri kulingana na mtazamo wako baada ya kurejea kwa watafiti wengine.mi bado ninaendea ata hivi hapa sitafuti alama mkuu.nilitaka nitoe ujumbe huo,ufundi haikuwa hoja yangu mkuu
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,055
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Achaneni na CCM jamani make ukiwaambia walikosea hivyo unalenga kuwashauri wajipange tena? ...kwa faida ya nani??kwa maana it's said,dont interupt when your enemy is making mistakes.. Sasa interuption hii unawasaidia kugundua nn kamanda?

  Sote tunaelewa mapungufu yao ila siyo kazi yetu ss kuwaambia kama kweli we need them out,then let the nature decide
   
 11. k

  kyening'ombe Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  muzoea vya kunyonga vya kuchinja hawezi, huku naweza kusema kwamba wanachama wa chadema waliamua kwa hali yoyote kushinda uchaguzi kwani ukiangalia kuanzia kwenye kampeni wananchi ,wanachamma na viongozi walionyesha umakini sana na hapa natoa mfano mmoja wa wabunge kuamua kuwa mawakara kitu ambacho siyo cha kawaida. yote haya yalitosha kuwafanya CCM washindwe kufanya mbinu zao chafu.
   
 12. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Magamba @ work
   
 13. k

  kaiyulankuba Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sikio la kufa halisikii dawa
   
 14. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni tafakuri yako wala si utafiti maana hujaonyesha method uliyotumia kuyapata hayo. Niongezee hapo tu kuwa kwa sasa wananchi wana ufahamu mkubwa wa kisiasa na wanataka mabadiliko hivo wanapima ni nani anayeonyesha kuleta mabadiliko. CCM waache mazoea ya zamani ama svo mbele inaweza kuwa giza kwao.
   
 15. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...nothing last forever.
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Sasa huko wanafanya nini? Kwa nini wanakubali kuishi nyumba moja na wezi? Kama si ujinga, ni nini? Ama ni walafi kama fisi, wanasubiri mkono wa binadamu udondoke, au ni wanafiki wakubwa. Vyo vyote vile, Nape na Lusinde hawatofautiani sana labda ujanja katika kula na kutumiwa.
  Sasa wanachokosa ni nini, ujasiri? Mbona kijana Nassari kaweza kujikomboa na sasa ni mbunge! Huo uwezo walio nao ndani ya CCM unawasaidiaje kama hawana wazazi wa kuwapakata? Kama wanataka kula kivulini huku wakiogopa kuhangaika juani basi hawatufai, wabaki huko huko CCM.
  Je, una hakika wana uwezo huo? Kama wanao kwa nini wasijiunge kabisa na upinzani? Ahaa, wanataka wale kipande chao cha keki na bado waendelee kubaki nacho! Basi wao ni hatari kuliko hata hao viongozi wao na bila shaka hiyo ndiyo sababu kubwa ya kutosikilizwa, je ni ndumilakuwili?
  Hapa, kusema kweli Kimboka one, sikuelewi una maana gani, yaani vijana hao kama Nape, wanaona heri wawe wanafiki na hivyo kupalilia njia waweze kuwa wachawi uzeeni! Kimboka one, lazima tukubaliane hapa kuwa hao vijana hawana nia, hekima wala ujasiri wa kuchukua maamuzi magumu kama wazee wao.
  Duh kumbe kijana kama Lusinde anawakilisha aina ya vijana wanaopendwa huko CCM? Sasa hao wengine kwani wamefungwa minyororo hadi hawawezi kujikomboa. Kwa nini wasihamie huko kuliko na uhuru zaidi wa kusema ukweli na kujenga hoja nzito au njaa yao ndio minyororo yenyewe?
  Unabadilikabadilika, kwani umekuwa kinyonga? Mimi wala sijiulizi uko chama gani kwa sababu maneno na matendo yako yanakuumbua. Kama ulipoishia ni sehemu ya kwanza, sidhani katika sehemu ya pili utaweza kuleta jipya, kaniki rangi yake hata ukiifua kwa OMO.
  Hapa ndio umeharibu kabisa, katika hizi harakati za kujikomboa kuondokana na udhalimu wa utawala huu tulio nao, kushindwa kujipambanua uko upande upi ni udhaifu mkubwa. Lakini maadamu unajitambulisha kwa tabia kama za kinyonga ni rahisi kujua wewe ni mtu wa namna gani. Ni watu kama wewe wanaoipa CCM (na kijana Nape?) ujasiri wa kudai itatawala kwa miaka 100, it's so sad!
   
 17. L

  Liarin New Member

  #17
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli bwana kombe hawa wameshiwa na sera
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Haihitaji utafiti kuyajua haya.
   
 19. Luse msomba

  Luse msomba JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  watu wanataka changes. uoga wetu kufanya mabadiliko umetufikisha pabaya tulipo
   
Loading...