Kilema cha Kuona Kilichopelea

Kilema cha Kuona Kilichopelea

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
919
Reaction score
794
Kuna wale wakaguzi wa kilichopelea. Kwa kila simulizi wanakuja na ushahidi wa kile ulichokisahau:

‘Jamaa ni mtu mwema sana. Napenda anavyojiongeza akisikia shida ya mtu’—ndio lakini ana tatizo hili usilolojua ngojea nikwambie.

‘Shule zikifunguliwa nampeleka mwanangu shule X’—ile shule nzuri lakini mwanangu ilimshinda. Kuna hiki na kile kwenye ile shule. Sikushauri umpeleke mtoto pale.

‘Nina wazo la kufungua biashara/kuanza kulima’—mamama utaweza kweli? Hiyo biashara (hicho kilimo) nilishajaribu sana. Hutoweza.

‘Mwezi ujao naoa nahitaji maombi yako ninapoanza maisha mapya’—umesikia takwimu lakini? Asilimia 20 ya wanaooa wanaachana ndani ya mwaka mmoja. Umechoka kuishi kwa amani ndugu yangu?

‘Kwenye hili tunalozungumzia, tatizo ninaloliona zaidi ni ABC’—sawa sawa lakini umesahau D.

‘Jamaa ni mzungumzaji nzuri. Kajenga hoja vizuri sana na nimependa’—ndio anaongea vizuri lakini hajatazama jambo hili kwa mtazamo mpana. Kuna marekebisho akifanya atakuwa mzuri zaidi.

Kilema cha kukamilisha. Kilema cha kuona kilichopelea. Kuna muda inatosha kusikiliza zaidi kuliko kutafuta mapungufu. Ukiwa msikilizaji mzuri kuna namna unapunguza macho yanayoona kilichobakia.
 
😆😆😆 Kuna vitu viwili tofauti hapa
1) Negative mindset. Hawa kwenye Kila kitu wanaonaga negative side. Yaani ubongo wao umekaa kujihami na hatari muda wote mostly kutoka na na experience mbaya huko nyuma.
2) Fault finders. Hawa ni wale wako positive lakini wanaona mapungufu ambayo wengine hawawezi kuona. So ukipresent issue Yako hataipinga, ila atakuonyesha mapungufu yaliyopo na kukupa suggestions za namna ya kuboresha.

Natamani kungekuwa na commenting ya voice nizielezee zaidi, ila kiufupi nimeupenda huu Uzi maana nimeresearch sana hivi tu.
 
Shukrani sana 😁
 
Back
Top Bottom