Kile kiupepo cha kwenye ugali

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
26,596
Reaction score
29,531
Ni tukio ambalo mpaka sasa siamini amini hadi imenipelekea kula ugali wangu kwa mkono wa kushoto maana kilichonitokea sijui ni uzembe wangu au kutokujua au ni kujisahau

ipo likizo kidogo kikazi sasa jana baada ya kushinda hapa home kukawa hamna mtu nikabaki mwenyewe imefika mchana hivi nikawa nafikiria nile nini wazo likanijia jikoko kuna unga kwenye ndoo na jiko gass imejaa

Nikaenda dukani nje fasta nikanunua maziwa ya pakti (yale ya tanga) basi mi nikawasha jiko nikatia maji kwenye sufuria yalipochemka nikalirusha (kusonga ugali) sasa si nikasakafia pale juu?

Sasa ule ugali pale pembeni pakawa panapuliza mbaya kiupepo hata kile cha pale ubungo songas hakioni mi si nikajifanya kama naweka mkono pale juu ya kile kiupepo kama kugadi fulani kwa kweli nimeungua sana hadi nimeahindwa kusokota tonge nikala na mkono wa kushoto.

Hili tukio nitakuja kuwasimulia watoto wangu huko baadae.
 
Pole sana Mkuu.
Nikifikiria kaupepo kenyewe kamejitokeza kwa ukali wa moto wa Gesi...!!

Sipatii jibu Makali yake...[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana Mkuu.
Nikifikiria kaupepo kenyewe kamejitokeza kwa ukali wa moto wa Gesi...!!

Sipatii jibu Makali yake...[emoji23][emoji23][emoji23]
Ndo maana nikasema ule wa pale kwenye mitambo ya songas hauoni ndani
 
Kile kiupepo ni ishara kwamba ugali umeiva tayari..
Wanawake kila siku tunapika ugali na bahati mbaya kinatuunguza but yupo kimya. mwanaume Mara moja tu unalia hadi unakula na mkono wa kushoto..kweli kazi ipo!
Mi niliuweka kabisa kama nakizuia nyie kinawa pepesa bana
 
Uzi tayari...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ha ha ha,
Umenikumbusha Mwanamuziki mmoja aliewahi kutamba miaka ya nyuma akiitwa Kanda Bongo Man. Huyu bana alikua bingwa Sana wa kucheza. Lakini wachezaji hawakua na hela kuliko waimbaji, so nae akaamua kua muimbaji.

Katika waimbaji matapeli huyu alitisha aisee. Ataizungumzia Lilongwe, ataitaja taja Lilongwe weeeee, mbeleni ataacha na kuanza kucheza, tayari hapo ni wimbo.

Atakuja atamtaja taja Yolanda weeee, mbeleni huko akicheza yeye, wimbo mwengine tayari.

Atakuja kukuambia Inde morning. Atairudia rudia weeeee, akija kucheza kuanzia katikati ya wimbo, tayari wimbo mwengine.

Mara aseme Isambe, hata Sijui ni nini. Ataitaja taja hiyo isambe karibia nusu wimbo mzima, nusu iliyobaki akicheza yeye ni wimbo mwengine tayari.

Kuja kushtuka ana album tayari, anauza na tours anafanya. Watu hawajui hata anaimba nini, wanachotaka ni kumuona akicheza tu. Baadhi ya nchi zilishtukia huu utapeli zikampiga marufuku kufanya tours nchini mwao.
 
Nimecheka kwa sauti ya juuuu....
 
Wapo wengi sana mjomba, hata Mimi nilikuwa na mawazo kama yako ila nikaja kugundua ndoa ni zaidi ya tunavyovihitaji kwa maana ya mwanamke mzuri,msomi,good sex,tabia nzuri n.k

Ndoa ni hatua nyingine ya maisha haijalishi ni katika kiwango gani maadamu ukubaliane na mwanamke yeyote na msahau historia zenu

Ndoa ina raha yake na karaha zake , we call them changamoto
Wanawake wa kuoa siwaoni hata
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aiseee ipo siku tutaleta mambo ya sirini humu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu popote ulipo ule usimibwako wa kuvuta sirini umejionyesha huku
 
We msikilize tu,
Nusu ya kwanza anazuga zuga tu kwa kutaja taja kitu hicho hicho. Anakirudia weeee kupitisha muda akisubir muda wake ufike, nusu ya pili anaweka mic chini na kuanza kucheza sasa, mwisho wa siku ni wimbo tayari.

Ha haa..Sikuwahi kujua hili.. Nimemaliza kuisikiliza Isambe naona ni kweli .. na inde monii nayo lol!! .. kweli jamaa ndo zilikua zake!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…