habari yako.. mkuu..![emoji120]
mahusiano kwa ujumla (kabla na baada ya ndoa) huwa yana changamoto zinazofanana,
ingawa kwenye ndoa huwa kuna kitu cha ziada kinachofanya wewe uhisi huwa kuna shetani anaingilia kati.
Kitu kinachoifanya ndoa iwe kitu Special,
ndoa ni FAMILIA
ni mahusiano ambayo yanawafanya wenye ndoa waanze kuishi maisha yenye MSINGI MAALUMU tofauti na maisha waliokuwa wanayaishi hapo kabla,
ni mahusiano ambayo SIO YA SIRI tena..
Usiseme ndoa sio Ishu tena siku hizi..
Sema wanandoa ndio sio Ishu siku hizi..
Matatizo ya kwenye ndoa hayaanzii kwenye ndoa.. huwa yanaandaliwa na wanandoa pasipo wao kujua..
Walio wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa na SABABU ambazo sio za msingi kabisa.. wengi wao HUSHINIKIZWA bila wao kujua..
Pia wengi wao wanaingia kwenye ndoa bila kujua WAJIBU wao katika ndoa..sasa baada ya ndoa ndio anaanza kujifunza..
NDOA NI NZURI MKUU...
ILA SIO KILA MWANAMKE ANAFAA KUWA MKE
NA
SIO KILA MWANAUME ANAFAA KUWA MUME
Mbona ndoa zenyewe siku hizi siyo issue kivile? siyo lazima kuoa wala kuolewa, ni kwavile tu wengi waliopo nje ya uwanja wanatamani kuingia uwanjani lakini ukweli usiosemwa na wanandoa wengi ni kwamba wanaofurahia maisha ya ndoa ni wachache sana tena for my opinion sidhani kama wanaweza kuzidi 20%
hakuna watu wanaoenjey kama ambao wapo tu kwenye mahusiano, sijui baada ya ndoa huwa anaingia shetani gani?