Kile kinachoitwa mwanamke kuzaa nje ya ndoa…..

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
Hivi sasa katika jamii yetu kuna
kundi la wanawake ambao wana
watoto lakini hawajaolewa lakini
pia lipo kundi kubwa la wanawake
ambao wako kwenye ndoa au
mahusiano kwa muda mrefu lakini
hawana watoto, hawa wamekuwa ni
wahanga wa kubwa wa makanisa
na hizi kliniki za tiba mbadala
zilizosheheni hapa nchini zikidai
kwamba zinasaidia wanawake
kupata watoto.

Kundi hili la wanawake ambao
hawajajaaliwa kupata watoto
kwenye ndoa zao wamejikuta
wakipoteza fedha nyingi sana ili
kupata watoto.

Dunia yetu imebadilika, mitindo ya
maisha nayo imebadiliaka, mila
desturi zetu nazo zimebadilika pia.

Zamani vijana walikuwa
wanalazimishwa na wazazi kuoa
mapema na kama kijana akifikisha
umri fulani hajaoa alikuwa
anaonekana mtu wa ajabu tofauti
na siku hizi shinikizo la vijana
kuoa halipo tena kama zamani
vijana wanawajibika kuamua
wenyewe ni wakati gani waoe kwa
sababu hata hivyo huduma ya
ngono inapatikana hovyo.

Kwa upande wa wanawake nao
shinikizo limebaki kwao, kwa kadiri
umri unavyosonga ndivyo wazazi,
jamii iliyomzunguka inavyozidi
kumpa shinikizo la kuhoji kwa nini
haolewi huku wanaume wakizidi
kubaki huru na maamuzi yao.

Kwa wale ambao waliamua kuzaa
kabla ya ndoa iwe ni kwa bahati
mbaya au kwa kukusudia ambao
wamebaki kuwa na watoto kabla ya
ndoa wanao mtihani mwingine wa
kupata wenza.

Wanaume wengi
wanashikwa na kigugumizi cha
kuoa wanawake waliokwisha kuzaa.

Lakini wanaume hao hao unaweza
kukuta nao wana watoto
waliowazaa nje ya ndoa
wakawatelekeza kwa mama zao.

Hapo ndipo ilipo hadithi ya kuku na
kifaranga haijulikani kipi ni kipi.
Bila shaka wengi wetu
tumeshakutana na wanawake
wenye kutafuta watoto wakiwa
tayari umri umeshawatupa mkono.

Ukweli ni kwamba, umri wa kupata
watoto kwa wanawake umepungua
sana tofauti na zamani.

Hivi sasa kutokana na mtindo wa
maisha na vyakula tunavyokula
watoto wa kike wanavunja ungo
mapema hivyo wanaanza kushiriki
ngono mapema, na hivyo kutokana
na utoaji wa mimba holela au
kutumia vidonge vya kuzuia mimba
mapema wengi wamejikuta
wakikosa uzazi pale wanapokata
shauri ya kutafuta watoto.

Lakini
pia maradhi ya ngono yaliyoachwa
kwa muda mrefu kabla ya kutibiwa
yameathiri via vya uzazi vya
wasichana wengi na hivyo kupoteza
uwezo wa kuzaa

Lakini pia vyakula tunavyokula na
madawa tunayotumia yanayotibu
maradhi mbalimbali nayo yana
mchango katika tatizo hilo.

Sasa basi labda changamoto tuliyo
nayo kwa sasa ni je kuna haja kweli
kwa wanawake kuwa na ulazima
wa kusubiri mpaka kufunga ndoa
ndipo wapate watoto au wanaweza
kupata watoto kabla ya ndoa
kutokana na kuepuka umri
kuwatupa mkono na kupoteza
kabisa uwezo wa kuzaa.

Je jamii inawachukuliaje wanawake
wenye watoto kabla ya ndao? Je
hawastahili kuolewa?
 
Dhaaaa nmekumbuka,shair flan hiv la class 4_5 ,,,kitambo hyo 2005


Anyway kuoa mwamke mwemy mtt n janga kubwa na kuoa mwanamke ambae hujamjaza ukaona tumbo pia n ttz

Sasa cjui tutapitia wap na kutokea wap
 
Kujibu swali....

Jamii jinsi inavyowachukulia wanawake waliozaa kabla ya ndoa inategemea na ustaarabu kati ya jamii na jamii..



Na wanawake ambao wanawatoto wanastahili ndoa pia.
Kama vile wanaume wenye watoto kablanya ndoa


Maisha ni mafupi.... msiyacomplicate bila sababu za msingi wala sekondari...

Mwisho kabisa...kuoa/kuolewa sio mwisho wa maisha na wala sio kuyapatia maisha
 
Kujibu swali....

Jamii jinsi inavyowachukulia wanawake waliozaa kabla ya ndoa inategemea na ustaarabu kati ya jamii na jamii..



Na wanawake ambao wanawatoto wanastahili ndoa pia.
Kama vile wanaume wenye watoto kablanya ndoa


Maisha ni mafupi.... msiyacomplicate bila sababu za msingi wala sekondari...

Mwisho kabisa...kuoa/kuolewa sio mwisho wa maisha na wala sio kuyapatia maisha
Mwanamke akikutwa na watoto wa Baba mwingine Atadhalauliwa sana

Ila mwanaume akikutwa na watoto Mara nyingi Hakuna shida Hapo
 
Mbona ndoa zenyewe siku hizi siyo issue kivile? siyo lazima kuoa wala kuolewa, ni kwavile tu wengi waliopo nje ya uwanja wanatamani kuingia uwanjani lakini ukweli usiosemwa na wanandoa wengi ni kwamba wanaofurahia maisha ya ndoa ni wachache sana tena for my opinion sidhani kama wanaweza kuzidi 20%

hakuna watu wanaoenjey kama ambao wapo tu kwenye mahusiano, sijui baada ya ndoa huwa anaingia shetani gani?
 
Mbona ndoa zenyewe siku hizi siyo issue kivile? siyo lazima kuoa wala kuolewa, ni kwavile tu wengi waliopo nje ya uwanja wanatamani kuingia uwanjani lakini ukweli usiosemwa na wanandoa wengi ni kwamba wanaofurahia maisha ya ndoa ni wachache sana tena for my opinion sidhani kama wanaweza kuzidi 20%

hakuna watu wanaoenjey kama ambao wapo tu kwenye mahusiano, sijui baada ya ndoa huwa anaingia shetani gani?
Hayo mambo ya kuchukuana Kienyeji sio mazur
 
Mi nimesena Hakuna shida

Yan nikute engen imeshushwa

Hapana kwa kweri
Tunarudi palepale.....

Mtazamo wako...ambao unabebwa na makuzi uliyotoka.

Wakati wewe hutaki mwenye mtoto kuna wengine wanawasaka....kuna wengine they don't care...anachoangalia kupendwa kuheshimiwa kuthaminiwa nk

Usioe/olewa kwa sababu amezaa au hajazaa.....oa kwa kuwa kuna upendo kusikilizana kuheshimiana...kuthaminiana....kuaminiana
 
Wanaume walio wengi huwakwepa wanawake walio kwisha kuzaa kwa hisia totauti nawengi uhofia kwa kuzani pengine hata akiamua kuishi nae anawezakua bado atakuwa na mahusino nahuyo mzazi mwenzi
 
Point tosha hii

Wenyewe wanasema

Bass Tujikumbushie
akili za kitoto hizi, mwanamke anayejiheshimu hawezi kufanya huo upuuzi. hizi ni mbwembwe za ujana zinawasumbuwa tu ngoja ufike miaka 50 huko na umefiwa na mke tuone kama utakuja kubana puwa hapa eti siwezi kuowa mwanamke aliyezaa, itafika hata huyo aliyezaa anakukataa.
 
Back
Top Bottom