Kilango: Mafisadi walitusumbua


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
23
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 23 135
MBUNGE mteule wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, amesema miongoni mwa mambo yaliyompa faraja kwenye uchaguzi wa mwaka huu ni kurejea bungeni kwa wabunge wa CCM ambao ni makamanda wa vita ya ufisadi.

Kilango ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alisema makamanda hao wa ufisadi walikabiliana na nguvu kubwa ya fedha kutoka mtandao wa mafisadi, lakini mwisho haki imeshinda.

Ingawa Kilango hakutaka kufafanua njia zilizotumiwa na mtandao huo wa mafisadi kuandama wapambanaji wa ufisadi, alisema anaamini kurejea kwao bungeni ni kielelezo cha kuungwa mkono na wananchi.
“Uchaguzi huu ulikuwa mgumu kiasi fulani hasa kwetu sisi tuliokuwa mstari wa mbele kupambana na mafisadi, kwa sababu nguvu zao za fedha walijaribu kuzipenyeza kwenye majimbo yetu lakini wakakwaa kisiki,” alisema.

Kilango ambaye ni mshindi wa tuzo ya mwanamke jasiri 2009 inayotolewa na Ubalozi wa Marekani, alisema japokuwa zipo kasoro zilizotokana na mchakato wa kura za maoni, lakini hoja za ufisadi ziliwasumbua baadhi ya wabunge.

Wabunge wanaotajwa walikuwa vinara wa vita ya ufisadi katika Bunge lililopita lililoshuhudia aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, akiwajibika kwa kujiuzulu ni pamoja na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

Lowassa alilazimika kujiuzulu wadhifa wake huo baada ya kuhusishwa na kashfa ya Kampuni ya kufua umeme wa dharura Richmond Development LC, uamuzi ambao ulimfanya Rais kuvunja Baraza la Mawaziri na kuunda jipya.
Sitta ambaye aliwahi kuomba kuongezewa ulinzi kutokana na kusakamwa na mafisadi, aliwania ubunge Jimbo la Urambo Mashariki na kuibuka na ushindi wa kura 19,947 huku mpinzani wake akiambulia 5,134.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa au kuunga mkono ufisadi, wamejikuta wakipata ushindi wa kati ya asilimia 50 na 55 hali inayotafsiriwa kuwa kukubalika kwao kumepungua.

Kigogo mmoja wa CCM ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema CCM ipende isipende, ajenda ya ufisadi ndio iliyofanya wabunge wengi kupoteza ubunge.
“Hata kama mgombea urais wa Chadema, Dk Wibroad Slaa, hatashinda lakini ujumbe umefika kwa serikali ya CCM kuwa inahitaji kukunjua makucha yake kwa mafisadi, vinginevyo 2015 hapatatosha,” alidai.
Kigogo huyo alisema serikali ya CCM inapaswa isirudie kosa kubwa ililofanya hasa kwa mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete, kuwanadi watuhumiwa wa ufisadi majimboni.

Wabunge wapambanaji wa ufisadi waliorejea na majimbo yao kwenye mabano ni Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Dk Harrison Mwakyembe (Kyela) na Victor Mwambalaswa (Lupa).
Wengine katika orodha hiyo ni Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki), Beatrice Shelukindo (Kilindi) na James Lembeli (Kahama) ambao wanatarajiwa kuendeleza vita yao katika bunge lijalo.
 
N

nina90

Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
38
Likes
0
Points
0
N

nina90

Member
Joined Oct 21, 2010
38 0 0
Una maana ya wabunge wa chama hicho hicho ambacho kimekumbatia mafisadi? au una maana ya wabunge waliorudi bungeni kwa gharama ya fedha hizo hizo ya mafisadi? au pengine unaongelea wabunge wanaopiga kelele sambamba na wabunge wenzao ambao wanatuhumiwa na ufisadi? na ni sera zipi zinazoongoza chama hicho? zinazopinga au zinazokumbatia?
 

Forum statistics

Threads 1,237,986
Members 475,809
Posts 29,308,910