Kilango asema hana Ugomvi na Lowassa

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Kilango amfagilia Lowassa

Asema hana sababu za kumchukia
Aonya kuna propaganda chafu
Alonga hajawahi kuchangia Monduli
Asisitiza hawezi kuvamia jimbo hilo.

Na Hamis Mkotya
MBUNGE wa Same Mashariki,Anne Kilango Malecela(CCM).amevujna ukimya na kueleza hisia zake za kuhusiana na Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa.katika mazungumzo kwa njia ya simu na gazeti hili jana.Kilango aliyeko mkoani Kilimanjaro kwa sasa, alisema kwazi kuwa hana ugomvi wala kinyongo chochote na kiongozi huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu.

Kilango anayetajwa kuwa mmoja wa wabunge waliojipambanua kama wapinga ufisadi, alisema hana sababu yoyote ya kumchukia Lowass, iwe kwa sababu za siasa au nyinginezo.

Kauli hiyo imekuja takribani wiki moja tu baada ya gazeti moja la kila siku (si MTANZANIA), kuchapisha habari kwamba wabunge hao, akiwamo kilango, wamejiwekea mkakati wa kuhakikisha Lowassa haruki bungeni katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

Katika taarifa hiyo, wabunge hao walitangazwa kushiriki katika harambee ya kuchangia watoto yatima wa Monduli juu, ingawa wenyewe hawakwenda huko.

Harambee hiyo iliyotafsiriwa kama uvamizi wa akina Kilango katika jimbo la Monduli, ilikusanya karibu sh. 10,000,000 huku Kilango, na wabunge wenzake Dk. Harrison Mwakyembe, na chiristopher ole Sendeka Lucas selelii, James Lembeli wakiongozwa minongi mwa wachangiaji wakubwa.

Ilidaiwa mtu mmoja ambaye hakutajwa jina ndiye aliyetoa fedha kwa niaba ya wabunge hao, ikiaminiwa kuwa walimpa fedha hizo au walitoa baraka ya kutoa fedha.

Tangu msiba ule utokee (Maporomoko yam lima huko same yaliyouawatu 24) na kuua watu wangu, sijatoka kwenda popote hii (ya Kilimanjaro ) ndiyo zira yangu ya kwanza na nimekuja huku kama mjumbe wa Halimashauri kuu ya chama cha Mapinduzi(NEC – CCM) sikuja kama mbunge” alisema.

Mimi sikui hata hiyo monduli yenyewe iko wapi. Hizo ni Propaganda ambazo hat sikui msingi wake ninini. Kama huyo mtu (aliyetoa fedha) yupo, kwa nini asiniletee huku akazipeleke Monduli? Kwanza nitoe mchango kwa ajili ya nini?

Alisema yeye ana shida ya fedha kwa ajili ya misaada jimboni kwake kwa hiyo asingeweza kutoa fedha kwa ajili ya kumsadidia mtu mwingine akachukue jimbo jingine.

Hivi nitakuwa na akili kweli? Wamuogope mungu, siwezi kumchangia mtu mwingine fedha wakati kwangu kunaungua.

Hizo taarifa ni za uongo, mimi na Lowassa wote ni wabunge wa CCM, sina sababu ya kufanya mikakati michafu dhidi yake. Hivi katika akili ya kawaida, nikuulize,sh. 500,000 zinaweza kumtoa Lowassa? Hizo ni propanganda tu, kuna watu wanaopenda kuona wenzao wakigombana mimi sina ugombi na Lowassa na hata yeye anajua.

Tunaogeza vizuri na tukikutana tunasalimiana. Sina sababu ya kwenda kumchafua jimboni kwake kama ambavyo yeye hana sababu ya kuja kunichafua jimboni kwangu” alisema kwa utuluvu mama Kilango.

Akizungumzia mkakati anaotangazwa kuwa kuna watu wameingiza fedha jimboni kwake kuhakikisha naye haruki bungeni mwakani mamwa kilango alisema:

Hata hizi taarifa za kwamba kuna mafisadi sijui watu gani wamejipanga kuhakikisha sirudi bungeni ni uono mbona sijaona mtu yeyote jimboni kwangu? Ni wananchi wa same walionipa ubunge na ndio watakaoamua kunirudisha bungeni au hapana.

Alisema kwa kuwa jimbo la same si miliki yake binafsi yuko tayari kuwakaribisha washindane wakati ukiwfika hivyo ni mara ya kwanza kwa mbunge huyo kuzungumza hadharani hisia zake nje ya bune, kumhusu Lowassa .

Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango Malecela(CCM),amfagilia Lowassa asema hana sababu za kumchukia,aonya kuna propaganda chafu,Alonga hajawi kuchangia Monduli,asisitiza hawezi kuvamia jimbo hilo.Katika mazungumzo kwa njia ya simu na gazeti la Mtanzania Kilango aliyeko Kilimanjaro kwa sasa alisema wazi kuwa hana ugomvi wala kinyongo chochote na kiongozi huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu.
Wakuu je mnalionaje hili,hii imekaaje?
 
kama ni kweli basi huyu mama anatakiwa akapimwe akili and i started getting the feeling that what Sofia Simba said holds water
 
hiyo habari haijatulia kama iko kwenye gazeti post it here watu wasoma wachangie. Kwani haiko straight kamfagilia katika lipi!!!!
 
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango Malecela(CCM),amfagilia Lowassa asema hana sababu za kumchukia,aonya kuna propaganda chafu,Alonga hajawi kuchangia Monduli,asisitiza hawezi kuvamia jimbo hilo.Katika mazungumzo kwa njia ya simu na gazeti la Mtanzania Kilango aliyeko Kilimanjaro kwa sasa alisema wazi kuwa hana ugomvi wala kinyongo chochote na kiongozi huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu.
Wakuu je mnalionaje hili,hii imekaaje?

Sijaona alipomfagilia, sanasana amesema hawezi kuvamia monduli (which is true), na kutokumchukia au kutokuwa na kinyongo mtu sio kumfagilia, angemsifia labda ndio ingekuwa hivyo, na ni kweli ameonya propaganda chafu (ambayo ndio mtanzania wanaandika kama hilo neno kufagilia)

BTW, source yake ni MTANZANIA, gazeti linalosimamiwa na haohao...
 
Mama Kilango naye awe anapima maneno anayoongea, anaropoka sana huyu mama yetu matamshi yake yanaweza kutafsiriwa vibaya na ikamharibia. Mambo ya kutokuwa na chuki ama kinyongo ayaweke moyoni mwake kuna haja gani ya kuyatamka hadharani unless anataka kujipendekeza kwa Lowassa! Na kwa nini awe na mawazo ya 'kuvamia' majimbo ya wengine wakati lake analo? Si awaache wanaowania kugombea kwenye majimbo hayo wao wenyewe ndio waseme ama wavalie njuga mapambano kwenye majimbo husika? Je ni background yake inafanya awe hivyo?
 
Nazani wanaosema mama kilango anaropoka na apime anayosema wanakuwa na upeo mdogo mno, mama kilango alichosema ni kwamba hana kinyongo na EL na that doesnt mean amemfagilia
 
Mama Kilango naye awe anapima maneno anayoongea, anaropoka sana huyu mama yetu matamshi yake yanaweza kutafsiriwa vibaya na ikamharibia. Mambo ya kutokuwa na chuki ama kinyongo ayaweke moyoni mwake kuna haja gani ya kuyatamka hadharani unless anataka kujipendekeza kwa Lowassa! Na kwa nini awe na mawazo ya 'kuvamia' majimbo ya wengine wakati lake analo? Si awaache wanaowania kugombea kwenye majimbo hayo wao wenyewe ndio waseme ama wavalie njuga mapambano kwenye majimbo husika? Je ni background yake inafanya awe hivyo?

sijakupata mkuu,
ungekuwa wewe ungejibu vipi maswali ya huyo mwandishi?, halafu hili la kuvamia jimbo nalo naona kama umeniacha, kavamia wapi?... kumbuka anatekeleza agenda ya chama chake sasa huu uvamizi ni upi?
 
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango Malecela(CCM),amfagilia Lowassa asema hana sababu za kumchukia,aonya kuna propaganda chafu,Alonga hajawi kuchangia Monduli,asisitiza hawezi kuvamia jimbo hilo.Katika mazungumzo kwa njia ya simu na gazeti la Mtanzania Kilango aliyeko Kilimanjaro kwa sasa alisema wazi kuwa hana ugomvi wala kinyongo chochote na kiongozi huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu.
Wakuu je mnalionaje hili,hii imekaaje?
Mtanzania nalo gazeti? uhh
 
Nimesoma habari yote sijaona mahali mama A Kilango alipomsifia Lowassa.Mama Kilango kama mwanasiasa amejibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari.Kukanusha kwamba hajatoa mchango ndio kumfagilia au wanajamvi mnataka kuingia kwenye mtego wa waandishi wa habari uchwara.Kichwa cha habari ni tofauti na habari yenyewe tuwe makini na haya magazeti yasiyozingatia miiko ya uandishi wa habari.
mna kazi! sasa hivi watu wanaangalia kwa umakini kwani your next president ni EL..
Hapana mkuu huyu hawezi kuwa Rais wa Tanzania pamoja na mikakati ya kumsafisha ndio kwanza anazidi kuchafuka.

Duhhh..tutajuta.maana anaweza akaomba details zetu hapa JF na akaanza ku deal na wote tuliokuwa tunampiga mawe

Hatuwezi kujuta hata kidogo mkuu mawe tuliyokuwa tunamrushia na tunayoendelea kumrushia ni matokeo ya ufisadi alioshiriki na kuratibu yeye mwenyewe, hana wa kumlaumu bali nafsi yake kwa kupenda utajiri wa haraka haraka bila kujali maisha ya watanzania wengi maskini.
 
Lakini huyu Mama Kwenye kikao cha bunge, siku EL anajiuzulu alitoa maneno makali juu ya EL na wenzake, sasa sijui kinachomrudisha nyuma ni nini tena.
 
kama ni kweli basi huyu mama anatakiwa akapimwe akili and i started getting the feeling that what sofia simba said holds water
kumbe na mama kilango apelekwe mirembe ha ha ha ha ha ha ha!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom