Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 401
Wakuu,
Tukio la kishujaa la wabunge wa chadema kususia hotuba ya jk jana bungeni limekuwa na mwitikio tofauti miongoni mwa wananchi mitaani. Katika pitapita yangu mitaani nimegundua kuwa wananchi wengi wanaunga mkono hatua hiyo ya chadema. Lakini humu ndani ya JF kuna watu wameanza ku-argue kisomi kwamba kisheria chadema hawajaonyesha consistency ya kile wanachosusia. Kwamba hawawezi kutomtambua rais wakati huohuo walipiga kura ya kupinga au kuunga mkono uteuzi wa rais wa waziri mkuu wake. Wengine wameeleza kuwa je chadema watasusia hata kujadili hotuba za bajeti za mawaziri ambao ni wa jk??
Mimi binafsi sidhani hicho ndicho wanacholenga kufanya chadema. Kwa kuangalia sheria yetu kandamizi ya uchaguzi, chadema wameridhika kuwa hawawezi kupeleka malalamiko yao kwenye chombo cha haki yaani mahakama. Sheria imeipatia NEC nguvu ya kimungu kwamba ikitamka rasmi kuwa fulani ndiye mshindi basi hakuna wa kupinga. Hivyo, chadema ni wanyonge mbele ya sheria hiyo kandamizi na silaha yao pekee ya kuonyesha hisia yao ni kutomtambua rais aliyepo madarakani. Kwa maana hiyo, chadema hawana haja ya kuzingatia sana hicho kinachoitwa 'consistency'. Badala yake wanaweza wakaamua tu kwamba kila tukio ambalo wana uhakika jk atahudhuria, wao nao wanafika mapema, then, jk akifika wanaondoka kwa pamoja kuonyesha kuwa hawamtambui. Hii ni njia inayotosha kabisa kupeleka ujumbe kwa wahusika.
Shime chadema, endeleeni na msimamo huohuo. Tupo pamoja sana.