Kila tukio ambalo kikwete ni mgeni rasmi chadema hudhurieni akifika ondokeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila tukio ambalo kikwete ni mgeni rasmi chadema hudhurieni akifika ondokeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Nov 19, 2010.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Tukio la kishujaa la wabunge wa chadema kususia hotuba ya jk jana bungeni limekuwa na mwitikio tofauti miongoni mwa wananchi mitaani. Katika pitapita yangu mitaani nimegundua kuwa wananchi wengi wanaunga mkono hatua hiyo ya chadema. Lakini humu ndani ya JF kuna watu wameanza ku-argue kisomi kwamba kisheria chadema hawajaonyesha consistency ya kile wanachosusia. Kwamba hawawezi kutomtambua rais wakati huohuo walipiga kura ya kupinga au kuunga mkono uteuzi wa rais wa waziri mkuu wake. Wengine wameeleza kuwa je chadema watasusia hata kujadili hotuba za bajeti za mawaziri ambao ni wa jk??

  Mimi binafsi sidhani hicho ndicho wanacholenga kufanya chadema. Kwa kuangalia sheria yetu kandamizi ya uchaguzi, chadema wameridhika kuwa hawawezi kupeleka malalamiko yao kwenye chombo cha haki yaani mahakama. Sheria imeipatia NEC nguvu ya kimungu kwamba ikitamka rasmi kuwa fulani ndiye mshindi basi hakuna wa kupinga. Hivyo, chadema ni wanyonge mbele ya sheria hiyo kandamizi na silaha yao pekee ya kuonyesha hisia yao ni kutomtambua rais aliyepo madarakani. Kwa maana hiyo, chadema hawana haja ya kuzingatia sana hicho kinachoitwa 'consistency'. Badala yake wanaweza wakaamua tu kwamba kila tukio ambalo wana uhakika jk atahudhuria, wao nao wanafika mapema, then, jk akifika wanaondoka kwa pamoja kuonyesha kuwa hawamtambui. Hii ni njia inayotosha kabisa kupeleka ujumbe kwa wahusika.

  Shime chadema, endeleeni na msimamo huohuo. Tupo pamoja sana.
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  They have to calculate the risks. Kwa mfano kukiwa na misiba ya kitaifa?
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Busara itatumika tu, shida ipo wapi!! Kwa viongozi makini lazima wataguswa sana na mwenendo huo wa chadema. Wa kwanza anayeonekana dhahiri ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda tangu wakati wa kikao cha bunge kilichokaa kupitisha uteuzi wake ambapo alikuwa na uhakika kuwa wabunge wa chadema wote hawakuunga mkono na wakati wa kutangaza matokeo hawakupiga makofi. Aliposimama, kuwashukuru wabunge alizungumzia jambo hilo. Tukio la pili ni kwenye sherehe ya kuapishwa ambapo chadema waliandaliwa sehemu ya kukaa lakini hawakuhudhuria. Hiyo ndiyo silaha pekee waliyo nayo chadema.
   
 4. n

  nyangwe Senior Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanajamvi mi naunga mkono kitendo wabunge wa CHADEMA kutoka bungeni.mi nawashangaa wanaokosoa,nadhani wanatakiwa kusoma history ya namna jamii mbalimbali duniani zilivyo jikomboa kutoka katika tawala gadamizi zilizojitengenea katiba kwa manufaa yao. ''shallow understanding of people of good will is more frustrating than absolute misunderstanding of people of evil will''
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  KAMA NI WA KIKWETE, RIGHIWANI, LOWASSA, ROSTAM and the alikes nawashauri wasikose hata nukta moja...MWANZO MWISHO.

  HII HATA MIMI NITAHUDHURIA KWA MOYO MKUNJUFU KABISA NA MACHOZI KIBAO
   
Loading...