Kila taifa imara lina nguzo zake za kiroho

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,417
9,805
Kila taifa imara duniani lina nguzo za kiroho. Wachina wana confucianism, wajapan wana shintoism, Urusi wana orthodox church, Ueropeans wana christianity, wayaudi wana judaism, wahindi wana hinduism n.k . Kama Afrika tunataka kujikomboa basi tuangalie nyuma na tujiunganishe na nguzo zetu za kiroho.

Ukristo hauwezi kuwa nguzo yetu ya kiroho ni mambo ya Europeans na uislamu pia vile vile. Kuazima nguvu kunakufanya uwe dhaifu mbele ya sponsor wako. Najua muafrika unaona aibu kufata utamaduni wako kwa sababu ushapandikizwa fikra kwamba ni imani potofu, mambo machafu na ujinga ndio maana unapigania kufuata tamaduni za watu weupe, pamoja na faida za haraka haraka utakazopata ila kwa kipindi kirefu wewe na kizazi chako mtaendelea kuwa eternal losers.

Jipe ujasiri wa kuzipiga chini imani zote za kigeni na uikumbatie imani ya utamaduni wako. Pamoja na presha zote za kijamii kumbatia utamaduni wako songa mbele. Utamaduni wako ni kama immune system ikishakua dhaifu hauwezi kukabaliana na shambulio lolote la maradhi na ndio sababu waliotuletea dini walipambana kuzialibu imani zetu za kitamaduni kwanza walijua baada ya hapo kazi ya kutufanya kuwa mazombi yao itakua rahisi.

Taasisi ya kanisa ni utapeli ivyo ivyo kwa misikiti pia. Nakuombea mizimu ya mababu zako iendelee kukulinda.
 
Back
Top Bottom