- Source #1
- View Source #1
Nyuki ni mkali lakini asali yake ni tamu.
Katika jamii inajulikana kuwa nyuki ni mkali lakini ukali wake huzidi zaidi unapomfata kwenye makazi yake, atakushambulia pia atakuacha na uvimbe pamoja na maumivu mwili mzima.
lakini kuna baadhi ya watu wanasema kuwa licha ya ukali wa nyuki lakini akikuuma baada ya saa 2 hufa.
Je, kuna ukweli wowote kuhusu hayo madai?
Katika jamii inajulikana kuwa nyuki ni mkali lakini ukali wake huzidi zaidi unapomfata kwenye makazi yake, atakushambulia pia atakuacha na uvimbe pamoja na maumivu mwili mzima.
lakini kuna baadhi ya watu wanasema kuwa licha ya ukali wa nyuki lakini akikuuma baada ya saa 2 hufa.
Je, kuna ukweli wowote kuhusu hayo madai?
- Tunachokijua
- Nyuki ni wadudu warukao wakiwa na spishi zaidi ya 20,000 wakiwa kwenye familia 7 ikiwemo ya nyuki wa asali (Apis) na nyuki aina ya bumblebee (Bombus). Nyuki wakubwa wanaweza kufikia hadi urefu wa sentimeta 4.
Madai
Kumekuwa na madai kwa dhana kuwa nyuki akikungata hupoteza maisha maada ya muda mfupi.
“Nyuki akikung’ata anakufa kwasababu ule mwiba aliokudunga nao unabakia kwenye mwili wako,na kawaida mwiba huo huwa umeunganishwa na utumbo wa nyuki hivyo akikung’ata hawezi kudumu zaidi ya saa mbili ni lazima atakufa” Kiliandika chanzo kimoja.
Uhalisia wa madai hayo ni upi.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa ni kweli Nyuki hufa baada kukung’ata lakini hii si kwa nyuki wote.
Chuo kikuu cha Sydney kinaeleza kuwa ni aina chache tu za nyuki tu ndio wanaoweza kuuma na kupoteza maisha huku asilimia 96.99 wenyewe hali hii haiwahuhusu na haiwatokei. Zaidi inabainisha kuwa ni spishi nane tu kati ya spishi zote ndiyo wanaokufa baada ya kuuma.
Kwanini baadhi ya Nyuki hufa baada ya kuuma?
Nyuki wanaotajwa kufa baada ya kumuuma binadamu ni nyuki wa asali wa Ulaya ambao wana mwiba wenye ndoano ambao hunasa kwenye ngozi. Anapojaribu kujinasua na kuondoka, mwiba huo pamoja na mfuko wake wa sumu hung'oka kutoka kwenye mwili wake. Hufa ndani ya dakika chache. Hali hii inawahusu nyuki wa asali pekee.
Kwanini Nyuki huuma?
Nyuki huuma wanapohisi kutishiwa, hasa ili kujilinda wenyewe au kundi lao. Katika matukio mengi, nyuki wa asali (Apis mellifera) ndio wanaohusika zaidi, kiasi kikubwa kutokana na asili yao ya kuishi kijamii na uhitaji wa kulinda mzinga wao.
Nyuki wafanyakazi ambao ndio pekee wenye uwezo wa kuuma hulinda kundi pale wanapohisi hatari. Hii inajumuisha vitisho dhidi ya mzinga wao, ambapo rasilimali muhimu kama vile asali na mabuu yanayokua huhifadhiwa.
Jambo la msingi ni kwamba, kuuma huwa ni hatua ya mwisho kabisa. Kabla ya kuchukua hatua hiyo, mara nyingi nyuki hujaribu kuzuia tishio kwa kuvuma kwa sauti kubwa au kuruka moja kwa moja kuelekea kwenye kile wanachokiona kama hatari.