Kila nionapo picha ya Rais Mstaafu Kikwete machozi yananitoka kwa uchungu

Yale yalikuwa maisha ya kibepari,
sasa tunarudi kwenye ujamaa wetu ulioachwa na hawa waswahili,
wananchi tujifunge mikanda..
 
Ukiwa kiongozi huwezi kujua ugumu wa maisha kwa sababu unaishi kwa kodi za walala hoi. Huwezi kuja kuniambia eti kiongozi wa nchi anafanya kazi kubwa kuliko baadhi ya watumishi , hili si kweli.

Watumishi wanateseka na familia zao, lakini viongozi walio madarakani wanapongezana na kufurahia maisha kwa kodi zetu.

Nitakukumbuka sana Dr. Mrisho Jakaya Kikwete, kwani licha ya kuongoza nchi ikiwa na watumishi hewa lakini uliweza kulinda maslahi ya watumishi. Leo hii machozi yananidondoka kwa uchungu pale ninapoona picha yako.

Kweli ulikuwa kiongozi mpenzi wa Mungu, mwenye huruma, mvumilivu, mpole, mwenye hekima na busara. Nakuombea kwa mwenyezi Mungu akupe afya na maisha marefu.

Nitakulilia maisha yangu yote, you are the hero!
We ni miongoni kwa wale mliokuwa mmezoea kukaa kijiweni na ofisi zenu za mfukoni, mkiulizwa mnasema eti mjini nipango. Zilipendwa hizo!!.. Hizi ni za Magufuli si za Jakaya.
 
Kwa kweli sijui hatma ya maisha ya kuwa mtumishi wa serikali. Hakuna nyongeza ya maana,hakuna kupanda vyeo sasa sijui wanafikiria nini hawa viongozi wetu wa juu?
Kama hakuna madili na mshahara hautoshi acha kazi, uone umuhimu wa kuwa na kazi.
 
  • Thanks
Reactions: 454
Back
Top Bottom