Chuda Kashara
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 849
- 554
Wakuu wa baraza heshima kwenu,
Kila ninapokuwa watu wananikodolea macho kupita kiasi. Niwe mitaani, barabarani, sokoni au sehemu yoyote watu wananishangaa bila kujua nini sababu. Watoto, wazee, watu wa rika langu, watu wazima na wa jinsia zote wamekuwa wakinikodolea macho sana. Wengine wanakodoa kwa kujificha na wengine waziwazi.
Nashtushwa na hiyo hali cause nikipita sehemu na kuwa kama mzimu uliofufukia kwenye mtaa uliozikwa kutokana na jinsi wanavyonishangaa. Sometimes inanilazimu kuingia chimbo kujikagua kama zipu ipo sawasawa au ndege ameninyea bila kujua ila najikuta nipo sawa. Nimevumilia ila nikaona si vibaya kuja kuuliza nini sababu ya watu kuwashangaa watu wengine pindi wawapo kwenye mishe mishe zao? Kama umewahi kumkodolea macho mtu mwingine sababu inakuwa ni kitu gani?
Asanteni!