Kila ninaempata ananizidi kielimu.

tehee....tehee....teheee! imenikumbusha mbali sana kipindi cha nyuma nilikuwa dancing fulooo na bi mdada fulani hivi katika mahojiano (ya kitoto wakati huo) nikajitanua nafanya kazi sehemu fulani na nikweli nilikuwa nafanya kazi lakini alivyoniambia yuko chuo mwaka wa pili confo likashuka nikajivutavuta na kumwambia akazane shule ni ya maana sana huku japo kwa kweli niliomba mziki uishe haraka na mwaka uliofuata nilienda shule
hivyo dogo nenda shule acha uzembe vyuo kibao kwa sasa kama unajisikia vibaya

Nimeipenda hio DANCING FULOO
 
hata mimi nazeeka wachumba siwaoni wote wanataka mke mwenye degree,mie nimeamua nianze kwa diploma kwanza sijui lini nitagraduate,isikushangai ukifika age fulani na hujasoma unaona uvivu sio km ukiwa young na nguvu zako
 
kijana kama unataka kusoma wewe soma lakini elimu sio kigezo cha mapenzi, ingelikuwa elimu ndio kigezo cha mapenzi sie tuliokimbia shule tungelikuwa tunasikiliza mapenzi RTD
 
Mapenzi hayaangalii elimu lakini linapokuja swala la maendeleo hapo ndipo kipengele cha elimu huingia.Sawa waweza ukawa huna elimu na ukawa na maendeleo ila kasi ya kuyafikia malengo yako na mikakati yake ni tofauti na aliyesoma. Aliyesoma kasi yake ni kubwa.
The matter of fact is; Wanawake wana asiri ya kuwa na mwanaume aliyemzidi kitu fulani [ that's their nature in life], sasa wengi wao huangalia elimu maana ndo kila kitu in life. Endelea kutafuta maana somewhere there's a beautiful wuman waiting for you.
 
Mdanganye mwambie wewe una degree, kama mm nlivofanya japo atakuja kugundua ila atakuwa amechelewa ww vp? Acha uvivu unamwambia maswala ya coursework,
 
wekomaa au haujui kuimbisha ni pm nikupe mashaili niliyo muimbisha mwanashelia wangu. {degree ya shelia kwa std vii "f"ongeza watoto wangu watano kawakuta na analea } fedha ndiyo kilakitu {chezea ukulima wa kuku, chezea mistari ya masikini?}
 
Ndugu wana MMU poleni kwa majukumu. Mimi ni mwanaume mwenye umri wa kutosha kuwa na familia. Shida inakuja pale ambapo kila mchumba ninaemuona ananifaa kuoa na anaendana na sera zangu ananizidi kwa elimu. Nikimpata mwenye sera kama za kwangu aniuliza nina elimu ya kiwango gani?nikimwambia elimu yangu ananiambia kaka elimu yako haiendani na yangu. Na kwa bahati mbaya wanawake wote ambao nimekutana nao wamenizidi kwa elimu. Kama mnavyojua wanawake wenye elimu huwa wanapenda wanaume waliowazidi kwa elimu angalau kidogo. Mimi nina elimu ya form4 ila nimebahatika kuwa na kazi ambayo kipato chake kinanitosha kuendesha maisha yangu na pia mimi ni mjasiriamali. Nasema inanitosha kwani imenijengea nyumba ambayo ndo naishi kwa sasa na inaniwezesha kula vizur kila cku. Naombeni ushauri, nifanyaje nimpate wangu anaendana na elimu yangu?ukizingatia umri ndo huo miaka30.

pole elimu siyo kipimo cha mapenzi, subiri wakati wako haujafika ukifika utampata mke mwema
 
Ni wanawake wachache walioolewa na wanaume wanaowazidi elimu wanaoishi vizuri katika ndoa zao. Wengi wanaishia kuachana baada ya muda siyo mrefu. Nakushauri tafuta mwanamke mtakayeendana kwa kila kitu. Siyo baadaye awe mzigo kwako.
 
Back
Top Bottom