Kila ninaempata ananizidi kielimu.

Kila ninaempata ananizidi kielimu.

Possible walichokuzidi wewe ni elimu ya kwenye karatasi tu lakini si elimu ya maisha,Usikate tamaa naamini hao waliokuzidi elimu ndo wanaokufaa wewe kwa kuwa ndiyo wamekuwa na vigezo utakavyo naamini Mwenyezi Mungu ana mpango na wewe,yupo wa aina yako she is waiting for you to meet her,so vuta subra utampata na hata tizama elimu yako bali namna mtakavojenga maisha yenu ya sasa na baadae.Be Blessed Bro!

Asante Mgaya D.w kwa ushauri wako mzuri ntaufanyia kazi.
 
elimu ya chini inaanzia wapi?

Kama wewe huwezi, je wanawake wote hawawezi?

Je, ndoa za wasomi zote zina furaha?

ndo mana huko kote alikopita wanamzngua kama ingekua sio hivo asingelalamika hapa angeshampata, na kwa uwezo wake kiuchumi ndo mana anakutana nao walomzidi elimu..and mara nyingi mwanamke akimzidi mwanaume elimu huwa neno kidogo
 
kwani wee mtoa mada kufikisha miaka 30 ndio nini? Ndio lazima uoe hata kisiki?

Tafuta mwanamke anayekufaa haya mengine ni maelezo ya ziada tu.

Kama elimu mali ungewaambia wakaolewe na Nkurumal Hall au mdigirii
Hahahhahahhahaaaa umenipa raha sana
 
Options ni tatu hapa, 1. Nenda shule ujiendeleze 2. Tafuta of your caliber 3. Kuwa single for life
 
Ndugu wana MMU poleni kwa majukumu. Mimi ni mwanaume mwenye umri wa kutosha kuwa na familia. Shida inakuja pale ambapo kila mchumba ninaemuona ananifaa kuoa na anaendana na sera zangu ananizidi kwa elimu. Nikimpata mwenye sera kama za kwangu aniuliza nina elimu ya kiwango gani?nikimwambia elimu yangu ananiambia kaka elimu yako haiendani na yangu. Na kwa bahati mbaya wanawake wote ambao nimekutana nao wamenizidi kwa elimu. Kama mnavyojua wanawake wenye elimu huwa wanapenda wanaume waliowazidi kwa elimu angalau kidogo. Mimi nina elimu ya form4 ila nimebahatika kuwa na kazi ambayo kipato chake kinanitosha kuendesha maisha yangu na pia mimi ni mjasiriamali. Nasema inanitosha kwani imenijengea nyumba ambayo ndo naishi kwa sasa na inaniwezesha kula vizur kila cku. Naombeni ushauri, nifanyaje nimpate wangu anaendana na elimu yangu?ukizingatia umri ndo huo miaka30.

Unataka mtu wa kuishi nae au kushindana nae elimu?

Kula vizuri ndio lengo la maisha yako?

Hivi kupata mwanamke aliyesoma ni bahati au nzuri? This is very strange, what a primitive mind
 
ndo mana huko kote alikopita wanamzngua kama ingekua sio hivo asingelalamika hapa angeshampata, na kwa uwezo wake kiuchumi ndo mana anakutana nao walomzidi elimu..and mara nyingi mwanamke akimzidi mwanaume elimu huwa neno kidogo

Another primitive mind.

Hicho kinacholeta maneno sio elimu ni VYETI. Mwanamke aliyeelimika hana neno kwa mumewe kwani elimu huleta busara na hekima kichwani.
 
Tafuta walimu au manesi wako vizuri tu na upeo wao ni mzuri na mtatengeneza familia safi tu!
 
HorsePower kweli umesema
Ila sidhani kama elimu ni kizuizi kitakachokufanya ushindwe kuoa
nafikiri wewe ndiye mwenye matatizo kwa kuwa unakimbilia sana kuuliza suala la elimu japo hapa umeliweka kama vile unaulizwa wewe
Na hao wote uliokutana nao nafikiri sio wife material wanataka watu wa show off
Tulia na tafuta wa kweli wa kuoa

Kweli jamaa hakijiamini maana ukijiamini demu mara nyingi hata kukuuliza masuala ya elimu mwanzoni haoni haja maana akikuangalia anakuona kama level yake the way mnavyoongea na unavom-handle. inaelekea mdau ndio anakuwa wa kwanza kuwauliza na akisikia wamemzidi tu anajinyanyapaa. Hata kama elimu ndogo kwenye mazungumzo yake asijishushe sana bali angalau aweke wayforward kuhusu mustakabali wake kielimu kwani kama ameweza kuzitafuta ela mpaka akajenga na kufanya ujasiamali maana yake akiweka nia ya kupiga shule pia anaweza. KAMA SHULE NDOGO WEWE KATIKA MASUALA YA ELIMU NI KUWEKA FUTURE PLAN NA KUMWULIZA KOZI GANI NZURI KUONYESHA ANA NIA YA KUSOMA, FORM 4 MBONA ELIMU KUBWA KABISA KUJIENDELEZA HATA KWA LONG DISTANCE NA ZILE QT ZETU MPAKA UNAKUWA MBOBEFU KTK ELIMU
 
Tatizo nadhani sio elimu tatizo ni PESA ungekua nazo nyingi kumzidi yeye wala wasingejali elimu wala as long as ATM inatema bila kikwazo mbona ungempa unaemtaka sasa nadhani haina haja yakujitabisha tafuta anaekupenda kwa dhati
na atakae kupenda wewe kama wewe sio pesa yako..
 
Ndugu wana MMU poleni kwa majukumu. Mimi ni mwanaume mwenye umri wa kutosha kuwa na familia. Shida inakuja pale ambapo kila mchumba ninaemuona ananifaa kuoa na anaendana na sera zangu ananizidi kwa elimu. Nikimpata mwenye sera kama za kwangu aniuliza nina elimu ya kiwango gani?nikimwambia elimu yangu ananiambia kaka elimu yako haiendani na yangu. Na kwa bahati mbaya wanawake wote ambao nimekutana nao wamenizidi kwa elimu. Kama mnavyojua wanawake wenye elimu huwa wanapenda wanaume waliowazidi kwa elimu angalau kidogo. Mimi nina elimu ya form4 ila nimebahatika kuwa na kazi ambayo kipato chake kinanitosha kuendesha maisha yangu na pia mimi ni mjasiriamali. Nasema inanitosha kwani imenijengea nyumba ambayo ndo naishi kwa sasa na inaniwezesha kula vizur kila cku. Naombeni ushauri, nifanyaje nimpate wangu anaendana na elimu yangu?ukizingatia umri ndo huo miaka30.

Inaonesha unapenda wanawake wa class fulani ambao wengi ni wasomi na hata kama sio wasomi wanataka mtu msomi, find a simple loving woman hata kama anakuzidi elimu mtaheshimiana na kufika mbali. usitafute kwa kuangalia kuwa ni mtoto wa nani, amefika nchi gani na leo kavaanguo ya designer gani hapo utaumia sana au kubali matokeo urudi shule kwanza mpaka unafikia PHD utakuwa 40 na hao unaowasomea watakukimbia utakuwa kizee.
 
Kwanza jiamini!!!elimu yako c ndogo kiasi hicho!!!ww amini mwenye mapenzi ya dhati kwako hajatokea na hayupo mbali!!!
 
Back
Top Bottom