Kila nikipata mwanamke, dada na mama wanasema hafai

Kila nikipata mwanamke, dada na mama wanasema hafai

Kila nikiwa na mahusiano lazima dada na mzazi (mama) waniambie mwanamke hanifai na nikimuacha wanaanza kunisengenya kuwa siwezi kuishi na mwanamke.

Hali hii inasababishwa na nini?
Iyo hali inasababishwa na wewe na kweli wamekwisha ona hujui unataka nini, mke ni kwa ajili yako iweje mama na dada ndo wachague?
 
Dawa ni moja tu anza kutembea na best friends wa Dada yako na mama yako hakikisha wanaaminiwa na hao ndugu zako.
Kwa wao wamewezaje kuwa na best friends ambao hawafai?
Over
 
Isack,

Huwezi fanya maamuzi yako wewe kama mwanaume? Mpaka mama na dada wakupangie, seriously? Unakoelekea utapangiwa mpaka siku za kupiga game na mkeo walaqhi!
Kwa picha ya fasta huenda kalelewa sana na mama wakisaidiana na dadaake pia huenda baba hayupo na kama yupo hakuna mahusiano mazuri baina yao kiasi washauri wakuu wamebaki hao.
 
Kila nikiwa na mahusiano lazima dada na mzazi (mama) waniambie mwanamke hanifai na nikimuacha wanaanza kunisengenya kuwa siwezi kuishi na mwanamke.

Hali hii inasababishwa na nini?
Kwa kifupi tuu wazazi wako sahihi kwa sababu zifuatazo

1.sababu ya kwanza wanakuona wewe bado mvulana na sio mwanaume

2.cha pili zile sifa za kuitwa mwanaume bado haujazikamilisha

3.ukizikamilisha sifa za kuitwa mwanaume haya yote hawawezi kukuambia
 
Kila nikiwa na mahusiano lazima dada na mzazi (mama) waniambie mwanamke hanifai na nikimuacha wanaanza kunisengenya kuwa siwezi kuishi na mwanamke.

Hali hii inasababishwa na nini?
Next time hebu wapelekee mwanaume maana kama wanasema "mwanamke hakufai", "huwezi kuishi na mwanamke" basi swala liko wazi.
 
Kila nikiwa na mahusiano lazima dada na mzazi (mama) waniambie mwanamke hanifai na nikimuacha wanaanza kunisengenya kuwa siwezi kuishi na mwanamke.

Hali hii inasababishwa na nini?
Ni kwa sababu wewe bado mvulana hujawa mwanaume, siku ukiwa mwanaume kamili basi mama na dada wataacha kuingilia maisha yako binafsi especially mahusiono

Jinsi ya kuwa mwanaune kamili ni kuwa na maamuzi na misimamo pamoja na uhakika wa kila unachokifanya

Kauli yako iwe ya mwisho kwenye mahusiano yako whether they like it or not maana atakaeishi na huyu mwanamke ni wewe, sio mama wala dada
 
Kila nikiwa na mahusiano lazima dada na mzazi (mama) waniambie mwanamke hanifai na nikimuacha wanaanza kunisengenya kuwa siwezi kuishi na mwanamke.

Hali hii inasababishwa na nini?
HUWA WANAKUPA SABABU KWA NINI HAWAFAI?
 
Back
Top Bottom