Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 739
Kwa wale wanawake wenye tabia ya kusema hawataolewa na mwanaume suruali ambaye hana pesa basi kazi wanayo maana takwimu zinaonyesha kuwa takribani asilimia themanini ya wanaume wenye mafanikio kimaisha basi nyuma yao kuna sapoti ya mwanamke.
Hii ina maana ya kuwa wewe kama mwanamke ni bora utafute mwanaume ambaye hana chochote ili mustraggle wote maana ukisema hutaki mwanaume suruali asiye na pesa kumbuka huyo unayemuona kuwa ana pesa na ukamng'ang'ania kuwa huyo ndo wako kaa ukijua atakutumia na mwisho wa siku atakuacha kwani kuna mwanamke nyuma yake ambaye wametoka mbali kimaisha na hatokuwa tayari kumuacha na kukuoa wewe ambaye umemkuta akiwa tayari na mafanikio.
Na hata hapa jamvini tumekuwa tukishuhudia nyuzi nyingi za akina Dada wakiwalaumu wanaume kuwa eti ni matapeli na mara nyingi huwadanganya kuwa watawaoa lakini baada ya mda huwaacha na kuoa wanawake wengine, kumbuka huyo mwanamke aliyemuoa baada ya kukuacha wewe alikuwa naye tangu mwanzo na ndio maana hakuwa tayari kukuoa wewe na kumuacha yeye.
Kwa hivyo wewe kama ni mwanamke mwenye future na malengo katika maisha yako ni heri utafute mwanaume asiye na pesa ili mshirikiane na mpambane kutafuta zenu kuliko kukimbilia wenye pesa maana mwisho wa siku utaumizwa maana huyo mwenye pesa nyuma yake kuna mwanamke so take care as life doesn't get easier you just get stronger.