Kila mwana JF akiwafungua macho watu 100, Tanzania itakombolewa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila mwana JF akiwafungua macho watu 100, Tanzania itakombolewa.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dopas, Aug 29, 2010.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wapendwa wanaJF, ni yamkini tulifuatilia kwa makini tangu mbio za uraisi zilipoanza rasmi 20/08/2010 pale ambapo wagombea wote wa viti vya urais na wabunge walipotakikana kwa utaratibu, kurudisha fomu ili kuthibitisha kuwa wana nia thabiti kwa nafasi hiyo.

  Ni imani yangu kuwa wengi wetu wamefuatilia kwa umakini mkubwa bila ushabiki wa kijinga yaliyofuata baada ya hapo.

  Binafsi nimefuatilia hoja nyingi zilizotolewa na wachangiaji mbalimbali katika magazeti ya mwananchi, Tanzania daima na mengine, ingawa Tanzania Daima hatuipatikani mtandaoni kwa sasa.

  Ni wazi kuwa kila moja wetu anafahamu vizuri hali ya nchi yetu, walau hali ya sehemu anayotoka.

  Ni wazi kuwa kila mwananchi makini anatambua kuwa kuna haja ya mabadiliko ya uongozi wa nchi tukitaka tusonge mbele. Haidhuru kiongozi wa mabadiliko hayo atoke chama gani, dini gani kabila gani, sehemu gani ya nchi yetu, wadhifa gani alionao, nk.

  Ni wazi pia wengi wetu, kama sio wote tumefuatilia ufunguzi wa kampeni za vyama vitatu: CCM, CUF, CHADEMA.

  Kuna mambo mengi ya kulalamikiwa, kuna mengi ya kupongezwa, kuna mengi ya kurekebishwa katika vyama vyote hivyo.

  Moja ambayo imenigusa niwaandikie ninyi wanaJF ili tuwe sote vyombo vya habari.

  Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu vyombo vya habari kuwapendelea vyama vingine. Tusisahau kuwa kipindi hiki pia ni kipindi cha mavuno kwa wengine. Ndio maana utaona msururu wa wanamuziki wa bf na hata wa dini wakimzingira JK ili waambilie kitu. Mbwa hawezi kumfuata asiye na chakula mkononi. Ndiyo maana CCM imewawekea alama mbwa wake-wamevishwa ma... ya CCM ili waweze kufuata amri ya bwana wao. Na wasiofuata hutimuliwa kama tulivyosikia wiki jana, ingawa sirikali imekana.......! Ni bahati mbaya hata TBC chombo ambacho kinalipiwa kodi na wanachi wote bila kujali chama kinawapendelea mafisadi wa CCM. Lawama nyingi anatupiwa Tido lakini, kumbuka mbwa hutawaliwa na mmiliki wake. Akiambiwa kamata... akiambiwa achaaaa... hufuata sauti ya anayempa kunya...

  Kumekuwa na dalili pia ya vyombo binafsi ambavyo tulivitegemea viwe mkombozi wa vyama vya upinzani kama ITV, kuegemea upande wa CCM. Inashangaza, hatuwezi kujua sababu lakini ndiyo hali halisi.

  Je, tufanye nini katika hali hiyo? Tukate tamaa na kusema ushindi ni wa JK na mafisadi wake RA, EL, kina Makamba na wenzao? Je, turidhike kuwa hatuwezi kufanya chochote kama ambavyo baadhi ya wachangiaji kwenye JF kukata tamaa ingawa wanaonesha nia ya kutaka mabadiliko na kuiondoa CCM madarakani? Je, tuendelee kulalamika kuwa CCM inahujumu vyama vingine kwa kuvithibiti vyombo vya habari,ulinzi, Tume ya uchaguzi, nk?

  Natumaini kila mwenye mapenzi mema na nchi yetu ana ufumbuzi.

  Lakini kuna maswali ya msingi kwako mwanaJF. Je, umejiandikisha kupiga kura? Utampigia kura nani? Je, unawaelimisha wengine wajibu wao wa kupiga kura na wajibu wa kuchamgua mtu au chama kwa aajili ya ukombozi wa nchi yetu?

  Ni wazi kuwa tunatumia internet kwa mawasiliano, lakini vijijini mwetu hakuna hata umeme wa kawaida sembuse internet.

  Ombi walau kila mwanaJF awaelimishe wapiga kura 100, ili kwanza wafahamu wajibu na haki yao ya kupiga kura. Pili, wafahamu lengo, na hitaji la ukombozi wa nchi hii ili wampigie kura wanayeona anafaa kuleta ukombozi huo, ila sio JK wa CCM na mtandao wote wa ufisadi. JK, amefanya sehemu yake. Inatosha, aitwe tu rais mstaafu wa awamu ya 4.

  Hili linawezekana. Ni utambuzi tu. Kumbuka pengine baba, mama, babu na bibi yako sio wanaJF, na hawajapata utambuzi wa hili. Wakumbuke ndugu zako, jamaa zako, majirani zako na wote ambao hufikiri CCm ni maisha yao, wapate kuelewa hitaji la kutaka mabadiliko.

  Mungu awaongoze katika maamuzi mtakayochukua kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Poa sana!
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Idea nzuri ila sisi Watanzania ni waoga hadi wanaboa. Kuna mdau alishawahi kuuliza kwenye topic nyingine kama siku tukisema wanaJF tukutane pale Diamond Jumbilee tufanye discussions zetu live and kuwaelimisha wananchi wa kawaida ni wangapi watakuja? Kuna watu wataogopa kufika wakifikiri watakamatwa au watajulika kuwa wao ni members wa JF Forums. Watanzania tuna asili ya woga tu na hivyo kutufanya tuonekane wanafiki hatuwezi kupigania tunachoamini. Ndio maana tuna find a comfort zone kama JF Forums. Kama kweli "we dare to talk openly" then we need to go out there and spread the message. Otherwise, tutaishia kwenye hizi confort zones ambazo ni Watanzania wachache sana wana access nazo.
   
Loading...