Kila mwana CCM ni msemaji wa serikali?

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,583
3,182
Hivi karibuni kumetokea tabia hapa nchini kila serikali inapokosolewa iwe na wapinzani au mtu mwingine yeyote yule watu wanasimama kutetea bila kujua kama jambo husika lina ukweli kiasi gani na kuwafanya wakosoaji kuwa hawajui kitu na hata kama suala lenyewe linahusu kutekeleza taratibu, kanuni ama sheria.

Ndugu zangu eleweni kuwa watu wanapokosoa hawalengi kuichukia ama kupinga mazuri yanayofanywa na serikali bali ifanye kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria hapo inapendeza sana, leo magufuli ametoa mwongozo kama wapinzani walivyotaka mkawazomea sawa mtaficha wapi nyuso zenu imbeni tena huo wimbo mpya nawashauri mkasome kitabu cha shamba la wanyama 'the animal farm' huko mtajifunza vizuri kuhusu upambe usiofaa, watanzania tuheshimiane mbona tutaenda vizuri tu sisi sote tu binadamu kukosea ni jambo la kawaida tu mbona .
Att:jingalao
 
Na serikali inayokubali kukosolewa ina sifa ya kufanya vizuri katika kuwatumikia wananchi. MTU asiyekubali kukosolewa hawezi kujifunza kipya anadumaa hatimae anachokwa. N miaka mingi mno wapinzani wamekuwa wakiikosoa serikali lakini waliwabeza na kuwatusi .lakini sahv jpm anajitahidi kufanyia kazi mambo yaleyale waliyopigia kelele wapinzani .MF aliyekuwa mkurugenzi wa jiji DSM . ni rai yangu kwamba kila mtu auheshimu upinzani kwa kazi nzuri wanayofanya. Huwa nawaza tu kwamba hivi hii nchi bila upinzani wananchi tungekuwa kwenye tope na macho yetu yakiwa na tongotongo nyingi.
 
Hata mawaziri wakitoa majibu huwa ni ya hovyo hovyo pia...ccm kujitoa ufahamu ni jadi yao....ngoja waje humu ndo utajua namaanisha nn
 
CCM imejenga utamaduni wa kuhakikisha wanachama na wadhabiki wake hawafahamu kabisa tofauti ya dola na chama.
Ndio maana wao hata waziri awachinje hawawezi kuhoji kwani ni kukidhalilisha chama
 
Unapokosoa kitu ni lazima ukosoe kile ambacho unaona hakipo vizuri na kimefanywa bila kuangalia maslahi ya Wananchi. Lakini ukosoaji wenu nyie wengine hutokea hata pale ambapo hapapaswi kukosolewa. Kitu kimefanywa kwa maslahi yetu lakini kwa kuwa wewe huipendi ccm unakosoa tu, huo ndio ujinga ambao hautakiwi... MTU HAKATAZWI KUKOSOA LAKINI JE UNACHOKOSOA NI SAHIHI? HAPA NDIPO TUNAPOTOFAUTIANA
 
Hivi karibuni kumetokea tabia hapa nchini kila serikali inapokosolewa iwe na wapinzani au mtu mwingine yeyote yule watu wanasimama kutetea bila kujua kama jambo husika lina ukweli kiasi gani na kuwafanya wakosoaji kuwa hawajui kitu na hata kama suala lenyewe linahusu kutekeleza taratibu, kanuni ama sheria.

Ndugu zangu eleweni kuwa watu wanapokosoa hawalengi kuichukia ama kupinga mazuri yanayofanywa na serikali bali ifanye kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria hapo inapendeza sana, leo magufuli ametoa mwongozo kama wapinzani walivyotaka mkawazomea sawa mtaficha wapi nyuso zenu imbeni tena huo wimbo mpya nawashauri mkasome kitabu cha shamba la wanyama 'the animal farm' huko mtajifunza vizuri kuhusu upambe usiofaa, watanzania tuheshimiane mbona tutaenda vizuri tu sisi sote tu binadamu kukosea ni jambo la kawaida tu mbona .
Att:jingalao
Toa suluhu baada ya kukosoa. usipofanya hivyo utakuwa huna msaada.
Pia wapinzani nao wamekuwa watu wa kulalamika tu kiasi cha kupoteza malengo ya elimu itolewayo nchini kuwa inazalisha walalamishi. Eti ili kijana wa Kitanzania aliyesoma kwa mujibu wa wapinzani lazima awe fundi wa kuorodhesha kero na kulaumu.
 
Na serikali inayokubali kukosolewa ina sifa ya kufanya vizuri katika kuwatumikia wananchi. MTU asiyekubali kukosolewa hawezi kujifunza kipya anadumaa hatimae anachokwa. N miaka mingi mno wapinzani wamekuwa wakiikosoa serikali lakini waliwabeza na kuwatusi .lakini sahv jpm anajitahidi kufanyia kazi mambo yaleyale waliyopigia kelele wapinzani .MF aliyekuwa mkurugenzi wa jiji DSM . ni rai yangu kwamba kila mtu auheshimu upinzani kwa kazi nzuri wanayofanya. Huwa nawaza tu kwamba hivi hii nchi bila upinzani wananchi tungekuwa kwenye tope na macho yetu yakiwa na tongotongo nyingi.
Wapinzani wenyewe hutegemea taarifa ya CAG ndiyo huona wamepata hoja za kusema. Hawana kitu. Sasa wameshupalia Lugumi kama njia mpya ya kupata umakini wa watanzania maana kila wafanyacho sasa hivi wananchi wanawapotezea.
Nchi ilikwisha weka taasisi ya kufuatilia matumizi ya serikali yaani CAG kwenye katiba kabla ya vyama vingi. Hivyo hata kusiwepo wapinzani taasisi hii ndiyo inayotosha. kwani kila ubadhilifu unaousikia wapinzani wanshangaika nao chanzo ni hii taasisi. Tambua hilo.
 
Ungejua ni lini upinzani umeanza na harakati za kupambana na mafidadi na wizi wa nchi hii usingesema hivo. Hivi jiulize tu hii nchi bila mltipartism tungewezaje kujua wezi wa nchi hii . uliwahi kuona wapi nyani anampelekea ngedere kesi
 
Hivi karibuni kumetokea tabia hapa nchini kila serikali inapokosolewa iwe na wapinzani au mtu mwingine yeyote yule watu wanasimama kutetea bila kujua kama jambo husika lina ukweli kiasi gani na kuwafanya wakosoaji kuwa hawajui kitu na hata kama suala lenyewe linahusu kutekeleza taratibu, kanuni ama sheria.

Ndugu zangu eleweni kuwa watu wanapokosoa hawalengi kuichukia ama kupinga mazuri yanayofanywa na serikali bali ifanye kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria hapo inapendeza sana, leo magufuli ametoa mwongozo kama wapinzani walivyotaka mkawazomea sawa mtaficha wapi nyuso zenu imbeni tena huo wimbo mpya nawashauri mkasome kitabu cha shamba la wanyama 'the animal farm' huko mtajifunza vizuri kuhusu upambe usiofaa, watanzania tuheshimiane mbona tutaenda vizuri tu sisi sote tu binadamu kukosea ni jambo la kawaida tu mbona .
Att:jingalao
Uko sahihi mr . ccm wao kujua ni kisa mpaka rais aseme
 
Unapokosoa kitu ni lazima ukosoe kile ambacho unaona hakipo vizuri na kimefanywa bila kuangalia maslahi ya Wananchi. Lakini ukosoaji wenu nyie wengine hutokea hata pale ambapo hapapaswi kukosolewa. Kitu kimefanywa kwa maslahi yetu lakini kwa kuwa wewe huipendi ccm unakosoa tu, huo ndio ujinga ambao hautakiwi... MTU HAKATAZWI KUKOSOA LAKINI JE UNACHOKOSOA NI SAHIHI? HAPA NDIPO TUNAPOTOFAUTIANA
Kuna wakati serikali na ccm waliwahi kukubali kukosolewa? Tanzania siyo kisiwa ktk hii dunia. Tatizo serikali na ccm wanashindwa kukubali kuwa wao si malaika
 
Yaani utoke huko mambo ya kienyeji yasiyo source utegemee tukae kimya, kumbuka "wenye ufahamu wakikaa kimya wajinga hutawala" ni lazma tuseme kumwelewesha yule asiefahamu na sio lazima awe mwana ccm
 
Wapinzani wenyewe hutegemea taarifa ya CAG ndiyo huona wamepata hoja za kusema. Hawana kitu. Sasa wameshupalia Lugumi kama njia mpya ya kupata umakini wa watanzania maana kila wafanyacho sasa hivi wananchi wanawapotezea.
Nchi ilikwisha weka taasisi ya kufuatilia matumizi ya serikali yaani CAG kwenye katiba kabla ya vyama vingi. Hivyo hata kusiwepo wapinzani taasisi hii ndiyo inayotosha. kwani kila ubadhilifu unaousikia wapinzani wanshangaika nao chanzo ni hii taasisi. Tambua hilo.
Acha umalaya wa mdomo. Kama CAG iko miaka hiyo kwa nini ubadhirifu uliweka mizizi? CAG ni mkaguzi tu, na bado anawakabidhi taarifa wabadhirfu/wezi walewale. Bila upinzani ni vigumu ccm na serikali kujirekebisha
 
ccm bila upinzani cjui nchi hii walikuwa wanaipeleka wapi yani ...chini ya dr chimpumu tusitalajie chochote cha maana
 
Acha umalaya wa mdomo. Kama CAG iko miaka hiyo kwa nini ubadhirifu uliweka mizizi? CAG ni mkaguzi tu, na bado anawakabidhi taarifa wabadhirfu/wezi walewale. Bila upinzani ni vigumu ccm na serikali kujirekebisha
Wewe unayejua umalaya wa mdomo ndiye unajua unafanyikaje. Nimekusaidia kujua umri wa ofisi ya CAG unazidi vyama vya upinzani beba hili sikunyingine utaonekana mwelevu. Nikuongezee hili baada ya Kikwete kushika madaraka aliagiza taarifa hii iwe inajadiliwa bundeni. Pia alikwenda mbali na mkutaka CAG awe anakwenda na polisi au PCCB ili pale manyanga yanapogundulika awakabidhi polisi au PCCB waendelee na huo uozo sio kusubiri mpaka taarifa itolewe. Sasa baada ya hapo ndipo upinzani wemekuwa wakipatiapo hoja. Huenda ulikuwa mtoto kujua haya, basi jifunze usikurupuke.
 
T
Ungejua ni lini upinzani umeanza na harakati za kupambana na mafidadi na wizi wa nchi hii usingesema hivo. Hivi jiulize tu hii nchi bila mltipartism tungewezaje kujua wezi wa nchi hii . uliwahi kuona wapi nyani anampelekea ngedere kesi
Tumia akili kidogo tu kutambua hili. Kila linalofanywa bungeni uamuzi hufanywa na wabunge wa ccm. Tambua kuwa uamuzi wowote uliofanywa bungeni uwe mzuri kwako au mbaya umefanywa na wabunge wa ccm. Wabunge wa upinzani wanechangia mawazo yao. Kwakuwa huwa unawaelewa watu wa upinzani kwa kuwa akili zenu ziko sawa wewe huwaona wao.
 
Back
Top Bottom