Kila mtu na ndoto zake

Chilojnr

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
302
1,306
Wakati mwingine maisha ni kama bahati. Inawezekana Mh. Samiah Suluhu hakuwa kufikiria kuwa rais. Inawezekana kabisa kama angekuwa na ndoto za kuwa rais siku moja na kuwaambia marafiki zake, wengi wangemcheka na kumuona ni kituko, ila mwisho wa siku, anakuwa rais wa Tanzania.

Si kila ndoto kubwa iliyotimia ilipangwa tangu zamani, ndoto nyingine zinakuja ghafla tu unakuta zimetimia, unabaki ukimshangaa Mungu. Inawezekana kuna mbunge hakuwahi kufikiria kuwa mbunge maishani mwake. Ila siku moja alipokaa nyumbani, wenzake wakamwambia mbona unakubalika sana, hebu gombea uenyekiti wa mtaa, jamaa akagombea, akaupata.

Baadaye akashawishiwa kugombea udiwani, akafanya hivyo na akaupata. Sasa akawa na ndoto za kuwa mbunge, ndoto iliyoanza ghafla kwenye safari yake, mtu huyo akagombea, kweli akaupata, akatimiza ndoto ya ghafla aliyoipanga ukubwa.

Watanzania huwa hatuna ukawaida wa kupanga ndoto kubwa, huwa hatunaga imani, tofauti na wenzetu. Wake wa marais wengi akiwemo Michelle (Mke wa Obama) alikuwa na ndoto ya kuwa mke wa rais siku moja. Maisha yake yakawa na muonekano wa mke wa rais, hakuishi Kislay Queen, alihisi kwa kujiheshimu kwa kuwa aliamini kuna siku ndoto yake ingetimia, ila hakujua kwa namna gani.

Obama hakuwa na ndoto za kuwa rais, ila baada ya kumpata Michelle aliyekuwa na ndoto za kuwa mke wa rais tangu udogoni mwake, Mungu akatimiza kwa kumpa Obama urais.

Donald Trump alikuwa na pesa, utajiri mkubwa ila alichokitaka ni heshima. Alihitaji kuwa rais kwa kuwa alijua una heshima yake. Alipata kila kitu ila alikosa heshima ya kirais tu, hivyo akaipambania ndoto yake ya ukubwani, akawa rais na kupata heshima aliyoita ikiwemo kupigiwa saluti.

Unaweza kuwa na ndoto ndogo na ya kawaida, ila nataka kila utakapopiga hatua, jiwekee kutimiza ndoto kubwa zaidi na zaidi. Ishi kwenye ndoto zako, hata kama watu watakucheka, usijali, hakikisha unatimiza hizo ndoto. Siku zikitimia, panga ndoto nyingine.

Imeandikwa na Nyemo Chilongani.


1752757349.jpg
 
Umeandika kinyonge sana mkuu.

Ila ninachoamini maisha ya Mtu yamechorwa remani yake na Mungu.

Ni kazi yetu kufanya kazi kwa bidii na maarifa pale tulipo tukiamini lolote laweza kutokea.

Mama kiukweli kaokota dodo kwenye Mnazi kama ilivyokuwa kwa Hayati Magufuri kwenye mbio za uraia 2010 pale dodoma
 
Back
Top Bottom