Introver
JF-Expert Member
- Apr 6, 2019
- 565
- 656
(Mafunzo maalumu kwa watoto na walezi).
Kama wewe ni mtoto basi jifunze haya, na kama ni mzazi basi pia jifunze haya na pia mfunze mwanao…
“Kumcha mzazi” sio “kumwabudu” bali ni kumpa heshima ya hali ya juu sana, ikiwemo kumsikiliza, kumtii na kufanya yale anayosema bila kumsumbua sumbua ikiwa jambo hilo si nje na mapenzi ya MUNGU.
Maana yake kama tunavyomcha MUNGU, kila atuambiacho tunakizingatia, kwasababu tunajua kwake kuna baraka na laana, kadhalika na wazazi hivyp hivyo wanaweza kutubariki na kutulaani.
Sasa wengi wetu inapofika eneo hili la kutafakari mzazi na mtoto akili zetu huwa zinalenga kufikiri wale watoto walio chini ya malezi ya wazazi, pasipo kujua kuwa hata uwe na miaka 70 na kama mzazi wako yupo hai bado hiyo amri inakuhusu hata wewe ya kumcha mzazi wako, kwani wewe bado ni mtoto kwake.
Amri ya watoto kuwatii na kuwaheshimu wazazi inawahusu hata wenye ndevu na hata wazee wenye mvi, haijalishi wewe sasa ni bibi au babu na unao wajukuu…kama mzazi wako yupo hai unayo amri ya kumcha..
Lakini ukimvunjia heshima mzazi kwasababu ni mzee, basi fahamu kuwa bado hujayajua maandiko.

Biblia imetumia neno “kumcha” kuonyesha msisitizo wa jambo hilo, jinsi lilivyo la msingi.Mambo ya Walawi 19:3 “Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu”