Kila mtu kumiliki laini 1 mtandao 1

Kila mtu kumiliki laini 1 mtandao 1

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1079667


KUANZIA Mei Mosi mwaka huu, kila Mtanzania atatakiwa kusajili laini kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha Taifa, ambako kila mtu atakuwa na laini moja kwa mtandao mmoja. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alitoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) kuuliza swali bungeni jana.

Selasini alisema katika usajili huo wa Mei Mosi, amesikia kwamba naibu waziri alitangaza mtu anatakiwa kusajili kwa alama za vidole laini moja tu wakati katika baadhi ya maeneo baadhi ya mitandao haipatikani. Naibu Waziri Nditiye alisema ni kweli kuanzia Mei Mosi usajili wa alama za vidole utaanza, ambako kila mtu atasajili laini yake kwa mtandao mmoja.

Alisema alinukuliwa vibaya kwamba mtu anatakiwa kusajili laini moja tu, bali kinachotakiwa hapo ni kuhakikisha kwamba kila mtu anamiliki laini moja kwa mtandao mmoja. “Lengo la usajili huo ni kupunguza utitiri wa laini nyingi ambazo nyingine hazina tija na zinaongeza gharama kwa Watanzania,” alisema Nditiye. Alisema kwa wabunge watasajili laini zao wakiwa wanaendelea na shughuli za Bunge.

Alisema ataomba wamiliki wa kampuni za mitandao ya simu, kupeleka madawati yao hapo bungeni ili wabunge wasajili laini zao. Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Gidirya (Chadema) aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka huduma hiyo katika vijiji vya Yorotonik, Endagwe, Hoshan na Endakiso katika Jimbo la Babati Vijijini, alisema serikali inaendelea kuratibu utekelezaji wa jitihada muhimu za kuwezesha maeneo yote nchini kukiwa na huduma za mawasiliano, sawa na maelekezo ya Sera ya Taifa ya Tehama ya mwaka 2016.

Kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, serikali itavianisha vijiji hivyo kwa kuangalia ukubwa wa eneo, idadi ya wakazi wake na kufanya tathmini ya mahitaji halisi ya ruzuku kwa ajili ya kukisha huduma ya mawasiliano. Baada ya tathmini kukamilika, vijiji hivyo vitajumuishwa katika orodha ya miradi itakayoingia katika zabuni zinazotarajiwa kutangazwa katika mwaka wa fedha 2019/20.
 
maajabu ya tisa ya dunia haya? una line ya kuongea kwenye simu na una kine ya modem ya mtandao mwengine unaposajili laini ya simu je ya modem utasajili vp? naona kuna kifo cha kiasili cha mitandao ya simu inakuja
 
maajabu ya tisa ya dunia haya? una line ya kuongea kwenye simu na una kine ya modem ya mtandao mwengine unaposajili laini ya simu je ya modem utasajili vp? naona kuna kifo cha kiasili cha mitandao ya simu inakuja
Unatakiwa uwe na line ya Tigo 1, Voda 1, TTCL 1, Airtel 1 sio kuwa na Tigo 2, Voda 2, TTCL 2. Kifo cha mitandao ya simu kitatokeaje sasa!?..
Sawa na Mods humu JF wanavyotaka kila mtu amiliki ID moja badala ya Multiple IDs!.
 
Unatakiwa uwe na line ya Tigo 1, Voda 1, TTCL 1, Airtel 1 sio kuwa na Tigo 2, Voda 2, TTCL 2. Kifo cha mitandao ya simu kitatokeaje sasa!?..
Sawa na Mods humu JF wanavyotaka kila mtu amiliki ID moja badala ya Multiple IDs!.
hapo nimekusoma vizuri sana kamanda , nadhani ile dhana ya kuwa na laini moja sikuielewa kwa kila mtandao. Hongera kwa kunielimisha
 
Kuhusu maswala ya laini nahisi hayo ndiyo maendeleo pekee yaliyofanywa na awamu ya 5
 
Mtu huwa na sababu kadhaa za kuwa na laini nyingi za mtandao mmoja kama hizi;

MTU ana simu smartphone na Nokia tochi hapa anakimbia swala la kuishiwa charge

Tena ana simu na moderm hapo anapambana na swala la mtandao na ufanyikaji wa wa kazi kiurahisi

Tena wengine wana simu wanatembea nazo na nyingine kamwachia house boy wake nyumbani aweze kuwasiliana nae kwa urahisi na mtandao ni huo huo ili tarrifs zipungue.

Naona kuna kupungua kwa Wateja au laini moja iwe na looping kwenye simu zote anazomiliki mteja.

Ngoja tuone na makusanyo ya kodi hapa itashuka tu
 
Back
Top Bottom