KILA MTU ANA BEI

KILA MTU ANA BEI

Septem

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2018
Posts
313
Reaction score
404
Pole bwana Chahali.

Jana nilipata ujumbe kutoka kwa mheshimiwa mmoja akinieleza masikitiko yake kuwa licha ya jitihada zake kubwa kunisaidia kupata malipo kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, yaliyotokana na ushiriki wangu kwenye kampeni za chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, suala hilo ilibidi liishe kienyeji yaani bila malipo hayo kufanyika.

Sijawahi kuficha kuwa licha ya sababu nyingine za ushairiki wangu kwenye kampeni za CCM, pia nilifanya kazi ya usadi kwa makubaliano ya malipo. Na si kwamba sikulipwa hata senti tano.Hapana.Muungwana mmoja alitimiza ahadi yake, na nikalipwa kila nilichostahili.

Kazi iliyostahili malipo kutoka kwa Kinana tuliifanya mie na mhusika flani yupo hapa Uingereza, na makubaliano yalikuwa shilingi milioni 12.5 kwa kila mmoja wetu. Kazi tuliyofanya ilipitia kwa dada Mwele Malecela kwa maelekezo ya Kinana mwenyewe.

Awali sikuamini kabisa kuwa mtu anayeonekana “mwema” kama Kinana, na ambaye “hana shida kifedha” angeweza kupuuzia kutupatia haki yetu.Lakini jitihada mbalimbali zangu binafsi, dada Mwele na huyo mhusika mwingine wa hapa, na pamoja na kuwashirikisha watu mbalimbali ikiwa pamoja na huyo mheshimiwa aliyenitumia ujumbe jana, Bwana Kinana “akachikichia” stahili yetu.

Dhuluma sio kitu kizuri. Na ninaamini ipo siku Bwana Kinana atatambua kuhusu hilo the hard way. Kuna uwezekanao mkubwa ameshasahau kuhusu alichotutenda, lakini waswahili husema “mla kunde husahau ila mtupa maganda hasahau.”

Na hili la Kinana “kuchikichia” stahili yetu ni maumivu ya awali kabla ya “kugeukwa” na mtu ambaye baadhi yetu tulitukanwa kila aina ya tusi tulipokuwa tunamnadi, mgombea wa CCM John Magufuli, ambaye sasa anatamani kuona baadhi yetu tukidhuriwa, kisa tunamkosoa.

Lakini yote tunamwachia Mungu. Duniani tunapita tu, na ipo siku tutawajibika kwa Mola kwa matendo yetu wakati wa uhai wetu
 
Kumbe ulilipwa? Una haki ya kusema usemayo. Wazalendo wa kweli hatukulipwa hata sumuni pamoja na kupigwa ngumi na kukwepa visu vya wahuni wa Chadema na mpaka leo bado tunasupport kazi nzuri ya Rais wetu. Go Magu Go.
 
Back
Top Bottom