Pole sana mkuu...ila hapo unaposema unatoa mlio wa kugonga sijakuelewa kidogo...sauti inakuwa kama beep flani hivi au kama vitu vinakuwa vinagongagonga kwa ndani? mana kugonga na mlio wa beep ni vitu viwili tofauti...na huwa inawaka baada ya huo mlio au mpaka uzime na uwashe tena??Mkuu sijui nini, kwa kuwa haupo kibishara I hope nitapata msaada mzuri wa ushauri...
I have Dell Laptop. Tatizo ni kwamba, ninapojaribu kuiwasha, huwa inatoa mlio wa kugonga na hivyo kushindwa kuwaka mara moja. Huu mlio huwa ni endelevu, nilishawahi ku-count nione utaishia wapi lakini hadi nafika 15, mlio ulikuwa unaendelea bila laptop kuwaka. Inapotokea hali kama hiyo, basi ni lazima niitekenye sana ndipo finally itawaka.
The question is: are you familiar with that problem? Do yu have any recommendation... kwa maana fundi unayemfahamu anayeweza ku-deal na issue kama hii? Nalazimika kuuliza kwanza coz' siku nyuma nimeshawahi kupoteza laptop mara mbili baada ya kuzipeleka kwa fundi! Good enough, wakati huo nilikuwa na uwezo wa kupata pesa ya chapchap na kuweza nunua nyingine pindi laptop inaponifia. For the time being, mnh! So, naogopa nisije nikapeleka kwa fundi kichwa kichwa na matokeo yake ndo nikashindwa moja kwa moja hata kuiwasha kwa kuitekenya na hivyo kusimamisha shughuli zangu moja kwa moja! Kama nitapata highlights, I hope hata ninapokutana na fundi, naweza kulinganisha maelezo yako na yake hata kama hayawezi kuwa sheria! Mathalani, ikiwa unasema tatizo is probably motherboard halafu yeye anasema tatizo ni DVD Rom basi bila shaka hapo busara itakuwa ni kumwambia "okay, nitakucheki basi mambo yakishakaa level...!"
Anyway, BETTER TO BE SAFE THAN SORRY!
Fahamuni kitu kimoja tu,wale mafundi pasi,redio za mkulima na simu za siemen za mwanzo na nokia tochi -ndio mafundi wetu wa sasa wa computers,na smart phones-kwa mafundi hawa wameniulia laptop mbili,smartphone 4(za kwangu wife na mtoto)kifupi ukiwakabidhi device yako then nenda kafanye maombi irudi salama!anachokisema mkuu hapo juu ni kweli kabisa..sawa inatakiwa kama mtumiaji wa kitu chochote uwe unajua jinsi ya kutatua mambo madogomadogo..ila kwa hali ilivyo sasa huko mitaani si nzuri kila kona fundi kompyuta na ukienda na tatizo lolote lile hata kama adapter haichaji utaambiwa kuformatt..mi nlishenda sehem kununua tu kitu kingine nikakuta mtu amepeleka pc yake adapter inapga shoti wakambia inabid kuformatt..nilishangaa sana..so anachosema ni sahihi..sio wote ila wengi wa hawa vijana mitaani wanaojiita mafundi ni shida tupu..kama kweli wanania wanatakiwa kujifunza zaidi..tatizo unakuta hata mda wa kukaa kufungua tu online kujifunza vitu zaidi wengi wao ni games au picha za ajabu tu wakati wanainternet full time..
duh. mtu ameweka ram ya ddr2 5300 kwenye mobo inayo support maximum speed 4200. pc imegoma kuwaka anasema hii pc ni mbovu inachagua ram....... na ni fundi wa computer...
Mkuu sijui nini
Ahsante kwa maelezo yako! Kwa kweli hili tatizo am certain halihusiani na keyboard au hard disk... in fact, hili tatizo ninalo kwa zaidi ya miezi sita sasa na lilianza kujitokeza wakati nimeitumia for only one year! Binafsi, ninashuku hiyo hoja yako ya mwisho kwamba probably ni motherboard but I am afraid to take the risk ya kugharamia motherboard kwa fundi halafu bado tatizo linabaki pale pale!!
Tukija upande wa huo mlio, kimsingi ni kwamba ina-beep... lakini nimetumia neno kugonga coz' beeping yake inatoa sauti kali sana tofauti ni hii beeping ya kawaida! And if i have to categorize it kati ya "bip bip" na "bip bip bip", basi hiyo beep beep beep ndo yenyewe hasa. Few hours ago nilijaribu ku-visit Dell's community forum... huko nimekuata ni tatizo la kawaida kabisa kwa Dell Laptops lakini ni kama wenyewe hawajui solution ni nini unless kama wanafanya makusudi ili watu wanunue new laptops!
Mkuu Ndeshau,Athen hilo tatizo la PC yako inaeza kuepo kati ya maeneo mawili:
Kwanza, inaezakua operating system(OP) haifanyi kazi vizuri au imekufa kutokana na sababu mbalimbali kama vile virus,hard disk imekufa, uliformat pasipo kujua n.k. Jaribu kurepair au kuinstall window mpya kama ikiwezekana. Suluhisho lingne ni kubadili hard disk ikiwa imekufa.
pili jaribu pia kufuata ushauri wa #SijuiNini kuchek memory (RAM) kama zinafanyakazi au zmekufa. kama zmekufa unaeza kuzbadili kwa kuweka nyingne mpya.
kila la heri!
Hahaha! naona una bif na wazee wa kuformat kwa kila tatizo...
Watu wakikosa ajira vitu kama hivi lazima viwepo mbona, kuformat wanapiga hela maana atakuchaji hadi softwares kuinstall upya, hahaha
kweli kaka upo sahihi, but kuna watu wengi nowday hua wanajifanya ni mafundi haswa upande wa hardware hua wanaharibu sana hili suala nakutana nalo mara nyingi sana kwa upande motherboard, na husababisha hasara kubwa sana kwa mwenye mali.
MFANO, kuna baadhi ya laptop acer mini zikileta black screen hapo inabidi ku-update bios kwa utu aliye-kariri ataacha ku-repair display processor na hapo ndio unakua mwisho wa computer kumbe tatizo lilikua ni ku-update bios kwa kutumia usb so hapo tatizo linakua kubwa sana inabidi kubadili motherboard.
Ushauri. kama computer yako ina tatizo kama sio mzoefu haswa masuala ya hardware jaribu vitu vidogo kama, kufuta vumbi, kubadili ram, hdd, processor, sound card, kwa complex issues kama kubadili ic, ac, capacitor, power unit, power diode, kupima components kwenye motherboard ni vizuri hizo kazi waachiwe wenye hiyo fani il kuepika hasara.
Wenzio mamekariri DDR1 zote zinaingiliana,DDR2 zote zinaingiliana hivyo hivyo kwa DDR3 hayo ya speed hawayajui!!!duh. mtu ameweka ram ya ddr2 5300 kwenye mobo inayo support maximum speed 4200. pc imegoma kuwaka anasema hii pc ni mbovu inachagua ram....... na ni fundi wa computer...
Installation yenyewe ni fake OS?Alafu kitu kingine hawa vijana wameshusha ghalama ya kuservice computer na kuformat zamani miaka ya 2004 wakati nimetoka India kusoma hapa town kuformat computer tulikuwa tuna chaji siyo chini ya laki moja na nusu mpk laki mbili inategemea na mtu lakini siku hizi hawa watoto wanaformat kwa sh elfu tano? Jamani hata Microsoft wanasema kufanya installation isiwe chini ya USD 50 yani mpaka inauma Sana.
samahani ninaweza pata mwasiliano yakoCheap is expensive.Wengi wanapenda vitu vya bei nafuu,fundi wa computer hajui hata umuhimu wa kubackup data kama anaformat,by the way solution ya kuformat ni ya watu ambao si experts,hii ni option ya mwisho kabisa.Mtu computer ina virus kibao,antivirus yake ni ya bure na haiko updated,fundi anamwambia solution ni kuformat wakati anahitaji antivirus nzuri tu.
Endeleeni kuibiwa na kupotezewa data zenu mpaka mtakapoelewa kwanini kuna certificate,diploma ,degree na experience is the best teacher.Kuna watu nilitaka kuwafanyia kazi nikawambia 2M,akaja mwingine 1.6M sijui walimpa yeye au walipata wa chini zaidi,aka extend network yao.Siku wamepata tatizo wananiita nikakuta kazi ilifanyika ina hata termination ya cable inaonyesha ni mwanafunzi au haelewi.Within a short time nikatatua tatizo lao huku nikiwaelimisha na kuwaambia "cheap is always expensive.
Tatizo hii fani ya IT hakuna board inayosimamia kama kwa mfano wahasibu,kuna kazi huwezi fanya kama hujakidhi vitu fulani,sasa huku IT kila mtu ni IT,kila chuo kikianzishwa hakijakamilika kama hawafundishi IT(kufundisha IT si shida issue ni how competent walimu wao walivyo).
So tuendelee hivyohivyo,nyie mmeona ya mtaani tu lakini hata kuna makampuni ya IT bado wafanyakazi baadhi siyo competent.Hii ni opportunity kwako unayejiamini uko safi,just stand out of the crowd.
Njoo PM mkuu tuongeesamahani ninaweza pata mwasiliano yako