Kila kitu Makonda

Kila kitu Makonda

Ngoja nakushauri hizi itikadi zenu za kisiasa zingekuwa Zina faida kwenu zingewanufaidisha Sana mngekuwa mmefika mbali Sana kimaisha bahati mbaya zinawapumbaza akili zenu mnakuwa hampo huru kimawazo nakufikiri kila mtu anapokuwa ana mawazo tofauti na zenu mnafikiri umetoka upande mwengine wa kisiasa lakini pia zinawapotezea muda kutokana na hili mnashindwa kuongeza ufahamu mpya tofauti na unachoamini.Badilika mzee baba
Si ndio kishabadilika, sasa hivi yeye ni Harambee Stars au unataka abadilikeje? Aah, halafu nilisahau kukusalimia, shikamoo!
 
Hata shetani huwa anazungumzwa sana, jambo lolote zuri au baya hupewa shetani, hii inatokana na gundu na tabia zake.
Malaika wala hawazungumziwi na ndio tunawaamini katika vitabu vya dini ila shetani nani asiyemjuwa front page kila siku katika maisha yetu
 
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kuniambia kitu kimoja ukiona unazungumziwa Sana au unahofiwa Sana ujue una kitu special.

Nimekuwa mijadala hapa jamiiforum nimeona wakimchukia Sana makonda iwe Kuna kitu kafanya kizuri au kibaya kwao Ni kibaya na kuhusishwa kwa Mambo mengi mabaya.

Je, ni waulize huyu mtu kawafanyia Nini kawabaka wake zenu? au kawafanyia kitu gani kiasi Cha kibaya kiwe chake. Halafu cha ajabu wanaomchukia ni wanaume wenzake hii tabia ya kuchukiana bila sababu za msingi zinatoka wapi?

Kwanza kabisa ana maisha mazuri kuliko wewe unayembeza pia ana kazi nzuri inayoeleweka.Kama ishu ni vyeti feki mimi nitajuaje wewe pia ni mmoja wapo wa kuwa na vyeti feki sababu unatumia vyeti feki hizo chuki zenu kwa huyu jamaa haziwafanyi muwe matajiri tabu zenu zinabaki pale pale.
Mwambie alete vyeti.....tuanze na hilo kwanza.
Afu mwambie kasababisha Stars imefungwa jana, kilichompeleka huko ni nini kama si kututia nuksi.
 
Jamaa wanampa kiki saaana na ni mtaji mkubwa sana kwake hawa jamaa, hawajui jinsi anavyotrend ndo wanazidi kumuimarisha.
 
Lengo langu sio kila mtu ampende ila nimeona wadau wamekuwa wakimsema na kumlalamikia Kwenye sehemu ambayo sioni kosa lake na saa nyingine kumzushia Mambo mabaya mfano mtu mmoja alifungua Uzi na kusema makonda adindi nikajiuliza we umemuonaje adindi lkn pia nimeona wanamlalamikia yeye amesababisha timu ya taifa kufungwa na Kenya eti kisa tu ameenda misri utazani taifa stars inauwezo wakuwafunga Kenya wakati mara nyingi Kenya inawafunga taifa stars wewe unaona sawa kweli?tukosoe panapo stahili pia tusifie panapo itaji sifa lkn sio lazima kusifia ndo maana nzima ya mijadala yenye kujenga.

So wewe umeona ni sahihi taifa star waende uwanjani kuipigania ilani ya ccm. Ni sahihi siasa kwenye michezo? Kwa nini ccm au makonda asianzishe klabu yake ikaitwa ccm itakayopigania ilani ya chama!
Kumbuka Gharama wanazotumia taifa stars huko Misri zinatokana na kodi iliyolipwa hata na wasio CCM.

Mwisho kabisa naomba nikuulize, samahani lakini, wewe umejuaje makonda anadindisha??
 
Mkubwa, wanaomchukia Makonda ni kagenge flani hivi kadogo sana, ila katapigwa na butwaa huyu jamaa akitwaa jimbo 2020 na kuwa waziri,

Kingine watz wengi ni wapumbavu hasa hawa wanaokesha kwenye social media, ukipita mitaani watu wenye akili zao wapo busy kutafutia familia zao ugali na hao ndio hasa watakao jitokeza pia 2020 kwenda kupiga kura.

Mfano kwa hili la stars, aisee katika watu 20 nliokutana wanaongelea mpira wa jana hakuna hata mmoja aliyekuwa analaumu sijui Makonda, isipokuwa lawama hizo utazikuta kwa wapumbavu wa chache hapa jf!
 
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kuniambia kitu kimoja ukiona unazungumziwa Sana au unahofiwa Sana ujue una kitu special.

Nimekuwa mijadala hapa jamiiforum nimeona wakimchukia Sana makonda iwe Kuna kitu kafanya kizuri au kibaya kwao Ni kibaya na kuhusishwa kwa Mambo mengi mabaya.

Je, ni waulize huyu mtu kawafanyia Nini kawabaka wake zenu? au kawafanyia kitu gani kiasi Cha kibaya kiwe chake. Halafu cha ajabu wanaomchukia ni wanaume wenzake hii tabia ya kuchukiana bila sababu za msingi zinatoka wapi?

Kwanza kabisa ana maisha mazuri kuliko wewe unayembeza pia ana kazi nzuri inayoeleweka.Kama ishu ni vyeti feki mimi nitajuaje wewe pia ni mmoja wapo wa kuwa na vyeti feki sababu unatumia vyeti feki hizo chuki zenu kwa huyu jamaa haziwafanyi muwe matajiri tabu zenu zinabaki pale pale.
Mzee umepiga cha chuga nini? Huyo unaemtete hapa alishaitwa na kamati ya maadili bungeni, jiulize wale wabunge wanamuonea donge kwakuwa ana kazi nzuri kuliko wao? Marehemu ruge alishamtuhumu kwa kuvamia ofisi yake kwahiyo ruge alikuwa anamuonea wivu makonda, katibu mkuu wa ccm alishatamka hadharani kuwa makonda alienda analia kuomba radhi, kwahiyo hawa wote wanamuonea makonda?
 
Daah Gwajima,Waziri mkuu,Katibu mkuu CCM,Spika,Manji,Mbowe,Wabunge kibao,familia ya kina rizione hao wote Makonds amekorofishana nao na inaonekana hao wote niliowataja Makonda anawazidi kwa maisha mazuri.
 
Back
Top Bottom