KILA JAMBO ULIFANYALO LIFANYE KWA HAKI NA UKWELI

La Quica

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
921
2,084
Mwanamama anaingia katika bucha , muda mfupi kabla ya kufungwa bucha na anamuuliza muuza nyama:

"Una kuku?

Muuza bucha anafungua friji yake na kumtoa kuku mmoja tu aliyebaki hakukua na kuku mwingine zaidi ya huyo kuku.

Akamuweka kwenye mzani kumpima ikaonekana huyo kuku ana kilo moja unusu.

Yule mama akauliza tena

"... je hauna kuku mkubwa zaidi ya huyu tafadhali...?

Ujanja wa kibiashara na tamaa ukamuingia muuza kuku,

Akajifanya kumchukua yule kuku kumrudisha kwenye friji , halafu akajifanya anamtoa kuku mwingine na kumuweka kwenye mzani na kwa ufundi na umahiri mkubwa wa kiujanja ujanja ,alipomuweka yule kuku kwenye mzani akaweka kidole chake kwenye mzani kiudanganyifu , mizani ikasoma kilo mbili

Yule mama akaagiza "nifungie wote wawili, yule uliyemrudisha na huyu wa sasa"

Ni hayo tu kwa sasa...
 
Unaghairi tu unasema nimeamua Leo siuzi kabisa huyu aliyebaki kwenye friji ntaenda kula nyumbani kwangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom